Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,120
- 3,468
Katika simulizi ya SATIVA naye anasema walipofika sehemu kule Arusha baada ya kumwambia wanaenda kumalizana naye alianza kuwaza hadi tumbo likachafuka akawaomba ajisaidie haja kubwa, walimpa chupa ya maji, wakamfungua pingu wakamuelekeza sehemu aende ajisaidie. Baada ya kufika Katavi wakampeleka kando ya mto wakampiga risasi kisha wakamfungua mask na pingu na kuondoka.Nilikuwa nikifikiri pingu zinapatikana Polisi tu, lakini kumbe hata "watu wengine" wanaweza kuwa nazo!
"Watekaji" waliomteka marehemu Ally Kibao na hatimaye "kumpoteza", walikuwa na pingu. Lakini Jeshi la Polisi lilikana kuwatambua, kwa hiyo "hawakuwa" askari Polisi.
Waliojaribu kumteka Deogratius Tarimo nao walikuwa na pingu, lakini Jeshi la Polisi limedai haliwatambui!
Ikiwa hawakuwa askari wa Jeshi la Polisi, walitoa wapi pingu? Siku hizi zinauzwa "Kariakoo"?
Serikali itoe tamko rasmi kwamba askari yeyote asiye na uniform iwe halali ya wananchi kwasababu atakuwa amekiuka sheria na taratibu za kazi. Tumechoka kusikia UTEKAJI NA MAUAJI.