Watato wakiniona huwa wanacheka sana na kunizoea hata niwe mkali

Kama kwenye profile ni picha yako sishangai. Lakini kupendwa na watoto ni kipaji. Fungua daycare

Aisee huwa mimi vinaniboaga sana basi tuu,
Unakuta kimekuja na andazi au bagia kinaanza kutaka kukulisha.
Unatamani hata ukaweke Teke moja kakatulie kule tuuu lakini ndiyo kanakazana hako.
 
Mimi nishang'ang'aniwa na mtoto supermarket 'daddy daddy....'

hii mbaya mkuu, kuna bwana mmoja aliwahi ng'ang'aniwa na katoto' baba' 'baba' jamaa akakibeba safiii kumbe baba yake anaona huo mchezo ukijumlisha na akili yake ndogo akakasirika.

Akamtuhumu jamaa kutembea na mke wake na mtoto atakua kaoneshwa na mama kwamba huyu ndo 'baba" sema wazee waliamua kwa busara pale.
 
Huyo jamaa hajiamini aisee..
 
Jua kua wewe ni mtoto mwenzao ila chunga usije kuundiwa zengwe kama la Babu seya hutasamehewa nakuambia
 
Acha mazoea na watoto asee utakuja kuzuliwa jambo kama la babu seya na wanae likakutupa ndani na hutapata msamaha wa mkulu wa kaya.
 
Wasalaam.
Kumekuwa na kawaida sana kwamba watoto wadogo wakiniona wananiangalia sanaaaaa.
Halafu baadae wanaanza kucheka kweli kweli. Hadi wazazi wao wanaanza kushangaa maana huwa hawachekagi hivyo sana. Siku nyingine nimekaa sehemu naingia tu nakuja katoto fulani kakike kamekuja kukaa karibu yangu kananiangalia sana usoni, baadae nikakapa simu yangu kakaanza kucheza Game ya Temple Run. Mama yake akaja pale kuniomba radhi na kuanza kukaraipia kwanini kanaazima simu za watu kasiowajua. Wale majirani zangu wakasema walihisi labda ni katoto kangu hivi. Nilimwambia mama yake mimi sina shida acheze tu, tukakaa nako pale kakacheza mpaka simu ikakata chaji. Kakaanza kunipigisha stori yani tumeongea nako hadi kakalala nikakabeba. Ile naondoka wacha kaanze kunililia ova kananijua yani.

Mara nyingi watoto huwa wanaanzanga kuniongelesha na kunizoea hadi nashangaa sana.
Sasa juzi nidyo nimeishiwa na nguvu, nimekaa kwenye mstari wa hospitali nikaona kajaa fulani kana kama mwaka moja hivi. Yaani kadogo balaa (Andunje) kakamuacha maza wake kakanifuata pale nilipokuwa nimekaa, kakaniangalia kwa muda mrefu kweli halafu baadae kakaanza kucheka kama mtu mzima. Kalicheka hadi kanakaa chini, watu pale hawana mbavu wanaanza kuniangalia mimi hadi nkajistukia yani. Hii sii mara ya kwanza yaani sijui kuna nini kati yangu mimi na hivi vijamaa.

Nikiweka sura ya ukali ili kuvifukuza nidyo kabisaa vinazidi kucheka,
Yaani hata niwe mkali vipi vyenyewe hivyo mwilini. Mara kinivute sharubu, mara kinivue miwani.
Hiki kiko na andazi lake kinataka kunilisha na mimi yaani vurugu ova vinanijua atiii.
Yaani sijuia vinaniona mimi nimekaa kama likatuni fulani.
angalia yasije yakakukuta ya Babu seya na kocha
 
strategy ya kuwakamata single mothers wa JF.
 
Chunga sana hiyo hali Mkuu siyo ya kuendekeza sana

Afadhali kidogo kama ni Mwalimu wa chekechea lakini vinginevyo wajabambikwa janga ujute
 
Kuna watu tupo hivyo afadhal nipata mwenzangu nilikua nawaza cpati picha saa mi hata kitoto kikiwa kinalia wameshindwa kukinyamazisha mi nkikibeba kinakaa kimya gaflaa full kunitumbulia macho na kukiacha baada ya hapo ni mbinde cjui tatzo ni nn mweeee
Msafi wa moyo au una babyface...
 
Back
Top Bottom