Watanzania wengi wanapenda kuwa Usalama wa Taifa

Acha uwongo. Kwanza wewe siyo TISS.

Ni mtu tu labda uliyekuwa unawaona wanakuja na kuondoka.

Tatu, Makinikia hayakua Zamcargo pekee yalikuwa mpaka TICTS ambako kote TISS na Feed Force walikuwa wanaenda.
Kaka funika kombe................. ,Umechokonolewa kidogo na wewe umechokonoka. Hii michezo haichezwi hivyo. Usimwage mchele kwenye kuku wengi..
 
Nimuongo!

Anakuzuga.
 
Unafanya kazi za kujificha ficha
Mara et unalinda wengine wanaokula na kunywa na familia zao

Naamini Kuna watu wako kwenye hiyo idara Ila WANAJUTA kwenye maisha Yao yote kuwa hukooo
Na huo ndo ukweli. Tatizo ni palee watu wanapotamani wasichokijua na hamadi Mungu akijalia yakatimia ndo inakuwa majuto kilio na kusaga meno. Ila acha waendelee TU ,maisha ndo yalivyo
 
Naomba connectiion nijiunge, ila watanzania walivyo wambea kila mtu ni usalama ha ha ha
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… "Mnachokitafuta mtakipata...πŸ˜ŠπŸ‘"
 
Ukibahatika kuingia huko UTAJUTA!

Na kule huenda ambaye hata hakutarajia wala hakutaka kwenda Ila kajikuta kaenda 😊😊😊 sasa we bora endelea na shughuli zako na za kujenga nchi kwa ujumla... nakushauri achana na hiyo kitu
Haina Hata haja ya kumshauri Kama sio mmoja Wao na anatuenjoy basi Hata pata hata kunusa pua yake mpaka anakufa. "Ile Kazi haitaki kabisaa Mtu anae itaka"
 
Mimi ni usalama wa nyumba yangu, nampeleleza panya alieiba mboga jikoni kwangu.
 
Hii mada ijadilini kujifurahisha ila mjue Mambo mengi yanayoitwa Siri Ni uongo ambao hamjawahi kuambiwa au kusemwa.
Mnachnganywa na tabiri za watu na kila mtu ana yake...
Chai zimekuwa nyingi mno.
kuna vitu vinakuja machoni penu ila kuvitambua mnahitaji trained eye Kama sio awareness Kali.
 
Vijana wengi wapo inspired kutoka katika movie za akina James bond na Tom cruise
 
Nami nikukosoe hakuna tofauti ya Mafunzo kimedani kati ya police na uhamiaji.

Kifupi hakuna kitu Cha police halafu uhamiaji akawa hawajui ila vipo vitu vya uhamiaji police hawaelewi.

Training ya Magereza pale kiwira ni ya kawaida wote wanafundishwa kuwa light infantry soldiers

Training ya PT pale kilele pori ni kawaida mno na zile ant tank za mwaka 47 na mabomu ya kishindo ambapo kule Ulaya zimewekwa museum.

Mgambo ndio huwa sielewi wanafundishwa nini? Au kuwa kiherehere kwenye uwanja wa mapambano.

Anyway sijui nimeandika nini?[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Nimuongo!

Anakuzuga.
Kwa faida ya nani? Ili iwejee...kifupi hajawai ruhusu mtoto wake wa kumzaa aende huko....

Kifupi hata watoto wake maisha Yao yote hakuwai kujua chochote....
Kipindi Cha uzee NDIO alianza kutupa
Ubuyu mdogo mdogo....

Alicho SEMA wao confidentiality ilikua ya Hali ya juu...alicho SEMA vijana wa Sasa alikua na taadhali nao maana wanaweza kukuuza.... Mwisho wa kunukuu....

Sijui chochote mm ni common man kama mpwayungu village
 
Walevi bar wanatusumbua sana, kila mmoja utasikia anakunong'oneza 'mi usalama wa taifa!'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…