Ukienda benki upande wa ATM mashine kati ya wateja 10 wanaotaka kutoa pesa, labda mteja moja ndio anaweza kutumia huduma ya contactless card reader. Kwani bado watu hawajui kuwa pia unaweza kutoa pesa kwenye ATM bila kuingiza kadi yako kwenye card slot kwani wengi wamekuwa wakilalamika kadi zao kumezwa wengine kadi hazisomi.
NFC reader ni nini?
Ni sehemu ya Atm mara nyingi huwa ni upande wa kushoto, yenye alama ya mawimbi kama Wi-fi hivi, ambapo unaweka kadi au kugusisha kadi yako ili iweze kusoma.
Hatua za kufuata;
1. Gusisha kadi kwenye nembo ya WiFi kwa sekunde chache.
2. ATM itakukaribisha na kukutaka uweke PIN yako
3. Chagua huduma unayotaka, kisha subiri huduma
4. Jihudumie kisha Chukua risiti
Huduma hii ni kwenye ATM zenye nembo ya WiFi
Japo kuna Atm mashine zingine zinaruhusu kutoa pesa bila kuwa na kadi kwa kutumia simu/app au QR number.
Epuka kadi yako kumezwa tereza kibosi.
Hili sio tangazo ila nmeamua nisaidie wale ambao bado hawajui huduma hii maana jana kuna mtu nmemsaidia baada ya kupata shida kwenye kadi yake na karibia wateja waliokuwa around walishangaa hiyo huduma.
View attachment 3646413