Watarajiwa wa ajabu!

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Mwaka jana kuna rafiki yangu ailkutana na msichana mmoja aliyesoma nae!Kwa muda msichana alimganda sana mshkaji na "I LOVE YOU" kibao.Mwezi uliopita mshkaji anaambiwa hivi unajua fulani kaolewa juzi?
Si zaidi ya miezi miwili kuna mshkaji wangu nae alikua ananiimbia nyimbo hizo hizo..leo ananiambia nijiandae kwa kadi ya harusi.

Nikajiuliza sasa hawa watu hua wanawachukulia vipi hao wachumba wao?Watu wengine kua nao ni hasara tu kwa kweli.Nawaonea huruma watarajiwa wao!Mungu awape ujasiri!
 
alikuwa anatafuta mchumba...ungekubali pengine wewe ndio ungekuwa mke mtarajiwa....just an assumption.
 
alikuwa anatafuta mchumba...ungekubali pengine wewe ndio ungekuwa mke mtarajiwa....just an assumption.

Ndani ya miezi miwili ameshampata na kutambua kwamba ndie na kutangaza ndoa??Kwa mazingira aliyomo sidhani!Ila ngoja ntamuuliza!
 
Kuna watu wengine huwa wanaona wenzao kama makaratasi vile anachezea feeling zako jinsi anavyojisikia bila kujali utajisikiaje

....tena karatasi yenyewe ile ya chooni (toilet paper)...akishamaliza kuitumia wala haiangalii..
ana flush iende zake huko!
 
...aaaah,
mimi wala siwalaumu.
"I love you!" na "Am In-Love with you!" zina maana mbili tofauti.:whistle:

Oh come on..sijaleta neno kwa neno kwahiyo hiyo tofauti tuiweke pembeni!Au inawezekana anaeoa/olewa nae akawa sio wa "In love with" bali wa "I love you?"
 
Kuna watu wengine huwa wanaona wenzao kama makaratasi vile anachezea feeling zako jinsi anavyojisikia bila kujali utajisikiaje

Embu fikiria kama kwenye maandalizi ya kitanzi tu watu hawana uaminifu hizo ndoa wanazozitaka ndo wataziweza kweli??
 
Kuna watu wengine huwa wanaona wenzao kama makaratasi vile anachezea feeling zako jinsi anavyojisikia bila kujali utajisikiaje

It goes both ways TF, unaweza fikiri unamchezea kumbe nae ana same thought.
It is a matter of being outsmarted.
 
nafikiri tatizo lilikuwa kwako..wewe hukuweza kusoma alama za nyakati. Inawezekana mchumba wako alikusoma, akaona hauko tayari kwa ndoa, na yeye asingeweza kusubiri mpaka uwe tayari...

Pia, inawezekana sio chaguo la Mungu kwa ajili yako, cha kufanya ni kumshukuru Mungu na kusubiri kwa hekima..
wakati mwingine hizi nafasi za kuoa na kuolewa ni nadra sana, pamoja na matatizo ya ndoa,
 
chezeaa alarm...zikilia yeyote utakayekutana nae, akili inasema sasa nataka mwenza tu. Atazungukia wote aliokuwa nawaadmire, atakayekubali kusema I do ndio huyo.

You are so right!Watu wanacheza sadakalawe na ndoa!!Alafu baadae wanakuja kulia ningejua ningejua!Arrgg!
 
Embu fikiria kama kwenye maandalizi ya kitanzi tu watu hawana uaminifu hizo ndoa wanazozitaka ndo wataziweza kweli??

you can't justify..huwezi kujua watawezana vipi! ni kuwaombea tu, wawe na maisha mema..
 
Hakua mchumba wangu Mpendwa na namshukuru Mungu kwa hilo!
 
Embu fikiria kama kwenye maandalizi ya kitanzi tu watu hawana uaminifu hizo ndoa wanazozitaka ndo wataziweza kweli??
Sijui niseme inakera sijui niseme inasikitisha hata sielewi yaani mimi nachoka kabisa
 
Oh come on..sijaleta neno kwa neno kwahiyo hiyo tofauti tuiweke pembeni!Au inawezekana anaeoa/olewa nae akawa sio wa "In love with" bali wa "I love you?"

...haya bana, niwie radhi. Mkono umeteleza!

Mbu how was ur easter?

...indoors bro! Debit na Credit cards zangu zinakuwa more safe kwenye friji!
temptations nyingi huko nje, LOL...
:focus:

...mtu akikutenda namna hii, halafu baada ya siku mbili tatu kinawaka huko kwenye ndoa yake utamuona mbio anakujia
'a shoulder to cry on!' Kazi kwako ukiamua kuwa 'Doormat' lake!

Anyway, tunashauriwa kuwaombea mungu huko waendako.
Jipe moyo..."Kila likuepukalo,....!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…