Watanzania wengi wanaotumia ATM machine kutoa pesa bado hawajui huduma ya kugusa kadi (NFC Reader) kutoa pesa wamezoea njia ya kuchomeka kadi

Nyoka kibisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2014
Posts
947
Reaction score
2,601
Ukienda benki upande wa ATM mashine kati ya wateja 10 wanaotaka kutoa pesa, labda mteja moja ndio anaweza kutumia huduma ya contactless card reader. Kwani bado watu hawajui kuwa pia unaweza kutoa pesa kwenye ATM bila kuingiza kadi yako kwenye card slot kwani wengi wamekuwa wakilalamika kadi zao kumezwa wengine kadi hazisomi.

NFC reader ni nini?

Ni sehemu ya Atm mara nyingi huwa ni upande wa kushoto, yenye alama ya mawimbi kama Wi-fi hivi, ambapo unaweka kadi au kugusisha kadi yako ili iweze kusoma.

Hatua za kufuata;
1. Gusisha kadi kwenye nembo ya WiFi kwa sekunde chache.
2. ATM itakukaribisha na kukutaka uweke PIN yako
3. Chagua huduma unayotaka, kisha subiri huduma
4. Jihudumie kisha Chukua risiti

Huduma hii ni kwenye ATM zenye nembo ya WiFi

Japo kuna Atm mashine zingine zinaruhusu kutoa pesa bila kuwa na kadi kwa kutumia simu/app au QR number.

Epuka kadi yako kumezwa tereza kibosi.
Hili sio tangazo ila nmeamua nisaidie wale ambao bado hawajui huduma hii maana jana kuna mtu nmemsaidia baada ya kupata shida kwenye kadi yake na karibia wateja waliokuwa around walishangaa hiyo huduma.

 
Pale huwa pako contaminated
 
Binafsi (kutokujua siyo ushamba) nilikuwa silijui hili ndiyo jamaa amenitoa tongotongo leo.

Kwa hiyo mleta mada nitajuaje kadi yangu ina uwezo wa kufanya hivyo,tukizingatia atm card za NMB?
Ukienda kwenye atm angalia pembeni kama ina sehem yenye alama ya mawimbi kama ya wifi angalia picha juu
 
Asante kwa elimu.
Hata mimi nilikuwa sifahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…