Watawala wa kike katika nchi za Kiislamu

Watawala wa kike katika nchi za Kiislamu

Write your reply...
NINASUBIRI JIBU LA juu ya swali je uislamu unasemaje kuhusu kutawaliwa na mwanamke? T
Ha haaa
Unakazia hoja mjumbe wa kamati ya roho mbaya ...😂
Mimi mkristo though..
 
Wayahudi si waarabu. Acha kupotosha watu. Kuwepo Wapalestina si kuwafanya Waisrael kuwa Waarabu. Nimeona nikuweke sawa sawa katika hili. Tafuta nchi ya Kiarabu ambayo ilitawaliwa na Mwanamke Achana Nigeria isnt an Islamic State/Country.
Msaada tutani:
Wayahudi ni watu gani?!

Uyahudi NI nini?
Ni Imani ya kidini au RACE/rangi ya mtu..!?

Msaada tafadhali!
 
Hata kule Bangladesh kulikuwa na mtawala wa kike nadhani aliitwa sheihk Asina kama sikosei wajuvi mtanisahihisha.
 
Unamaanisha nini unaposema Afrika haikuwepo?
Neno Africa lilikuja baadae kabisa karne ya 16tu, na ilitokana na neno la Kigiriki A'phrike maana yake sehemu isiyo na baridi (yaani kama ilivyo sehemu kubwa ya ulaya)

Mwasisi wa neno hilo aliitwa Africanus
 
Neno Africa lilikuja baadae kabisa karne ya 16tu, na ilitokana na neno la Kigiriki A'phrike maana yake sehemu isiyo na baridi (yaani kama ilivyo sehemu kubwa ya ulaya)

Mwasisi wa neno hilo aliitwa Africanus
Kwa maana hiyo ni sawa. I thought unamaanisha Afrika kwa maana ya eneo la kijiografia halikuwepo!
 
Watu wengi huamaini kuwa nchi za kiislamu huwa haziwaheshimu wanawake na haziwezi kutawaliwa na wanawake. Hata hivyo miaka ya hivi karibuni imeonakana kuwa hilo siyo kweli kwani kule Pakistani walitawaliwa na mwanamke Benazir Bhutto kwa muda mrefu kabla hawajamuua.

Ninataka kuchokonoa historia ya mtawala mmoja wa kike kule Nigeria ya kaskazini kwenye jamii ya wahausa ambayo ni ya kiislamu kwa muda mrefu sana aliyekuwa akiitwa malkia Amina. Mama huyu alitawala takriban miaka 200 kabla ya ujio wa Usman dan Fodio ambaye ndiye anyejulikana sana eno hilo kihistoria. Amina alikuwa ni mtoto kwanza wa mfalme Nikatau aliyekuwa anatawala kule kaskazini mwa Nigeria. Alikuwa na wadogo zake watatu; mdogo wake wa kiume alikuwa mtoto wa pili wa mfalme Nikatau alikuwa akiitwa Karama, halafu mdogo wake wa kike alikuwa akiitwa Zaria; leo hii kuna mji kule kaskazini mwa Nigeria unaitwa Zaria kwa sababu ya huyu mdogo wake wa kike.

Amina alijifunza kupigana vita angali kigoli wakati akiwa anaishi na babu yake; baada ya baba yake kufa, mdogo wake wa kiume ndiye aliyerithi ufalme wakati Amina akiwa anendelea na maisha ya kijeshi ya kupigana vita aliyokuwa amejifunza kutoka kwa babu yake; alikuwa msichana mrembo sana ambaye pamoja na ushujaaa wake wa kijeshi wanaume wengi walitaka kumwoa lakini hakuna aliyefanikiwa. Baada ya kukaa madarakani kwa miaka kumi, kaka yake, yaani mfalme Karama, naye alifariki, na hivyo Amina kuchukua mamlaka ya kuwa mtawala wa eneo hilo akijulikana kama malkia Aminatu.


Malkia Aminatu anakumbukuwa sana kwa kuliendeleza eneo la Zaria hadi kuwa kitovu kikubwa cha biashara kaskazini mwa Nigeria kama ilivyo leo.
Huyo mwanamke alitawalaje miaka 200?,kwa hiyo aliishi miaka mingapi?,huu si uongo mwingine kweli?
 
Huyo mwanamke alitawalaje miaka 200?,kwa hiyo aliishi miaka mingapi?,huu si uongo mwingine kweli?
Pumba tupu wewe hujui kusoma; post hiyo haikusema alitawala kwa miaka 200 bali imesema alitawala miaka 200 kabla ya ujio wa Osman Dan Fodio. Unatakaiwa ujue Usman dan Fodio alitawala lini halafu uondoe miaka 200 kujua Malkia Amina alitawala lini. Wewe ulisomea shule gani ili nikaongee na mwalimu mkuu akunyang'anye cheti ??
 
ukisoma vyema mzee utajua yakuwa uslamu umepandikizwa tuu baadaye sana wala hiyo nchi huwezi sema nchi ya kiislamu
napenda tukiongelea africa tungelee zaidi kulingana na uhalisia wa asili zetu,
nivyema kutumia marejeo ya bwafrica wenzetu kuliko hao wakoloni koloni tu
 
Back
Top Bottom