Watanzania wengi wanaotumia ATM machine kutoa pesa bado hawajui huduma ya kugusa kadi (NFC Reader) kutoa pesa wamezoea njia ya kuchomeka kadi

Ahsante saana kwa elimu. Japo mimi sina kadi ya benki wala similiki hata mia benki siku nikijipata sitokuwa mshamba kihivyo wa kutumia kadi.
Bado naendelea na lipa namba yangu ndio kadi yangu.
 
Ahsante saana kwa elimu. Japo mimi sina kadi ya benki wala similiki hata mia benki siku nikijipata sitokuwa mshamba kihivyo wa kutumia kadi.
Bado naendelea na lipa namba yangu ndio kadi yangu.
Kila hatua dua mzee
 
Hata POS za madukani au petrol station wanatumia hii sana badala ya ku swipe card yako.
 
Hiyo niteknolojia mpya kwa bongo ,ni ya hivi karibuni kwaio huwezi fanya kitu ambacho hujui na hujawahi kufanya.
Kwenye maisha kwa kila jambo Kuna mara ya kwanza na kufundishwa.
 
ATM za zamani hazikuwa na hizo options. Mfano hii hapa.


Ila ATM za kisasa zina options nyingi ikiwemo hiyo uliyosema mleta mada.

Zingine zina mpaka options za Fingerprint na Barcode Scanning. Kama hii hapa chini.


Pia siku hizi branches zilizo maeneo Prime wameweka ATM za kudeposit mwenyewe, yani hauhitajiki kwenda ndani na kupanga foleni ili kuweka pesa kwenye account yako, ni unaenda Deposit ATM unajihudumia mwenyewe chap chap.
 
Mimi kinachonikera nikitumia hiyo huduma option ya juu inakuwa 100k ila nikitumbukiza option za kutoa pesa zote zinarudi hii imenitokea zaidi ya ATM 2 benki ni ile ya orange na blue
 
Wengi wanajua lakini makato yake ni Makubwa.
 
Hiyo sehemu kwenye atm nilikuwa naiona Ila sikujua matumizi yake, hata ile chip kwenye kadi nilijua inatumika tuu kule ndani unapoingiza card, ndo mara ya kwanza najua hili
 
Safi mkuu umetoa elimu mujaarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…