Mimi nina asili ya kitutsi kwa upande wa mama,baba yangu ni mzaliwa wa Msoga.
Nguvu ya nama nikapewa jina la ujombani la kwanza,kosa kubwa..
Wiki mbili zilizopita kulukuwa na zoezi la kuandikisha NiDA wilayani kwetu,wajihi wangu mrefu na hili jina nusura viniponze sema kiswahili changu ni cha mwamvaomaana nimekulia pwani ila niko huku kikazi ujombani.
Kuna mwenzangu alianbiwa atamke nne akasema ine.boksi akatamka bokisi,alipigwa pingu pale pale mpaka walipojiridhisha kuwa amezaliwa Ngara.
Kijijini kwamama asilimia 50 ni wahamiaji wa kitutsi wenyemiaka mingi sana sema wanajiita kabila la hapo wilaya walipo.
Sina lengo la kuwapinga Mamlaka ya Vitambulisho maana lazima wajiridhishe na uraia wa wanaovihitaji ila mlijua kutuchangamsha.
Kuanzia kahama,nasumbwe,runzewe,ushirombo,ngara,karagwe,,biharamulo,watutsi ni wengi sana ni kama tuko Rwanda tu.tunaishi nao na tumezaa nao,sijajua miaka 20 ijayo itakuwaje wakiamua watambulike kama kabila rasmi la Tanzania?