Watanzania wenye uwezo kuwa CEO's wa multilateral companies tunakwama wapi? Kama Helios Towers Watanzania wameweza huko, kwingine tunakwama wapi?

Watanzania wenye uwezo kuwa CEO's wa multilateral companies tunakwama wapi? Kama Helios Towers Watanzania wameweza huko, kwingine tunakwama wapi?

Ndo umeongea nini Sasa ???
Ndiyo ujue aina ya watu walioko kwenye jamii yetu, kumbe jamii ndiyo inatakiwa ibuni mbinu za kukabiliana na changamoto zilizopo na zitakazo kuja

Society is obliged to create methods to overcome uncertainty, in reality though this type of contribution or mind set displays what type of the calibre available in our society which means we have a long way to go, towards achieving our goals of success
 
Ajira zinazolipa vizuri ni kampuni za kimataifa hizo hazijali uraia wa mtu ni hapa kazi tu ulichoandika ni nje ya mada
Pengine hujaelewa nilichokiandika rudia kusoma [sijawataja majina hapa hao watu wenye nafasi kubwa ambao wanaziongoza hizo ofisi wakiwa ni watanzani wa kuzaliwa ila kwa sasa sio watanzania tena]
Mleta mada anaongelea watanzania kuwa ma CEO wa makampuni ya kimataifa sio ya ndani kama TRA au treni ya mwendo kasi au shirika la masoko la kariakoo nk
Mashirika hayo hayo yanayopata ripoti za wizi na hasara kutoka kwa CAG mwaka huu na mwaka ujao hakuna mabadiliko?

Ni kwanini tukigusa mada ya uraia pacha watu mnaizima mapema??
 
Sisi tunaandaa chawa pekee
Chawa hawaandaliwi ni mibwege fulani hivi mitafuta vyeo serikalini na kwenye vyama kiwe tawala au upinzani ikidhani kuwa kupata vyeo unatakiwa kuwa mwimbaji na mtunga nyimbo za kusifu na kuabudu kiongozi unayedhani aweza kukubeba upate cheo

Machawa wengi ni wanakwaya watunga nyimbo tu za kusifu tu hawana lolote la maana

Kama nchi haiihitaji wana kwaya waimba nyimbo za kusifu hakuna nchi duniani huendelea kwa kwaya
 
Wewe umeongea vizuri tuu watz wenye uwezo wa ku-run business tupo wengi tuu.ila siyo kwenye taasis za serikali Siyo Zile zinazoitwa Government Business Entities "GBE"

Huko wanafundishwa coruption na wanasiasa ambao ndiyo wasimamizi wakubwa.Waziri wa wizara husika kila siku anataka apewe fedha.Hata miradi tuu ya maendeleo inakwama hapo.yaani mawaziri unawaona mqjukwani kama watu wa maana ila ni wa hovyo sana inqookuja kwenye maadili

Maahirika haya yote yanayofanya biashara
ikiwezekana hata vyuo vikuu yalitakiwa yote yasiwe chini ya wizara yoyote,ila yawe labda chini ya wizara moja tuu ya fedha chini ya Treasury Registra.
usumbufu wa wanasiasa ndiyo unaou mashirika.

Kingine ilibidi nafasi zao zitangazwe na wapewe wasimamizi huru wa usaili( Independent Hiring Consultancy company)

Vinginevyo ni ujinga mtuupu na hasara tupu.mgao wa kwenda serikalini kama faida watakuwa wanamega mtaji wala siyo faida
Wanahirisha kufikiri kizalendo a.k.a kujizima data
 
..miaka 10 ijayo utaanza kuwaona ktk hizo nafasi.

..hayo makampuni inabidi yawepo Tanzania kwa muda mrefu, na Watz wawe humo ndani wakipanda ngazi za kimajukumu.
 
..miaka 10 ijayo utaanza kuwaona ktk hizo nafasi.

..hayo makampuni inabidi yawepo Tanzania kwa muda mrefu, na Watz wawe humo ndani wakipanda ngazi za kimajukumu.
Sio kweli kuna watanzania nawajua waliomba nafasi nje ya nchi kwenye makampuni ya nje wakaajiriwa nje ziliko ofisi zao

Baadaye hizo kampuni zikataka kuwekeza Tanzania wakaletwa.kama mabosi wa Tanzania au East and Central Africa branch waajiriwa wa head office makao makuu ya kampuni ya nje wakilipwa dola head office sio Tanzania shillings sababu ajira zao sio local wameletwa tu kama branch bosses kama ambavyo angeletwa mzungu asiye raia wa Tanzania kuwa branch head wa foreign company
 
Tatizo ni uthubutu kuomba kazi kampuni za kimataifa ndio maana hata Pascal Mayala anayejiita mwandishi wa habari nguli uswahilini Tanzania anaishia tu kuandika vihabari uchwara vya ndani ya nchi vyombo vya habari vya ndani hajawahi ajiliwa BBC au Voice of America nk kama akina Kikeke nk
Ni kweli, mimi kiukweli uzalendo ndio umeniponza, nimeoa 1995, couple yetu wote ni wanahabari, 1996 tukatinga Bush House, London nikapewa offers, UK nikaona kumenikalia kushoto nikarudi Bongo.
1998 tukatia timu US, tukatinga VOA, nikaona US kumenikalia kushoto, wife na family wakabaki kule mimi nikarejea Bongo.
Sijawahi kuomba kazi foreign media.
Ila mimi sijiiti nguli bali kweli ni nguli, 34 years newsroom si haba, na habari ninazoandika sio vihabari ni habari, na kiukweli habari zangu zinalisaidia sana taifa kwasababu sindano zangu nadunga kwenye kichwa!.
Wenzie wamestaafu vyombo vya habari vya kimataifa wanalipwa monthly pensions kwa dola yeye anauza sura tu jamii forums na vigazeti vya uswahilini
ni kweli ila siandikii vigazeti, naandikia magazeti 6, Redio 5, TV 8 na blogs 5 vyote ni mainstream media.
P
 
Hapa tunao Chawa tu

Halafu wanajiita wasomi. Ndio nnapo choka. Ukiwa na mawazo mbadala, badala ya kujibiwa kwa hoja na kuelimishana, unaonekana ni mtu asiyestahili kuwepo.
Huyu ibilisi ipo siku atacheza nao dansi, wale wote ambao wanatumia vibaya nafasi zao, kutaka kutumainisha sisi sote hatuna akili, isipokuwa wale waliochaguliwa na kupewa dhamana tu. Hata kama akili hawana zaidi ya uchawa na ubabe wa kuyamazisha kila aina ya fikra mbadala
 
Sio kweli kuna watanzania nawajua waliomba nafasi nje ya nchi kwenye makampuni ya nje wakaajiriwa nje ziliko ofisi zao

Baadaye hizo kampuni zikataka kuwekeza Tanzania wakaletwa.kama mabosi wa Tanzania au East and Central Africa branch waajiriwa wa head office makao makuu ya kampuni ya nje wakilipwa dola head office sio Tanzania shillings sababu ajira zao sio local wameletwa tu kama branch bosses kama ambavyo angeletwa mzungu asiye raia wa Tanzania kuwa branch head wa foreign company
'Hawakurogwa au kupigwa majini? Wako wapi hao watu maana tuna allergy na watu wanaopenda kutumia akili zao kufikiri
 
Nepotism, Subordination vyote katika mfumo wa Kleptokrasia.

Watanzania walosoma nje wapo wengi tu lakini kwa mfumo huu hawawezi kufanya kazi Tanzania.
 
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo.

View attachment 3110071
Huu ni muendelezo wa sisi Watanzania kujitathmini uwezo wetu wa uongozi kwenye corporate level, jee Watanzania tuna uwezo wa kuongoza makampuni makubwa profitability, kama ATCL, SGR, TAZARA etc na yaka oparate kwa faida.

Kampuni ya Helios Towers Tanzania ni Kampuni ya kimataifa ya Uingereza, iko kwenye nchi 8 barani Afrika na Oman Arabuni. CEO wa Helios Towers ni Mtanzania, Gwakisa Stadi ambaye pia ni Boss wa Helios Towers Kanda ya Afrika Mashariki. Kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Helios Towers wapo, Ma CEO 3 ni Watanzania na habari njema zaidi ni hata CEO wa kwanza aliyeanzisha Helios Towers Oman, ni Mtanzania!.

Huu ni uthibitisho kuwa Watanzania tunaweza!. Kama Watanzania wameweza kwenye Helios Towers, huko kuingine kote Watanzania tunashindwa nini?.

Paskali
Huwezi kuvuna potential za watu na kuzitumia ipasavyo kwa kuendekeza uchawa na mambo ya kipuuzi ya ccm ya zidumu fikra za mwenyekiti wa mbogamboga , ni foolishness
 
ni kweli ila siandikii vigazeti, naandikia magazeti 6, Redio 5, TV 8 na blogs 5 vyote ni mainstream media.
P
Hizo ulizotaja ni main foreign media za nchi gani au ni local media ?Hebu fafanua moja moja kuwa hii ni main media ya nchi gani? Kwenye hizo umetaja au unaandikia tu vi local media vya Tanzania
 
Sio kweli kuna watanzania nawajua waliomba nafasi nje ya nchi kwenye makampuni ya nje wakaajiriwa nje ziliko ofisi zao

Baadaye hizo kampuni zikataka kuwekeza Tanzania wakaletwa.kama mabosi wa Tanzania au East and Central Africa branch waajiriwa wa head office makao makuu ya kampuni ya nje wakilipwa dola head office sio Tanzania shillings sababu ajira zao sio local wameletwa tu kama branch bosses kama ambavyo angeletwa mzungu asiye raia wa Tanzania kuwa branch head wa foreign company

..ni kweli wako Watz wengi ktk nchi na makampuni mbalimbali nje ya nchi.

..ninachojaribu kusema ni kwamba idadi yao itakuwa kubwa kwa kiwango anachokifikiria mtoa mada / Pascal ktk miaka 10 inayokuja.

..kwamba sasa hivi vijana wetu wengi wanapanda ngazi na muda si mrefu watakuja kuwa mabosi.
 
Nenda YouTube utaona watanzania wanavyodadavua maswala ya biashara na investments mpaka utajiuliza sasa huyu mjomba mbona sio sehemu ya maamuzi ya nchi.

Shida ni siasa na madaraka ya mawaziri, mamlaka ya teuzi na raisi. Hao watu hawafiki huko kwa merit (proper succession planning) na wao hawajui who to appoint. Ndio shida ilipo.

Lakini kuna watanzania wengi sana wana uwezo, msemaji wa UTT HAMIS, Mwigulu, Nehemia, Kafulila na watu wengine wa hovyo awamfikii hata robo ukimsikiliza yeye na wao.
 
Kwenye telecom, hakuna blablabla, kama serikalini, huku issues zinatafutiwa solutions, anayeleta madudu anaadhibiwa fasta, maana ukiruhusu madudu, unakosa mapato,kampuni inakufa, kila mfanyakazi, anajua juhudi zake kuhakikisha hakuna fuckups, ndio kampuni inasonga mbele,
Serikalini, kwanza kuna politics nyingi, mtaani kwangu, senior retired civil servants, hawalipi bill za maji, wala umeme, wanatumia bureeee, serikalini, hata usipojishughrisha Sana, salary will come, ukitibua Sana, unahamishwa tu, hakuna "owner ship" Ya task Fulani, madudu y akitokea, hujui nani atumbuliwe, kuna mlolongo mreeefu wa protocali!
Telecom, kuna clear standard operation procedures SOP, ikitokea shida tu, aliyechemka, anaanza kuwajibika, kurekebisha, kabla Mambo hayajawa mabaya!
Tatizo linaweza likatokea kwenye mnara Kyelwa mrongo border, inaweza ikawa issue ya pesa kibao, itasoviwa kwa conference call btn wahusika, hakuna eti MTU atoke Dar aende ziarani kagera, kote huko kuna watendaji, mnazungumza kupitia conference call, aliyechemka, anapata adhabu halo halo, kama kibarua kinaota nyasi, ni, hapo hapo uamuzi, unatoka,! No time to waste
Na sisi tulioko private sectors, siku unaenda serikalini, wallah utarogwa..!! mtu ushajizoelea kujiwekea targets za siku, wiki, mwezi, mwaka etc. na unazimaliza. Huko serikalini, ikifika hatua target yako moja au zaidi inahitaji mtu nje ya wewe kwenye hatua fulani, hapo ndo utakwamia.
 
Back
Top Bottom