Watanzania wenye depression hawawezi kushirikisha watu wengine kwa sababu matatizo yao hufika mpaka vijiweni, hakuna usiri !!

Watanzania wenye depression hawawezi kushirikisha watu wengine kwa sababu matatizo yao hufika mpaka vijiweni, hakuna usiri !!

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Baada ya mlolongo wa vifo vya Depression ikiwemo cha jana usiku mwanafunzi kujirusha ghorofani niseme tu kwamba watu wanapitia mengi sana, huwa inashauriwa kufunguka matatizo yako kwa watu wa karibu kundoa machungu lakini kwa hapa bongo hali watu wengi huyatunza rohoni.

Shida ni kwamba watu wengi wanapitia kwenye depression lakini hawawezi kusema kwa watu sababu sikuiz watu wamegeuza matatizo yetu kama matangazo😢 imagine unamwambia mtu wako wa karibu jambo lako alafu kesho unaliskia kwa mwingine, kesho kutwa unakuta matatizo yako yanajadiliwa vijiweni hadi bar, mbaya zaidi wanaojadili hawana lengo la kukusaidia zaidi ya kukusimanga.

unadhani kumshirikisha mwenzako at least itapunguza matatizo kumbe yanaenda kukuzwa mara 100
 
Ndio maana wengi tuna uthubutu wa kuja kuomba ushauri jamii forum kwakua usiri ni jambo muhimu sana
Na ukitaka kujua jinsi watu walivyoathirika kisaikolojia, hata wakija humu jamii forums bado wanasingizia tatizo ni la kaka, dada, ndugu, rafiki, n.k.
 
Back
Top Bottom