Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Kwani alikufata kukuomba pesa akamlipie mwanae ada?ungempa ukweli hapo hapo kuliko kuja kumsema humu . Nafikiri kila mtu apambane na hali Yake.
Halafu sijui kama unazijua kweli kayumba,uko kayumba hali ni mbaya kweli kweli usiwasikilize wanasiasa kwamba wameboresha elimu uko.
 
Kusoma kayumba kuna faida zake na hasara na pia kusoma EM kuna faida na hasara.
...
NB: Nimesoma zote kwa vipindi tofauti
...

Anayoyaeleza mtoa uzi yuko sahihi 90% huenda 10% hayuko sahihi, kwa vipato vya wazazi wengi(sio wote) wa kibongo kusomesha EM ni changamoto na maumivu kwani anaishia kukopa,kuuza vitu ili mtoto asome, ni faida kwa mtoto endapo atakuwa ana bright mind wale fast learner, usijidanganye wote wanaosoma medium wanakuwa average ety unawapindua, kuna madogo wapo very bright sample za kina Isaac newton kabisa.
Lakini pia kama mtoto hana uwezo mzuri wa kunasa masomo anapata mtindio effect yaani umesoma medium lakini ana uwezo mdogo kuzidi hata wa kayumba.
 
Mtoto akishaelewa kiingereza na kuwa na ufahamu mkubwa,inakuwa rahisi kwenda skondari yeyote.Wazazi wengi wamegundua shida ni kiingereza,huna haja ya kumpeleka tena sekondari za kulipia ghali.
Hata interview nyingi za KAZI zinaendeshwa kwa kiingereza.Imekuwa kipengele Sana watu kujieleza vizuri hata kama Wanajua. Kinachotafutwa ni kumpa mtoto msingi imara.Kwangu mimi Ni Bora akasoma Kayumba secondary.
 
Hivi unajua pale Udsm wanafunzi wengi wametokea Kayumba?

Alafu Kayumba Akiwa kichwa ujue ni kichwa kweli.

Mchukue kichwa wa Kayumba aliyepata One ya 7 alafu mchukue wa St. Aliyepata one ya 7 waweke waparangane Uone kama huyo wa St ataambulia chochote.

Pale Udsm au nenda Mzumbe Waliosoma EM hupata wakati mgumu Sana kukabiliana na mazingira ya chuoni.
Mkuu me naona wa medium akiwa kichwa na wa kayumba akawa kichwa, utakuta wa kayumba anamzidi social skills
kama kujiamini,kuongea na watu,kukabili changamoto n.k wa medium mara nyingi anakuwa na academic skills tu, hana social skills. Hivyo anapotea maana anajikuta mjuaji, lakini pia ana uoga uoga kama ndezi na chuo ukipeleka undezi/ujuaji hutoboi
 
Upo sahihi kabisa mkuu yani wanajitesa na kuwatesa watoto wao ili kuprove Kwa watu kwamba wao matajiri..

Huyu shoga yangu shule imefunguliwa mtoto wake yupo nyumbani haendi shule Kwa sababu ada hana wenzake wanaenda shule ya Kayumba nzuri tu Tena ina geti wanafurahia ila yeye yupo nyumbani amekaa tu Sasa hivi anamkomalia mama Ake ampeleke kwenye shule hiyo ya wenzake
Ni issue ya ushamba tu.
Si dhambi kusomesha mtoto shule binafsi ila ikifika wakati unakopa, unajibana kula ili ulipie ada wewe huna akili timamu
 
Mkuu me naona wa medium akiwa kichwa na wa kayumba akawa kichwa, utakuta wa kayumba anamzidi social skills
kama kujiamini,kuongea na watu,kukabili changamoto n.k wa medium mara nyingi anakuwa na academic skills tu, hana social skills. Hivyo anapotea maana anajikuta mjuaji, lakini pia ana uoga uoga kama ndezi na chuo ukipeleka undezi/ujuaji hutoboi
100% Fact
 
Halafu kuna ile kauli hasa mademu mnayo utaskia "mtoto wangu hawezi ishi Kama nlivyoishi" nitapambana...SAWA Ila sasa anayesema hivyo anauza uji mtaji 5k.
 
Unaota unajua ushindani wa mtu kujiunga na UDSM? Lazima mtoto.awe amefaulu sana Form four na form six kwa mpigo

Wengi wa kayumba huwa si rahisi kuingia UDSM sababu ufaulu wao huwa kiwango cha chini sana form sababu ya msingi mbovu wa kiingereza wanaishia tu kusoma vyuo vikuu vingine vya kata sio UDSM
Get this in your head. EM na Kayumba wakitoka UDSM wote ni UDSM products. Nobody gives a fvck where they went in Primary school.
 
Unajua mtoto anauma eeeee. Just imagine katoto kako kananyanyasika mtaani hadi kanakonda kakiona vigari vya njano vinawabeba wenzake waende shule.. hata kama wewe una ka Vitz kako unampeleka hapo kayumba, lakini yeye bado atatamani school bus... mbaya zaidi vitoto vya hizo miedium vinacheza kwa kiinglish muda woteee.. ... katoto kako kanakodoa macho tu... hakana raha mtaani, hakana raha nyumbani, kanatamani kangezaliwa kwa jirani. Hapo ndipo utakuta Mzazi anaamua kujitosa... kama mbwai na iwe mbwai wote watasoma huko huko kwenye kingereza cha kucheza na wenzao. Labda muishauri serikali ya government yenu ibadilishe mitaala, iweke na skulibasi. KUNA WALIONIELEWA
Hivi vitu vinawasumbua nyinyi wazazi. Mtoto wala habari hana labda mtoto wako lama amashinda njaa. Ila mengine ni mizigo mnajipqchika wazazi wa dotcom
 
Hata interview nyingi za KAZI zinaendeshwa kwa kiingereza.Imekuwa kipengele Sana watu kujieleza vizuri hata kama Wanajua. Kinachotafutwa ni kumpa mtoto msingi imara.Kwangu mimi Ni Bora akasoma Kayumba secondary.
Kweli kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom