Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tulishuhudia Mara kwa Mara, huko siku za nyuma, watawala wetu wakitupa updates, tena wakati mwingine hata wakitupa taarifa nyingine za ziada kama vile wametuma wanasheria wetu mahiri kwenda igomboa ndege yetu iliyokamatwa huko Afrika Kusini kutokana na deni tunalodaiwa na mkulima wa huko, Hermanus Steyn
Hatimaye tukaona ndege yetu ikiachiwa na serikali ya Afrika Kusini na watawala wetu hao, wakatoa kebehi nyingi sana kwa wale waliowaita kuwa walifurahia kukamatwa kwa ndege yetu hiyo, hadi kufikia hatua ya kuwakebehi watu hao kuwa ni wasaliti na wanatumika na mabeberu
Hata hivyo sidhani kama kuna mtu aliyefurahi kukamatwa kwa ndege yetu hiyo na badala yake niliona watanzania wengi wakisisitiza kuwa "dawa ya deni ni kulipa"
Lakini hali imekuwa tofauti sana baada ya ndege yetu nyingine kukamatwa huko Canada, ikiwa inajitayarisha kuja nchini kwetu
Zile mbwembwe na vijembe walivyokuwa wakivitoa watawala wetu kwa hao waliowabatiza majina kuwa ni wasaliti na wanatumika na mabeberu, nimeshangaa sana kuona safari hii wamekuwa kimya sana, utadhani wamepigwa ganzi!
Ndipo hapo ninapojiuliza kulikoni??
Hiyo ni ndege yetu sote watanzania na imenunuliwa kwa pesa ya kodi zetu, kwa hiyo tunapaswa kupewa "updates" ya kila kinachoendelea kuhusu ndege yetu, kwa kuwa ndege hiyo siyo Mali binafsi ya Rais Magufuli pamoja na wapambe wake, kwa hiyo tunapaswa kupata habari kamili ya nini kinachoendelea kuhusiana na ndege yetu hiyo