Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Kwani alikufata kukuomba pesa akamlipie mwanae ada?ungempa ukweli hapo hapo kuliko kuja kumsema humu . Nafikiri kila mtu apambane na hali Yake.
Halafu sijui kama unazijua kweli kayumba,uko kayumba hali ni mbaya kweli kweli usiwasikilize wanasiasa kwamba wameboresha elimu uko.
 
Kusoma kayumba kuna faida zake na hasara na pia kusoma EM kuna faida na hasara.
...
NB: Nimesoma zote kwa vipindi tofauti
...

Anayoyaeleza mtoa uzi yuko sahihi 90% huenda 10% hayuko sahihi, kwa vipato vya wazazi wengi(sio wote) wa kibongo kusomesha EM ni changamoto na maumivu kwani anaishia kukopa,kuuza vitu ili mtoto asome, ni faida kwa mtoto endapo atakuwa ana bright mind wale fast learner, usijidanganye wote wanaosoma medium wanakuwa average ety unawapindua, kuna madogo wapo very bright sample za kina Isaac newton kabisa.
Lakini pia kama mtoto hana uwezo mzuri wa kunasa masomo anapata mtindio effect yaani umesoma medium lakini ana uwezo mdogo kuzidi hata wa kayumba.
 
Mtoto akishaelewa kiingereza na kuwa na ufahamu mkubwa,inakuwa rahisi kwenda skondari yeyote.Wazazi wengi wamegundua shida ni kiingereza,huna haja ya kumpeleka tena sekondari za kulipia ghali.
Hata interview nyingi za KAZI zinaendeshwa kwa kiingereza.Imekuwa kipengele Sana watu kujieleza vizuri hata kama Wanajua. Kinachotafutwa ni kumpa mtoto msingi imara.Kwangu mimi Ni Bora akasoma Kayumba secondary.
 
Mkuu me naona wa medium akiwa kichwa na wa kayumba akawa kichwa, utakuta wa kayumba anamzidi social skills
kama kujiamini,kuongea na watu,kukabili changamoto n.k wa medium mara nyingi anakuwa na academic skills tu, hana social skills. Hivyo anapotea maana anajikuta mjuaji, lakini pia ana uoga uoga kama ndezi na chuo ukipeleka undezi/ujuaji hutoboi
 
Ni issue ya ushamba tu.
Si dhambi kusomesha mtoto shule binafsi ila ikifika wakati unakopa, unajibana kula ili ulipie ada wewe huna akili timamu
 
100% Fact
 
Halafu kuna ile kauli hasa mademu mnayo utaskia "mtoto wangu hawezi ishi Kama nlivyoishi" nitapambana...SAWA Ila sasa anayesema hivyo anauza uji mtaji 5k.
 
Get this in your head. EM na Kayumba wakitoka UDSM wote ni UDSM products. Nobody gives a fvck where they went in Primary school.
 
Hivi vitu vinawasumbua nyinyi wazazi. Mtoto wala habari hana labda mtoto wako lama amashinda njaa. Ila mengine ni mizigo mnajipqchika wazazi wa dotcom
 
Hata interview nyingi za KAZI zinaendeshwa kwa kiingereza.Imekuwa kipengele Sana watu kujieleza vizuri hata kama Wanajua. Kinachotafutwa ni kumpa mtoto msingi imara.Kwangu mimi Ni Bora akasoma Kayumba secondary.
Kweli kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…