Dr Samia Suluhu Hassan tokea alipoapishwa kuwa Rais baada ya kifo cha Hayati Dr John Joseph Pombe Magufuli amekuwa akifanya kazi kubwa sana katika kuijenga Tanzania mpya huku akionyesha uwezo na ujasiri mkubwa katika kulinda maslahi ya taifa.
Rais anaijenga Tanzania mpya ya watu wanaopendana,wachapa kazi,wazalendo,wacha Mungu na ambao wako tayari kusaidiana na kuinuana katika nyanja mbalimbali za maisha na hili linajidhihirisha wazi katika mabadiliko mbalimbali na maamuzi yenye tija kwa taifa
Pamoja na kazi hizo nzuri tumeanza kushuhudia matukio ya hovyo ambayo hayashabiiani na tabia,mwenendo na maono ya Rais Samia Suluhu ikiwemo utekaji na mauaji ya watu wasio na hatia.
Ikumbukwe kuwa Rais Samia anakiongoza Chama Cha Mapinduzi,Chama ambacho kina historia na heshima Afrika na Dunia.
CCM ni chama cha ukombozi wa Africa.
Hiki ni Chama ambacho kina historia ya kuwafunda wapigania Uhuru wa Afrika.
CCM ni chama ambacho mwasisi wake Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa miongoni mwa wanafalsafa mahiri wa Karne ya ishirini.
Kwa historia hii ya CCM ni ukweli usiopingika kuwa Chadema na vyama vya upinzani hapa Tanzania siyo level ya CCM hivyo siyo kosa nikisema kuwa hawa watekaji siyo wana CCM na kama wanatumwa na mtu au watu wanaotokana na CCM basi CCM itakuwa imevamiwa.
Kwa historia hii iliyotukuka naomba nisisitize kuwa CCM haina haja ya kuwaogopa wapinzani isipokuwa kina haja tu ya kurekebisha baadhi ya mambo ili kiendelee kushika Dola.
CCM haina haja ya kuwaogopa watu wenye fikra mbadala.
CCM ninayoifahamu haiwezi kumteka Soka na wenzake,vijana wadogo ambao hawajakomaa, tiktok generation.
Tundu Antipas Lissu ambaye pengine ndiye msomi hodari wa upinzani ila bado bwana mdogo Kwa CCM.
Mzee aliyestaafu Ally Mohamed kibao hakuwa na fikra wala ujuzi wala mikakati inayoweza kuinyima usingizi CCM mpaka iamue kuwa anastahili kutekwa kwenye basi na task force maalumu kwa kutumia silaha za vita kama SMG na na kumuua kikatili.Hapana.
CCM imekuwa na historia ya kutumia fikra na ushawishi katika kuongoza nchi na bado sera na falsafa zake zina appeal kwa kizazi cha sasa na Jumuiya ya kimataifa.
CCM ni level moja na Community Party of China (CCP),na ni zaidi ya ANC cha Afrika kusini,SWAPO, ZANU PF,FRELIMO nk.
CCM ni mwasisi na ni think tank kwa jumuiya za kimataifa na ni Baba wa kidemokrasia Afrika na Dunia
Hivyo kupitia andiko hili nasisitiza umuhimu wa kumuacha Dr Samia Suluhu Hassan asimame Kwa miguu yake katika kiongoza nchi na hapaswi kuwa na hofu kwani CCM ina hazina kubwa ya wazee wastaafu wenye hekima pengine kuliko chama chochote katika ulimwengu unaoendelea.
Hawa wahuni wanaoteka watu na kuwaua.
Hawa wahuni wanaowateka mpaka vijana wadogo sampuli ya akina Soka wasiojua wanachokifanya wabainiwe na washughulikiwe ipasavyo kwani wanavunja miiko ya CCM na serikali yake na taifa kwa ujumla..
Kama mwana CCM natamka wazi kuwa hatuwahitaji wahuni hao.
Kwa kazi kubwa iliyotukuka inayofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dr Samia Suluhu Hassan itakapofika wakati wa uchaguzi tutapata muda mzuri wa kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 na hakika Watanzania watatupa tena ridhaa ya kuongoza nchi.
Watanzania wanatambua kuwa CCM haina mbadala hapa Tanzania
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania