Watanzania wengi wanapenda kuwa Usalama wa Taifa

Watanzania wengi wanapenda kuwa Usalama wa Taifa

Acha uwongo. Kwanza wewe siyo TISS.

Ni mtu tu labda uliyekuwa unawaona wanakuja na kuondoka.

Tatu, Makinikia hayakua Zamcargo pekee yalikuwa mpaka TICTS ambako kote TISS na Feed Force walikuwa wanaenda.
Kaka funika kombe................. ,Umechokonolewa kidogo na wewe umechokonoka. Hii michezo haichezwi hivyo. Usimwage mchele kwenye kuku wengi..
 
Kuna mzee mmoja mwandamizi kitengo niliwai kukaa nae....

Aliniapia hato ruhusu mtoto Ake aingie huko....Na kwel nafahamu watoto Ake hakuna hata mmoja Alie fuata nyayo.....

Jamaa ni mkristo ila kipindi Cha Ramadhani ana hamia Zanzibar swala 5.....

Alinisimulia makashi Kashi mengi sana tangu ame be recruited kitengo....

Anasema walivalishaa mifuko usoni safari ika Anza......zungushwa sana mpak kujikuta kwenye msitu mnene.....
Anasema makashi Kashi ya siku za mwanzoni wali juta na walitamani kutoroka.....

Hajawai ruhusu mwanae afuate nyayo.....
Nimuongo!

Anakuzuga.
 
Unafanya kazi za kujificha ficha
Mara et unalinda wengine wanaokula na kunywa na familia zao

Naamini Kuna watu wako kwenye hiyo idara Ila WANAJUTA kwenye maisha Yao yote kuwa hukooo
Na huo ndo ukweli. Tatizo ni palee watu wanapotamani wasichokijua na hamadi Mungu akijalia yakatimia ndo inakuwa majuto kilio na kusaga meno. Ila acha waendelee TU ,maisha ndo yalivyo
 
Naomba connectiion nijiunge, ila watanzania walivyo wambea kila mtu ni usalama ha ha ha
 
Mngejua msingekuwa mnaropoka hovyo tu... kwanza TISS hawachukui watu wajingajinga na wakiona uko smart unahitaji msasa kidogo wataku-shape wanavyotaka wao.

Pia ni kazi hatari mno! Watu kila saa matumbo yanawauma kwa uoga we kalagabaho uliyefeli kila kitu maishani unadhania ni rahisirahisi tu au kila mtu anaweza kuwa kule 😊😊😊 acheni kabisa.

Alafu pia mbona nchini kuna issue nyingi tu za kuongelea na kushughulika nazo?! 🤔🤔🤔 mnaona haitoshi mnataka kupekua na mambo ya TISS pia 😃... kuna mwaka walitakaga kushughulika na JF mpaka wakamtia hatiani Mr. Melo sijui mnakumbuka?! Naona saiv imekuwa tena mada pambe humu eeh😃😃😃

Mnachokitafuta mtakipata...😊👍🏾
😅😅😅😅😅 "Mnachokitafuta mtakipata...😊👍"
 
Ukibahatika kuingia huko UTAJUTA!

Na kule huenda ambaye hata hakutarajia wala hakutaka kwenda Ila kajikuta kaenda 😊😊😊 sasa we bora endelea na shughuli zako na za kujenga nchi kwa ujumla... nakushauri achana na hiyo kitu
Haina Hata haja ya kumshauri Kama sio mmoja Wao na anatuenjoy basi Hata pata hata kunusa pua yake mpaka anakufa. "Ile Kazi haitaki kabisaa Mtu anae itaka"
 
Mimi ni usalama wa nyumba yangu, nampeleleza panya alieiba mboga jikoni kwangu.
 
Hii mada ijadilini kujifurahisha ila mjue Mambo mengi yanayoitwa Siri Ni uongo ambao hamjawahi kuambiwa au kusemwa.
Mnachnganywa na tabiri za watu na kila mtu ana yake...
Chai zimekuwa nyingi mno.
kuna vitu vinakuja machoni penu ila kuvitambua mnahitaji trained eye Kama sio awareness Kali.
 
Hata vijiweni tu anzisha mada ya Usalama wa Taifa utaona kila mmoja atakavyotiririka. Hapa kila mmoja atakuwa na aidha jamaa, ndugu au jirani ambaye ni Usalama wa Taifa.

Kila mmoja anataka kuwa Usalama... Sijui ni kwasababu ya kuishi kwenye comfort zones zetu! Kwasababu ni kazi ya Siri basi wengi wanadhania ndiyo Bora. Au kwasababu tunapenda kuonekana miamba kwa wengine!

Diwani yametokea ya kumtokea hapa jukwaani ikawa mshikemshike... kila mmoja yupo jikoni. Baada ya taarifa hii ni nyingine. Wengine wapo Makwao huko Nanjilinji ila anajua kinachoendelea Ikulu.

.............................................................
Vijana wengi wapo inspired kutoka katika movie za akina James bond na Tom cruise
 
Acha uwongo.

TISS ni Jeshi usu. Training zao physically hazizidi hata Magereza na Police. Ni mafunzo ya kawaida na matumizi ya silaha nyepesi Kama Mgambo, zimamoto, na Uhamiaji.

Pili, unaposema wanachukua watu smart, hizo ni stori zako za vijiweni tu.

Tatu, TISS wa TZ ni wa kawaida sana na utaratibu wao wa kazi unawakosesha Uhuru. Kwasababu TISS siyo taasisi ya kujitegemea, ni idara chini ya ofisi ya Rais. Hivyo wanafanya kazi zao Kama 'chawa' wa Rais.
Nami nikukosoe hakuna tofauti ya Mafunzo kimedani kati ya police na uhamiaji.

Kifupi hakuna kitu Cha police halafu uhamiaji akawa hawajui ila vipo vitu vya uhamiaji police hawaelewi.

Training ya Magereza pale kiwira ni ya kawaida wote wanafundishwa kuwa light infantry soldiers

Training ya PT pale kilele pori ni kawaida mno na zile ant tank za mwaka 47 na mabomu ya kishindo ambapo kule Ulaya zimewekwa museum.

Mgambo ndio huwa sielewi wanafundishwa nini? Au kuwa kiherehere kwenye uwanja wa mapambano.

Anyway sijui nimeandika nini?[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Nimuongo!

Anakuzuga.
Kwa faida ya nani? Ili iwejee...kifupi hajawai ruhusu mtoto wake wa kumzaa aende huko....

Kifupi hata watoto wake maisha Yao yote hakuwai kujua chochote....
Kipindi Cha uzee NDIO alianza kutupa
Ubuyu mdogo mdogo....

Alicho SEMA wao confidentiality ilikua ya Hali ya juu...alicho SEMA vijana wa Sasa alikua na taadhali nao maana wanaweza kukuuza.... Mwisho wa kunukuu....

Sijui chochote mm ni common man kama mpwayungu village
 
Walevi bar wanatusumbua sana, kila mmoja utasikia anakunong'oneza 'mi usalama wa taifa!'
 
Back
Top Bottom