Hao ndo marafiki zangu wa kweli nakupa kitu ilinitokea, mwaka 2017 nikiwa kwenye kazi zangu na kazi huwa naanza saa 12 asubuhi nakuwa bize sana mpaka mida ya saa 4 asubuhi napata muda kidogo wa kupumzika. Sasa ililetwa chai na best wateja wamepungua nikasema niinywe ile kunywa tu nilianguka na nilizinduka baada ya siku 3, nazinduka sijielewi nimepalalaiz upande mmoja yani sina hamu. Mume huyu huyu ndo alinihudumia na kupambana sana hapo ananihudumia huku kuna watoto mapacha. Rafiki sikuona hata mmoja zaidi ya mume na ndugu tena wa tumbo moja tu!