Watanzania wengi wakishajenga nyumba ya kuishi wanaona wamemaliza ndoto


Ahsante sana, hilo jambo muhimu sana.
 
Maendeleo kwa definition yako ni nini?

Kumbuka, pengine zaidi ya 70% ya watanganyika ni masikini. Na zaidi ya 20% ya wenye fedha za ziada, haziandikiki, yaani ni wezi na wapigaji! Pengine 10% ya wenye pesa mingi kupitiliza, ndio wakwepa kodi wakubwa, mafisadi papa, wauza ngada, watakatishaji etc.

Mtanganyika mwenye kipato halali bin haki, nyumba moja tu ya kulala, inaweza kumchukua miaka 10 kujenga na kuhamia!

Hitimisho langu kwa sasa, ni NDIO kujenga nyumba ya kuishi ni maendeleo sana tu! Watu wana mortgages za 60yrs huko duniani ili wapate pa kulala panapoitwa HOME.
 
✍️👍
 
Nyumba ni Liability kama ndoto zako ni kumiliki nyumba kwaajili ya kuishi amka amka kumekucha....

Sikuhz tunajenga nyumba alafu tunaifanya ya biashara/ nunua viwanja weka kama assets sio kwaajili ya kujenga nyumba ya kuishi matajiri sikuhz tunaishi kwenye apartments na nyumba zako unapangisha 😁
 
Ujumbe mzuri mkuu asante kwa chapuo
 
Napinga hoja zako hazina mshiko..
Sababu ukizidi kutafuta pesa kwa nguvu huenda ukaishia gerezani na hiyo nyumba wakalalia wengine.

Nashauri kwamba ukizidi kupata mafanikio especially kwa kazi za kurisk maisha,, unapaswa upunguze kasi ili usiishie pabaya..
 
Tatizo ni kwamba watz wengi tunafocus kwenye kuongeza liabilities yaani vitu vinavyotoa hela mfukoni kama gari na nyumba na si kwenye kuongeza assets.
 
Watu wenye akili za kitajiri wanatumia pesa kuongeza pesa, Akili ya kimasikini anatumia pesa kuonekana ana pesa.

Mfano hawa watu wawili wanaweza fanya kazi kwenye kampuni moja wote wakachukua mshahara wa laki5.

Mwenye akili ya kimasikini atakimbilia appartment, TV, sofa kali, Simu kali, Mavazi classic ili wengine wamuone anazo na ndiyo utakua mfumo wake forever.

Mwenye akili ya kitajiri atakimbilia kuwekeza aidha kilimo, ufugaji au biashara hata kama biashara ndogondogo huku akiamini siku1 atanunua kila anachokitamani bila kuathiri kipato.


 
Sijazungumzia kazi za kurisk.Hoja wengi wakishajenga wanaona wamemaliza hawapambani kupata uwekezaji zaidi.
 
Kupanga sio ushujaa lkn
 
Basi tukubaliane hapahapa kuanzia leo tusijenge tuishi kama machura kwenye matope!, tena ikabidi tuishi kama kamongo kwenye matope na maji!.
Hatujakataa kujenga si jambo bora,bali kwajili mtu akijenga anajiziuka na kujiona amemaliza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…