Nikiwa sijawa mtu wa maovu maovu watoto tulikuwa marafiki sana, nakumbuka mtaani kuna watoto watatu walipewa majina sawa na mimi.
Nilikuwa na macho makubwa kwa hiyo akizaliwa mtoto ana macho makubwa anapewa jina langu.
Sasa nikawa kila sikukuu nanunua pipi, biscuits, jojo na vitu vingine vya watoto wanakuja home, wakimkuta mama mimi sipo wanalia kweli, ikawa kama deni sasa, kila weekend lazima waje.
Siku moja kuna mtoto aliharisha na kutapika baada ya kula biscuits, mama yake akaja nyumbani anaongea mwanae kalishwa sumu, akifa tujiandae kuozea jela, tena akasema alishashtukia kwamba eti nafanya vile ili niwatoe sadaka wale watoto nitajirike, nilikuwa ni ule mwaka wa kusubiri kujoin chuo baada ya kumaliza form 6, nilimchukua yule mtoto mpaka hospital, tumefika tu akawa hata hatapiki tena, akapona tu mwenyewe.
Basi tukarudi. Sasa nikaachana na wale watoto, wanakuja kulia nyumbani mimi hata sina muda, mpaka wazazi wanakuja kuniomba msamaha eti watoto wanalia. Ile shida ilinifundisha kutodili na mtoto wa mtu, tena usimpe chakula chochote.