Watawala wetu tuliowachagua kupitia sanduku la kura, mbona hawatujali wananchi wao tunaoteseka, kutokana na kupanda bei ya mafuta Duniani?

Watawala wetu tuliowachagua kupitia sanduku la kura, mbona hawatujali wananchi wao tunaoteseka, kutokana na kupanda bei ya mafuta Duniani?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Nimekuwa nikijiuliza Katika mazingira ya nchi yetu, iliyobarikiwa na Mungu, rasilimali za kila aina, kama vile, gesi, madini ya kila aina, ardhi yenye rutuba, inayoweza kustawisha mazao ya biashara na chakula kwa kipindi chote cha mwaka.

Hivi Katika mazingira hayo, ndiyo watawala wetu wameona njia moja pekee, ya kutukamua kwa tozo za Kila aina wananchi wake, hadi tuna-suffocate??

Kwa kufafanua zaidi mada yangu ni kuwa bei za mafuta ya Petroli, hapa nchini, haishikiki na imeleta taharuki kubwa Sana Katika nyanja mbalimbali za usafiri za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, Hadi kutokelezea kupanda kwa bidhaa Karibu zote.

Japo tunafahamu kuwa kupanda huko kwa bei ni kwa Dunia nzima, hata hivyo mataifa mbalimbali yamechukua hatua za dharura za kuondoa tozo kwenye mafuta hayo na Serikali yenyewe kuchukua hatua za ziada kwa ku-subsidize, Ili bei hizo zisiweze kuwaumiza wananchi wao masikini.

Hebu tuchukulie mfano wa nchi jirani za Zanzibar na Kenya, ambazo aidha zimefuta tozo mbalimbali za kwenye mafuta au zime-subsidize bei ya watumiaji wa mafuta hayo.

Mfano ni nchi "jirani" yetu ya Zanzibar, ambayo wananchi wake wameendelea kununua mafuta kwa shilingi 2,600 wakati sisi watanganyika tukikwamuliwa kwa zaidi ya shilingi 3,100!

Nakuwa nikijiuliza, hivi inakuwaje kwa baadhi ya viongozi wetu, wakitamba kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa nchi yetu ni tajiri Sana, Hadi tunaweza kuwa "donor county"Hadi kwenye hizo nchi za magharibi, zinazotamba kuwa ni matajiri wa Dunia??

Ni hayo tu maoni yangu machache kwa watawala wetu.
 
Lakini huyu mtawala tuliyenaye sasa amewekwa na Katiba mbovu tuliyonayo.
 
Lakini huyu mtawala tuliyenaye sasa amewekwa na Katiba mbovu tuliyonayo.
Pamoja na wizi mkubwa wa kura walioufanya, lakini ni vyema wakawajali angalau kidogo wananchi wao, lakini siyo kwa Hawa watawala tulionao, ambao wao mawazo yao ni maslahi yao binafsi pekee!

Rejea yule mama, the former first lady, ambaye licha ya yeye "kupendelewa" kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge na mwanaye naye "kupewa" ubunge na pia Waziri mdogo na mumewe anapata mafao ya 80% ya mshahara aliokuwa anaupata wakati akiwa Rais, bado na yeye ameomba afikiriwe kwa mafao ya "the former first lady"

Haya maajabu utayaona kwenye nchi yetu pekee Katika Dunia hii!
 
Back
Top Bottom