Watato wakiniona huwa wanacheka sana na kunizoea hata niwe mkali

Watato wakiniona huwa wanacheka sana na kunizoea hata niwe mkali

Hahaha,
Juzi nimekaa kanisani kwenye Ibada ya Christmas.
Watu wako kimya kuna katoto pembeni kakaniropokea "Heee mama huyu mbaba ni mweusi huyoo halafu ana mindevu"
Watu wakageuka na kuangalia nikabaki nachekaaa.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wasalaam.
Kumekuwa na kawaida sana kwamba watoto wadogo wakiniona wananiangalia sanaaaaa.
Halafu baadae wanaanza kucheka kweli kweli. Hadi wazazi wao wanaanza kushangaa maana huwa hawachekagi hivyo sana. Siku nyingine nimekaa sehemu naingia tu nakuja katoto fulani kakike kamekuja kukaa karibu yangu kananiangalia sana usoni, baadae nikakapa simu yangu kakaanza kucheza Game ya Temple Run. Mama yake akaja pale kuniomba radhi na kuanza kukaraipia kwanini kanaazima simu za watu kasiowajua. Wale majirani zangu wakasema walihisi labda ni katoto kangu hivi. Nilimwambia mama yake mimi sina shida acheze tu, tukakaa nako pale kakacheza mpaka simu ikakata chaji. Kakaanza kunipigisha stori yani tumeongea nako hadi kakalala nikakabeba. Ile naondoka wacha kaanze kunililia ova kananijua yani.

Mara nyingi watoto huwa wanaanzanga kuniongelesha na kunizoea hadi nashangaa sana.
Sasa juzi nidyo nimeishiwa na nguvu, nimekaa kwenye mstari wa hospitali nikaona kajaa fulani kana kama mwaka moja hivi. Yaani kadogo balaa (Andunje) kakamuacha maza wake kakanifuata pale nilipokuwa nimekaa, kakaniangalia kwa muda mrefu kweli halafu baadae kakaanza kucheka kama mtu mzima. Kalicheka hadi kanakaa chini, watu pale hawana mbavu wanaanza kuniangalia mimi hadi nkajistukia yani. Hii sii mara ya kwanza yaani sijui kuna nini kati yangu mimi na hivi vijamaa.

Nikiweka sura ya ukali ili kuvifukuza nidyo kabisaa vinazidi kucheka,
Yaani hata niwe mkali vipi vyenyewe hivyo mwilini. Mara kinivute sharubu, mara kinivue miwani.
Hiki kiko na andazi lake kinataka kunilisha na mimi yaani vurugu ova vinanijua atiii.
Yaani sijuia vinaniona mimi nimekaa kama likatuni fulani.
Mungu awalinde malaika wetu....wabakaji wa watoto ni wengi siku hizi[emoji22]
 
Jua kua wewe ni mtoto mwenzao ila chunga usije kuundiwa zengwe kama la Babu seya hutasamehewa nakuambia

Hahaha,
Mkuu zaidi ya watoto wa nyumbani kwangu hapa mimi sina hulka ya kucheza cheza na vitoto kabisa.
Wala sipendi hata kukaa navyo karibu lakini vikiniona vinahisi mimi katuni sijui mara vinivute ndevuu na kutaka miwani.
Uzuri mara nyingi huwa vinakuwa na wazazi wao aiseee....
 
Chunga sana hiyo hali Mkuu siyo ya kuendekeza sana

Afadhali kidogo kama ni Mwalimu wa chekechea lakini vinginevyo wajabambikwa janga ujute

Watoto wako na wazazi wao hapo kuna uhatari gani ??
Unakuta kitoto kipo na maza wake na dingi yake kinaanza kunililia nikibebe tu.
Mara kinaanza maswali, kinanichekea tu hadi wazazi wake wanashangaa.
 
Aisee huwa mimi vinaniboaga sana basi tuu,
Unakuta kimekuja na andazi au bagia kinaanza kutaka kukulisha.
Unatamani hata ukaweke Teke moja kakatulie kule tuuu lakini ndiyo kanakazana hako.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]teke tena mkuu[emoji23]uckacrike vinakuja na neema hivyo
 
Watoto wako na wazazi wao hapo kuna uhatari gani ??
Unakuta kitoto kipo na maza wake na dingi yake kinaanza kunililia nikibebe tu.
Mara kinaanza maswali, kinanichekea tu hadi wazazi wake wanashangaa.
hongera kwa kupendwa na watoto ila kuwa makini maana ipo siku kitoto kitakuita baba baba... halaf awe na wazazi wake wote hapo ndo utajua kama kuna hatari au lah!
 
hongera kwa kupendwa na watoto ila kuwa makini maana ipo siku kitoto kitakuita baba baba... halaf awe na wazazi wake wote hapo ndo utajua kama kuna hatari au lah!

Hahahaha,
Mkuu sasa hadi vitoto vya kizungu navyo ntakuwa baba yao ???
 
Raha sana kupendwa na watoto
Ila vinauzi sanaa,
Yaani mara kipo kichwani, mara hiki kinataka kiatu.
Wewe umechelewa kurudi usiku, saa kumi na mbili asubuhu kipo mlangoni "Baba nifungulie mlango" au "Baba naumwa tumbo" . Unakuta hata hakaumwi basi unajua tu kanataka kuja tu. Hicho kinazama kitandani kinaanza kuuliza maswali maswali wakati mimi nimekesha usiku.
Utoto bwanaaa....
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]teke tena mkuu[emoji23]uckacrike vinakuja na neema hivyo

Sasa mkuu saa kumi na mbili asubuhi,
Kanagonga mlango kanadanganya kanaumwa tumbo.
Ukikafungulia mlango hako kanazama kitandani kanaanza vimaswali- vimaswali tu...
Nina kazi mimi wewe.....
 
Hahaha,
Juzi nimekaa kanisani kwenye Ibada ya Christmas.
Watu wako kimya kuna katoto pembeni kakaniropokea "Heee mama huyu mbaba ni mweusi huyoo halafu ana mindevu"
Watu wakageuka na kuangalia nikabaki nachekaaa.
Cheusi mangala[emoji85] [emoji85] [emoji85]
 
Mimi nasumbuliwa na vitoto vya majirani zangu hapa,yaani sijui hata vinanipendea nini maana vikiniona tu vinaniganda mpaka naenda navyo kwangu,sometime vinaanza kulialia viletwe kwangu na mimi muda huo nataka kupumzika basi tabu tu! Na vikija kwangu wala havitulii utavisikia tu jirani leo mi nalala hukuhuku kwako!
 
kuvifukuza unashindwa ???
 
Back
Top Bottom