Watekaji wanamharibia Rais Samia pamoja na kazi hizo nzuri anazozifanya

Yeye ndiye anayejiharibia kwa kutowachukulia hatua japo hata kuwasimamisha kazi wakuu wa idara husika! Mfano mara moja angemsimamisha kazi Waziri wa Mambo ya ndani,IGP,RPC angekuwa amejijengea heshima!
Watu wangeendelea kukivumilia Chama,Chama kilichochokwa na wananchi kuliko vyama vingine vya Afrika!
Chama kinachoingia madakani kwa nguvu za kijeshi.
Akifanya hili Chama kinaweza kuendelea kupumua!
Kwa hiyo tusisingizie Watekaji na Wauaji.
 
Hiyo mentality ya kihistoria kuwa CCM sijui chama cha ukombozi imepitwa na wakati.Hata hiyo ANC imeshindwa vibaya...mnakalia mambo ya kizee.Generation inayokuja sasa hivi hayo mambo ya kusema sijui kilitukomboa toka ukoloni ni hoja mfu.
CCM mlibadirishana na mkoloni kututawala tu, wale walikua wazungu nyinyi waafrika weusi wenzetu mnafanya ujinga huohuo.
Watu wanataka maendeleo, amani, maisha bora, ajira na demokrasia - uhuru wao kinyume chake pamekuwa na state dictatorship, wizi wa mali za uma mkianza na nyinyi CCM mliochukua mali za serikali na kujimilikisha, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, maendeleo mwendo wa kobe, ajira ndo bomu la taifa kadiri miaka inavyoenda.
Chama chenu kimekua cha Matajiri, Wafanya biashara, wazalendo wachache pale, wengi sasa mpo kwa ajili ya matumbo yenu. Baba wa Taifa angekuwa na tamaa walizonazo baadhi ya wanaCCM kwa sasa hii nchi angejiuzia yote. Pia usijilinganishe na chama cha kikomunisti cha China - CCP..tumeona walichokifanya economically hata kama kisiasa sio sana - walichagua upande mmoja wame-excell - Nyie kwa nini hamkujifunza kwa CCP...nyie mnajifunza ANC matokeo yake nao wamefail vibaya.
CCM ina hazina ya watu na viongozi lkn mfumo tayari uko corrupt.
I WISH mamlaka za Usalama zifanye mission ,ziigawe CCM mbili watu wengine huku , wengine kule...tuvunje bureaucracy tupate vyama viwili vyenye mizizi vyote, vyenye watu then wagombanie uongozi, then wengine waende CHADEMA, ACT..
Kwa kinachoendelea sasa CCM hamna jipya mtakalo waambia watu- mpumzike kwanza..nyie ndo chanzo cha chokochoko zote hizi..mnaboa CCM.
 
Rais na chama chake ni hovyo
 
Kweli, yapo mazuri Mheshimiwa
ameyafanya, hata mengine nimeyaona kwa macho yangu.

Haya mauaji na utekaji kweli unaliletea taifa hofu.

Hao wanaojiita wana harakati, hawana serikali, hawana hata uchumi mkubwa, more times ni vijana wa mitandaoni.

Pia ukosefu wa ajira au mitaji unachangia vijana kuwa wapo tu vijiweni.

Hebu waapuuzeni, they don't have government.
 
Watanzania wanafiki sana, kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa yanayoendelea samia hajui?
 
Kimsingi Katiba hii iliyopo imetungwa na kikundi kidogo kabisa Cha Watu wanaCCM ambao idadi yao hawafiki hata Watu 50 enzi hizo za Utawala wa Mwl Nyerere. Huyu Samia yeye mwenyewe ameikuta tu hiyo Katiba tayari ipo na inatumika.
Je ya kusema usalama wa Taifa wakiua hawatakuwa na "hatua"
 
Tatizo sio kuteka tatizo wanateka na wanaua kisha wanarudisha Maiti au wanateka wanaua kisha Maiti wanabakia nayo hamtoiona popote, tatizo ndio linaanzia hapo, wanatumwa nendeni mkamteke fulani kisha ueni na wanaowatuma mboni wanajulikana
Tukubaliane kuna wapuuzi ndani ya vyombo viwili vya usalama (Polisi na TISS) àmbao wanafhani wanaisaidia CCM Kwa kuondoa wakosoaji kumbe wanaipaka matope. Kuna watu kama Cp Awaz wanaamini watapandishwa kuwa maIGP Kwa matendo hayo.
 
Kabisa
 
Sasa kwa miaka hii 3 ya Samia kitu gani kizuri kakifanya?kuuza bandari, kufukuza wamasai loliondo kuharalisha uhalamia wa babaake, kukopa pesa kila uchwao kwa maslahi yake na wachache wanaomzunguka na kuiweka nchi kama dhamana,,watz lazma tusimame imara na kuitoa ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…