Watawala wetu, tupeni "updates" ya ndege yetu iliyokamatwa huko Canada

Watawala wetu, tupeni "updates" ya ndege yetu iliyokamatwa huko Canada

Wako bize na CHADEMA kwanza
Hawawezi leta update wakati wanajua chadema uchaguzi haujaenda vizuri wanasubiri huo mjadala upoe ndipo wataleta yao, na wanajua mjadala wa ndege utaifunika chadema na itakuwa ni hasara kwao.
 
Tunataka tuone ile jeuri ya Waziri wetu wa Katiba, Profesa Kabidi, ya kudai kuwa amemuita Balozi wao na kumkemea vikali, angeendelea kutupa "updates" baada ya kumkemea Balozi wao, nini kimetokea, je ndege yetu tumeigomboa??
Maneno na sheria ni vitu viwili tofauti
 
Wawatume wasiojulikana kwenda kumpiga risasi 40 hadharani huyo mkulima
Halafu waseme kuwa kajishabulia mwenyewe.
 
Ukiona kimya ujue mfupa wa samaki umewakwama walioula, wangemeza ndo wangekuwa wakwanza kusema, serikari inataratibu zake za kusema. Just wait a_ moment at very soon mtapata habari njema
 
Mkulima kaigeuza fremu
Anauzia mananasi Canada.
kwa kweli hatuwezi kukubali nchi yetu inahujumiwa.
Huyu Jiwe kazi yake ni "kujimwambafai"

Sasa tuone huko kwa mabeberu kama kujimwambafai kwake kutafua dafu!

Miaka ya 78 nikiwa mitaa ya Mansfield karibu na Catholic bookshop walitokea majambazi wakiwa na silaha wakiwa wanafukuzwa na wanainchi, sikuamini macho yangu na sikuelewa inakuwaje jambazi ana silaha na bado watu wanaendelea kuwafukuza?...science hiyo mpaka leo sijaelewa.
 
Tulishuhudia Mara kwa Mara, huko siku za nyuma, watawala wetu wakitupa updates, tena wakati mwingine hata wakitupa taarifa nyingine za ziada kama vile wametuma wanasheria wetu mahiri kwenda igomboa ndege yetu iliyokamatwa huko Afrika Kusini kutokana na deni tunalodaiwa na mkulima wa huko

Hatimaye tukaona ndege yetu ikiachiwa na serikali ya Afrika Kusini na watawala wetu hao, wakatoa kebehi nyingi sana kwa wale waliowaita kuwa walifurahia kukamatwa kwa ndege yetu hiyo, hadi kufikia hatua ya kuwakebehi watu hao kuwa ni wasaliti na wanatumika na mabeberu

Hata hivyo sidhani kama kuna mtu aliyefurahi kukamatwa kwa ndege yetu hiyo na badala yake niliona watanzania wengi wakisisitiza kuwa "dawa ya deni ni kulipa"

Lakini hali imekuwa tofauti sana baada ya ndege yetu nyingine kukamatwa huko Canada, ikiwa inajitayarisha kuja nchini kwetu

Zile mbwembwe na vijembe walivyokuwa wakivitoa watawala wetu kwa hao waliowabatiza majina kuwa ni wasaliti na wanatumika na mabeberu, nimeshangaa sana kuona safari hii wamekuwa kimya sana, utadhani wamepigwa ganzi!

Ndipo hapo ninapojiuliza kulikoni??

Hiyo ni ndege yetu sote watanzania na imenunuliwa kwa pesa ya kodi zetu, kwa hiyo tunapaswa kupewa "updates" ya kila kinachoendelea kuhusu ndege yetu, kwa kuwa ndege hiyo siyo Mali binafsi ya Rais Magufuli pamoja na wapambe wake, kwa hiyo tunapaswa kupata habari kamili ya nini kinachoendelea kuhusiana na ndege yetu hiyo

Siyo lazima mujuwe kila kitu, fanzeni yanayowahusu tu,mengine yaacheni yalivyo....full stop
 
Ndiyo hivyo, mkulima atalipwa kimya kimya kama walivyofanya ile ya kwanza iliyokamatwa huko huko Canada.
Unaelekea kukosa uzalendo kama Mwakinyo na Matumla...
Hupaswi kusema chochote kinachofanana na ukweli kwanini hamsikii lakini?
 
Ndege ikiachiliwa na kutua bongo mtahamisha magoli na kuja na hoja nyingine.

Ushirikina ni tabia na siku zote mtu huzeeka na tabia zake.
 
Back
Top Bottom