Watanzania wenzangu tuanze kuweka akiba ya vyakula ndani

Una familia kweli wewe kwa uoga huu?
 
Ila we nawe acha Basi..nyuzi zako za leo ni za majanga tu
 
Nilenda njombe mwaka huu njombe vijjini kununua mahindi wakat wa mavuno kwenye mwezi wa kumi .akat nanunua kuna mama mmoja akasema mwangu kama utaweza kuhifadhi haya mahind yatapanda sana bei sisi wenyewe haijawahi tokea mahindi msimu wa mavuno yanunuliwe kwa 10000. ndio mara ya kwanza akasema na dhani kuna uwezekano kukawa na uhaba mkubwa sana wa chakula : akasema nauza kwasababu ya shida tuu mwanangu ila mwaka sio wakuuza sanachakula :so unachokisema inaweza kuwa sahihi: na njombe ndio wafalme wachakula kingi na mazao mengi sana kwa hapa Tz
 
Nchi hii imebarikiwa sana, ni bahati mbaya tumeshindwa kuitumia, mahindi mabichi yameanza kukomaa baadhi ya maeneo, mipunga ya umwagiliaji tumeanza kula, mvua zinanyesha kwa fujo, Bei ya mazao zimefanya kila mmoja aingie shambani, mwakani vyakula ni vingi na Bei zitashuka
 
Jamaa kaandika kwa hisia sana hata kupoteza kuaminika kwa mawazo yake. Nikuondoe hofu. Dunia haitaangamia kwa njaa bali kwa moto wa kibiriti. Hivyo kuwa na hofu ya dhambi na siyo njaa.
 
kwakweli lakini ngoja tulime tena mwakani bei juu tena mana hakuna kilichopunguwa kwenye pembejeo mbegu zimepanda toka 12000pakiti ya mbegu za mahindi hadi 16000-19000twafwa.
 
kwakweli lakini ngoja tulime tena mwakani bei juu tena mana hakuna kilichopunguwa kwenye pembejeo mbegu zimepanda toka 12000pakiti ya mbegu za mahindi hadi 16000-19000twafwa.
Kweli shujaa nunda
 
Jamaa kaandika kwa hisia sana hata kupoteza kuaminika kwa mawazo yake. Nikuondoe hofu. Dunia haitaangamia kwa njaa bali kwa moto wa kibiriti. Hivyo kuwa na hofu ya dhambi na siyo njaa.
Kwa hali inavyoenda soon itakuwa vita ya nyukilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…