English medium social skills wanazo ila kwa watu wa class yaoMkuu me naona wa medium akiwa kichwa na wa kayumba akawa kichwa, utakuta wa kayumba anamzidi social skills
kama kujiamini,kuongea na watu,kukabili changamoto n.k wa medium mara nyingi anakuwa na academic skills tu, hana social skills. Hivyo anapotea maana anajikuta mjuaji, lakini pia ana uoga uoga kama ndezi na chuo ukipeleka undezi/ujuaji hutoboi
Watu wao wa karibu wa kucheza nao ku socialize ni watoto wa wabunge mawaziri,wafanyabiashara wakubwa nk hupeana happy birthdays nk
Huwezi waona wana socialize na maskini ndio maana huwaoni huko mitaani wakicheza rede kama watoto wa uswahilini na hata kuoa au kuolewa wanaenda na class yao sio ya uswahilini
English medium ni njia mojawapo ya kupandisha class ya mtoto.aondokane na uswahiliswahili wa mitaani