Eli Cohen
JF-Expert Member
- Jun 19, 2023
- 4,460
- 13,715
Paul Getty, huyu ndio mmoja ya wawekezaji wa kwanza kuvuta mafuta Saudi Arabia miaka hio bado ni nchi isio na maendeleo makubwa.
Mwanzoni Waandishi walivyomuuliza kwa nini hataki kutoa ransom alijibu hivi
"Nina wajukuu kumi nne. Kama nikitoa pesa ya huyu mmoja basi 14 wengine watatekwa"
Watekaji walihitaji $17milion, akagoma, then wakakata sikio la mjukuu wake wakamtumia, alivyoona hivyo ndio akasema wapunguze pesa maana tayari wameshamzuru mjukuu wake, wakahangaishana sana hadi $3million ila mwamba alishuka nao hadi $2million ndio wakamwachia dogo.
Ingawa pesa hio alitaka mjukuu wake akisharudi ailipe kwa riba ya asilimia 4 🤣🤣🤣
Mjukuu wake baadae kutokana na msongo wa mawazo kwa aliyoyapitia aliingia katika ulevi mzito kupelekea kupata stroke.