Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Ili kujenga jamii iliyobora mawasiliano katika kutatua changamoto za jamii ni muhimu sana. Lakini katika hili ofisi na taasisi za Serikali zimekuwa na changamoto katika kutoa mawasiliano kwa Umma na taarifa muhimu zinazowafaa wananchi.
Ukianza kutafuta taarifa za jambo fulani katika Serikali na Taasisi zake utatumia nguvu kubwa na muda mrefu bila sababu za msingi na wakati mwingine kukutana na majibu yasiyo ridhisha.
Serikali imekuwa ikitoa kwa njia mbalimbali japo njia zote zinakuwa na changamoto nyingi sana nazo ni:-
Mawasiliano ya simu
Serikali na Taasisis zake hutoa au kuweka njia za mawasiliano kama simu barua pepe nk, lakini cha ajabu unaweza kupiga simu bila mafanikio, utapiga simu inaita tu bila kupokelewa japo ni saa za kazi na wakati mwingine unaambiwa namba ya simu uliyopiga haipo.
Pia inaweza kupokelewa na ukajibiwa anayetakiwa kujibu hili hayupo, na kabla hujauliza swali lingine simu inakatwa na ukipiga haipokelewi tena, au utajibiwa suala lako tumelipokea na linashughulikiwa, limefikishwa sehemu au kwa muhusika na hupewi jibu la lini litashughulikiwa na kila ukiuliza jibu ni lilelile kuwa linashughulikiwa. Itapita muda unakuwa mwendelezo wa jibu hilo kila mara.
Tovuti
Kwenye Tovuti za Serikali kuna changamoto ya kutokusasisha taarifa mpya ambazo zinaendana na wakati uliopo, taarifa nyingi zinakuwa zimepitwa na wakati. Pia unaweza kukutana na taarifa ambazo hazikizi mahitaji yaani hazijisholezi.
Nini kifanyike
Watu wanaohusika na mawasiliano ('simu, tovuti nk) wajue wajibu wao. Watambue kuwa watu wanategemea ushirikiano wao hivyo waache kuona kama namba za simu zipo kama mapambo. Zitumike ili kufanya lengo kussudiwa kufikiwa.
Tambueni kuwa watu wengi huishi mbali na ofisi zenu au makao yenu makuu, hivyo msipotoa ushirikiano wa kupokea simu, au kutoa taarifa kwa wakati inawagharimu watu kusafiri umbali mrefu kuja ofisini kwenu ili kuja kupata huduma amabzo wangeweza kuzipata kwa majibu ya simu tu na wakaokoa muda, na gharama
Pia wakaondokana na usumbufu ambao si wa lazima lakini pia muda huo wakautumia katika kuzalisha na kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.
Zingatieni kuwa taarifa ni rasilimali muhimu katika kufanya mambo yote, hivyo zikiwepo kwa wakati na mkatoa ushirikiano bila shida mtasaidia kuokoa fedha, muda na kuchangia maendeleo kwa jamii nzima.