Watawala wetu, tupeni "updates" ya ndege yetu iliyokamatwa huko Canada

Watawala wetu, tupeni "updates" ya ndege yetu iliyokamatwa huko Canada

Lipeni deni tu yote yataisha. Pesa inayotumika kusafirisha makundi ya wanasheria ingetumika kupunguza kidogo kidogo ingesaidia kuliko ngonjera zenu za kitoto. Hakuna ushirikina hapa.
Wanaosafirisha wanasheria wanao ufahamu mkubwa wa hili suala kuliko wewe na mimi.
 
ikiachiliwa? bado inashikiliwa? acha utani. jopo la phd kibao limekwama wapi? walisahau kusema kuwa hii ndege haswa ingetumiwa na rais. kuna special gadgets kumsaidia rais kudukua kila atakalo. ikiendelea kukaa huko mabeberu wanaweza kuweka vifaa vyao kumdukua rais wetu!
Akili za usaliti katika ubora wake.
 
Tunataka tuone ile jeuri ya Waziri wetu wa Katiba, Profesa Kabidi, ya kudai kuwa amemuita Balozi wao na kumkemea vikali, angeendelea kutupa "updates" baada ya kumkemea Balozi wao, nini kimetokea, je ndege yetu tumeigomboa??
Au angalau atuambia nini yalikuwa majibu ya balazi baada ya kumgombeza na kumkemea vikali
 
Tunataka tuone ile jeuri ya Waziri wetu wa Katiba, Profesa Kabidi, ya kudai kuwa amemuita Balozi wao na kumkemea vikali, angeendelea kutupa "updates" baada ya kumkemea Balozi wao, nini kimetokea, je ndege yetu tumeigomboa??

Point of Correction:

Palamaganga Kabudi sio Waziri wa Sheria na Katiba (Waziri husika ni Balozi Mahiga)

Palamaganda Kabudi ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Africa Mashariki.
 
Subiri tumtume jafo akamseme mkulima wa kizungu, tutapata tu majibu..
 
Umeshawaita ni watawala kwa hiyo hawawezi kukupa update yeyote! Tanzania tunachagua kutawaliwa na watawala badala ya viongozi halafu unauliza wakupe updates?!
 
Point of Correction:

Palamaganga Kabudi sio Waziri wa Sheria na Katiba (Waziri husika ni Balozi Mahiga)

Palamaganda Kabudi ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Africa Mashariki.
Noted
 
Anaweza kuamuru wanachama wote SADC kufunga ofisi zao za ubalozi na Canada kwa kuleta ubeberu wao! Chezea ngosha!
Kwa hapa TZ yeye ndiyo kila kitu

Anatamani awe IGP..........

Anatamani pia awe CJ............

Pia anautamani U-Spika wa Bunge.......

Anachoshangaa huko kwa wenzetu, kila mhimili unafanya shughuli zake ukiwa huru kabisa, bila kuingiliwa na mtu yeyote yule, kiasi ambacho anapandwa na hasira , hadi kukaribia kupasuka
 
blah blah so....
unahisi kisha unaamini unachohisi
Habari ndio hiyo, kule viongozi wao wanatii sheria, wana utu na hawana ulevi wa madaraka, sio huku kiongozi anaipangia mahakama ikomoe wasiomsujudia na mahakama inatii!
 
Au yawezekana ‘mkulima’ keshamilikishwa ndege yetu.
Huo ungekuwa uamuzi wa busara kufuta deni na mkulima angeanzisha kampuni take usafiri wa anga badala ya SAA ya serkali ambayo iko ICU karibu ife kama ATCL. Siyo kama wateuliwa wetu hapa, mkulima anauzoefu mkubwa na ndege maana alikuwanazo nyingi tu kwenye mashamba yake. Chapa ng'ombe wangebaki na kitoeo tu.
 
Kwani yule naibu waziri anayeongozwa na jamaa wa majalalani amesemaje? Maana yeye ni mwanasheria msomi kabisa.
 
Back
Top Bottom