Tetesi: Watanzania zaidi ya milioni 50 wanakosa Lishe bora UN wabainisha.

Tetesi: Watanzania zaidi ya milioni 50 wanakosa Lishe bora UN wabainisha.

Mtambachuo

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
2,919
Reaction score
5,558
Ndugu zangu kama ripoti ya UN ni kweli basi bado Tanzania tuna umasikini mkubwa na naweza kukubaliana nao kwa sababu ni familia chache sana Tanzania zinazoweza kupata mboga za majani na matunda angalu kwenye mlo wa mchana na usiku au tuseme milo angalau miwili kwa siku bila kujali muda.

Vyakula kama Samaki, Nyama, Maziwa na Mayai kwa familia nyingi ni kama anasa. Kwa kiasi kikubwa watu wanakula wanga asubuhi mpaka usiku na ndio maana uzito uliokithiri na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari yanaongezeka kwa kasi.

Suala la umasikini wa kipato kwenye kaya ni mkubwa. Nakumbuka hata Makamu wa Raisi mstaafu akiwa Waziri wa Fedha na Mipango kipindi cha Magufuli Philip Mpango alisema wazi kuwa pamoja na kuingia uchumi wa kati bado Watanzania wengi hasa viijini wanaishi kwenye umasikini uliokithiri.

Wale wapiga mapambio Lucas Mwashabwa, Tlaatlaa na yule mlowezi wa Dodoma tokea Mbeya sijui Songwe waje wakanushe.
 

Attachments

  • IMG-20260817-WA0000.jpg
    IMG-20260817-WA0000.jpg
    143.6 KB · Views: 14
Hiyo ni watu wa mikoani sisi wa dasalama haituhusu tunakulaga utumbo, firigisi na miguu ya kuku vina protini nyingi
 
Msigwa ajiandae kukanusha. Ila ni ukweli tuna kula uchafu ni vile tumezoea.
 
Hiyo ni watu wa mikoani sisi wa dasalama haituhusu tunakulaga utumbo, firigisi na miguu ya kuku vina protini nyingi

Ahaaa haaa mboga za majani na matunda unakula mara ngapi kwa siku?

Je utumbo, firigisi na miguu ya kuku ni Protein iliyobora? hata mjini bado umasikini upo wazi kabisa.
 
Ngoja msigwa aje tunamsubiri

Aje akanushe kwa data kwa sababu udumavu kwa watoto wa chini ya miaka mitano ni zaidi ya asilimia 30, ukondefu ndio usiseme, upungufu wa madini chuma/ damu miongoni mwa mama wajawazito ni mkubwa bado.
 
Ukimuliza mtu mara ya mwisho we kula samaki wa
Kuvuliwa baharini lini?atakuambia nna miaka hata 6 sijamtia mdomoni 😄

Ova
Kabisa ni walio wakavu ambao ubora umepungua na hata hao ni baada ya mwezi mzima

Samaki wabichi anawasikia na kuwaona kwenye TV.
 
Hapo sasa, ulizia kipato cha familia ya mtanzania ni kiasi gani kwa siku.
Zamani mboga mwokozi ilikuwa maharage,dagaa ila hko sahv kushakuwa pa moto
Samaki wa baharini ndiyo usiguse wanakula matajiri na watu wenye mahoteli
Sahv lbd watu wakomae na ugali tembele nyanyachungu 😄

Ova
 
Hao mabebelu wanatuonea wivu sisi watanzania tuna afya yakutosha na vyakula vingi hasa mahindi na maharage,yawezekana UN wameona picha za wanachi wa sudan (in msigwa voice)
 
Zamani mboga mwokozi ilikuwa maharage,dagaa ila hko sahv kushakuwa pa moto
Samaki wa baharini ndiyo usiguse wanakula matajiri na watu wenye mahoteli
Sahv lbd watu wakomae na ugali tembele nyanyachungu 😄

Ova

Ni hatari sana ndugu na ndio mlo wa watu wengi hapa mjini. Akila mihogo saa 4 asubuhi, jioni anakula ugali nyanya chungu siku imepita.
 
Back
Top Bottom