Watasalimika wangapi?

Watasalimika wangapi?

Kwenye Kipindi changu chote kwenye Tasnia hii ya habari sikumbuki siku nyingine zaidi ya siku ya Jana ambapo ndipo nilipoona Taifa likisimama pamoja kwa lugha moja na kwa kupaza sauti moja. Sauti iliyokuwa ikisika kutokea pande zote za Nchi ilikuwa, "Haki itendeke kwa Bw. Mohamed Ali Kibao". Mzee Ali alikuwa kiongozi wa CHADEMA, Bahati mbaya kurasa zake za uhai zimefungwa kikatili baada ya Uhai wake kufisadiwa na kuporwa na wale "wasiofahamika", katika hali isiyoweza kusimulika kirahisi.

Leo Jumatatu Mzee Kibao atapumzishwa kwenye makazi yake ya Milele, nyuma akituachia Maswali mengi, hofu, wasiwasi na uoga unaofunikwa na fukuto la kutaka kuona hatua zikichukuliwa kwa wote wanaohusika na tukio hilo la kinyama.

Kauli ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa jana jioni kupitia mitandao yake ya kijamii akiagiza mamlaka hususan vyombo vya uchunguzi kumpatia taarifa ya kina kuhusu mauaji ya Mzee Kibao imeamsha hisia nyingine mpya ya kutaka uwajibikaji zaidi miongoni mwa wale wanaoonekana kushindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu.

"Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi, serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vua kikatili vya namna hii.", Ujumbe wa Rais ulisomeka.

Wengi wa watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaamini kuwa kauli ya Rais Samia haitoshi, ilihali bado Waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni, Mkuu wa Polisi ya Tanzania IGP Camillus Wambura na Kamishna wa operesheni na mafunzo Awadh Jumbe, wote wapo Maofisini. "Wote wajiuzulu kutokana na wimbi la utekaji na mauaji ya raia nchini", wamesema watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii.

Ismail Jussa Mwanachama wa ACT Wazalendo amenukuliwa akisema "Uchunguzi huru wa kimahakama (Independent Judicial Inquiry) tu tena uwe HURU hasa ndiyo unaweza kutupa ukweli kuhusu matukio haya ya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini. Na wakati tunasubiri hatua hiyo, hawa wawili (Masauni na Wambura) wanapaswa kuondolewa bila ya kuchelewa kwa kushindwa kazi!"

Mtumiaji wa mtandao wa X aliyejitambulisha kama Luhaga Mpina amechapisha andiko lake akisema, "Tweet hii ( Ya Rais Samia) ingependeza zaidi kama ingeambatana na utenguzi wa mara moja wa Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni na IGP Wambura. Watu hawa wanatia doa baya kwenye uongozi wako. Vitendo vya kutekana na kutishana vimetamalaki mno hali inayoleta hofu kwa Watanzania."

Martin Masese naye kupitia ukurasa wake wa X amesema "Kama kweli RAIS @SuluhuSamia angelikuwa ameumizwa na kukereka na tukio la Mzee #AllyMohammedKibao kutekwa, kuteswa, kuuuwawa na kutupwa UNUNIO, tungeona hadi muda huu kuna watu wamewajibishwa akiwepo MASAUNI. Huwezi kuwa WAZIRI wa mambo ya ndani watu wanatekwa na kuuwawa. NO.

Aidha katika hatua nyingine, baadhi ya wananchi wametaka uboreshaji wa mfumo wa utendaji wa Jeshi la Polisi, wakiamini kuwa hatua hiyo ndiyo itakayoiweka Tanzania na Raia wake kuwa salama kwa kuondokana na vitendo vya mateso, udhalilishaji, ukandamiza, mauaji na utekaji unaoonekana kushamiri kwa siku za hivi karibuni.

Bw. Onesmo Mushi, mtumiaji wa Mtandao wa X anasema "Kuwa na independent oversight body mwenendo wa jeshi la polisi nayo ni kupoteza muda tu. Unaoversee nini ili ureport kwa nani afanye nini? As long as tutaendelea kuwa na jeshi linaloapa kutii amri za watawala, haya matukio hayawezi kuisha.

..... So long as tutaendelea kuwa na katiba inayomfanya Rais kuwa Mungu mtu, polisi wataendelea kutumika kulinda dola tu. Hata ukifanya overhaul ya jeshi zima la polisi leo na kuintroduce structure mpya, bila kugusa madaraka ya kimungu aliyopewa Rais ni kazi bure.

Bw. Onesmo amepingana na Kiongozi mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo Bw. Zitto Kabwe ambaye awali alichapisha taarifa yake akisema "Tume huru ya uchunguzi, Presidential Commission of Inquiry, kwa mujibu wa Sheria ndiyo njia sahihi, bora na ya kuaminika kupata ukweli wa tukio hili na mengine kama hili."
20240910_071314.jpg
 
1.Unamteka mtoto wa kike kwa mtutu wa bunduki

2.Kundi la wanaume saba wakatili mnakubali kwenda kumteka, kumdalilisha, kumnyanyasa na kutweza utu wa mwanamke kwa ujira wa fedha?

3.Mnafunga kitambaa usoni mwanamke kisha mnamtoa nyumbani kwake Kibiti mnamsafirisha hadi mapori ya Kisarawe kwenda kumnyanyasa na kumfanyia ukatili

4.Mnajitambulisha kuwa ni maafisa wa chombo cha dola kisha mnatumia gari la kodi za wananchi, pingu na bunduki zilizonunuliwa kwa kodi zetu.

5.Mnachana nguo za mwanamke aliyefunzwa kujistiri kwa dini yake safi ya kiislamu tangu utotoni na kumuacha utupu.

6.Mwanamke mmoja anashirikiana na wanaume saba kumshambulia na kumdhalilisha mwanamke mwenzake kwa ujira wa pesa tu

7.Mmemaliza kumfanyia ukatili Mwanamke mnamtekeleza maporini mnaondoka na kujiona wajanja... mnajiona mmeyapatia maisha kweli.

8.Nawakumbusha yupo Mungu juu anayeona kila kitu muda wote na sehemu zote. Ipo siku kabla hamjazikwa na kufukiwa na udongo huu mnaotumia kumwaga damu, mtakumbushwa kila tukio moja mlilotenda.

9.Nawaonea huruma ninyi watekaji na wauaji, kwa kuwa najua hamjui watu makatili kama ninyi mwisho wenu unakuwaga vipi.

10.Lakini niwahakikishie akili za upinzani na harakati hazizimwi kwa mtutu wa bunduki na kufuli la Jela tulifikiri mmejifunza kwa Hayati Magufuli

Hamtoweza kuua watu wote,wapo watakaobaki nyuma yetu,wao watatulipia visasi vyetu.hilo mnatakiwa kulielewa siku zote.

Hakunaga Jambo linafanywa na watu zaidi ya wawili likabakia kuwa siri.
Boni yai Twitter
20241023_051623.jpg
 
Boni yai TwitterView attachment 3133118
Hii habari haijanikalia sawa.
. Maadui wa Tanzania yenye amani wako wengi.
 
Ni chama lako, usijitoe akili
Siyo kweli, huyo mama hasemi kweli.

Hapo naona huyo ni msaliti wa mitaa ya kibiti, anajulwa alichoulizwa na alichojibu na onyo alilopewa hajalisema.

Once a system always a system - Zomba.
 
Ni siku ya furaha na huzuni pia

1. Ni siku ya huzuni kwakuwa bado Kombo Mbwana anasota rumande licha ya kutimiza vigezo vyote vya dhamana.. Simulizi yake inajulikana wazi hakuna haja ya kuirudia hapa

2. Ni siku ya huzuni kwakuwa Shadrack kijana aliyechoma picha ya mkuu wa kaya kisha kukamatwa kupandishwa kizombani, kuhukumiwa kifungo na hatimaye kulipiwa faini na Watanganyika wazalendo na kutoka lupango sasa ni saa 48+ zimepita tangu atekwe na wasiojulikana

3. Ni siku ya faraja na furaha kuu kwakuwa katikati ya mtanziko, taharuki, fadhaa na mashaka makuu wakili msomi Mwabukusi kashinda kinyang'anyiro cha kuwa rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (Tanganyika law society) Anastahili pongezi nyingi mno maana haikuwa rahisi kabisa...!

Utekaji bado upo.. Utekaji na watekaji is for real.... Watu bado wanatekwa na kutokomezwa kusikojulikana na wasiojulikana.. Hali ni mbaya kuliko tunavyodhania.

Watakaosalimika ni wachache kati ya wengi ama ni wengi kati ya wachache
Wafaidikaji
Chawa, kunguni na viroboto
Waunga juhudi
'Wenzetu'
Watakaoweza kukaa kimya kabisa
Wa ndio mkuu
Wasiojua kuhoji
Wasioweza kuhoji
Waabudu sanamu
Wasifuni.. nk

Hapo kabla Watanganyika walikuwa wakihoji kimya kimya na wazi wazi kuhusu wanaopotea na huko wanakopotea.. Lakini baada ya simulizi ya Katavi jibu likapatikana

Ogopa sana mateke ya mwisho ya mnyama anayekufa.. Yaogope mno! Maana ni mateke ya kutafuta wa kuondoka naye

Walioko kwenye list ni wengi.. Pengine hata wewe na mimi tumo!
Swali muhimu: Ni nani atasalimika?

View attachment 3060067
Je, kijana huyu amepatikana au bado?
 
Siyo kweli, huyo mama hasemi kweli.

Hapo naona huyo ni msaliti wa mitaa ya kibiti, anajulwa alichoulizwa na alichojibu na onyo alilopewa hajalisema.

Once a system always a system - Zomba.
Doesn’t matter, no justification kwa ushenzi aliofanyiwa, 60 years tangu mtawale, siku ya independent tulikuwa sawa na South Korea na Singapore lakini sasa wenzetu ni first world with GDP per capital better than US, sasa Rwanda ananunua Gold yetu kuliko BOT na Ana refineries kuliko Tanzania, najua huelewi , pumbaf sana CCM
 
Mlaumu aliyeweka misingi yautawala.
 
Back
Top Bottom