"Watekaji" wanatoa wapi pingu?

"Watekaji" wanatoa wapi pingu?

Nilikuwa nikifikiri pingu zinapatikana Polisi tu, lakini kumbe hata "watu wengine" wanaweza kuwa nazo!

"Watekaji" waliomteka marehemu Ally Kibao na hatimaye "kumpoteza", walikuwa na pingu. Lakini Jeshi la Polisi lilikana kuwatambua, kwa hiyo "hawakuwa" askari Polisi.

Waliojaribu kumteka Deogratius Tarimo nao walikuwa na pingu, lakini Jeshi la Polisi limedai haliwatambui!

Ikiwa hawakuwa askari wa Jeshi la Polisi, walitoa wapi pingu? Siku hizi zinauzwa "Kariakoo"?

Katika simulizi ya SATIVA naye anasema walipofika sehemu kule Arusha baada ya kumwambia wanaenda kumalizana naye alianza kuwaza hadi tumbo likachafuka akawaomba ajisaidie haja kubwa, walimpa chupa ya maji, wakamfungua pingu wakamuelekeza sehemu aende ajisaidie. Baada ya kufika Katavi wakampeleka kando ya mto wakampiga risasi kisha wakamfungua mask na pingu na kuondoka.

Serikali itoe tamko rasmi kwamba askari yeyote asiye na uniform iwe halali ya wananchi kwasababu atakuwa amekiuka sheria na taratibu za kazi. Tumechoka kusikia UTEKAJI NA MAUAJI.
 
Nilikuwa nikifikiri pingu zinapatikana Polisi tu, lakini kumbe hata "watu wengine" wanaweza kuwa nazo!

"Watekaji" waliomteka marehemu Ally Kibao na hatimaye "kumpoteza", walikuwa na pingu. Lakini Jeshi la Polisi lilikana kuwatambua, kwa hiyo "hawakuwa" askari Polisi.

Waliojaribu kumteka Deogratius Tarimo nao walikuwa na pingu, lakini Jeshi la Polisi limedai haliwatambui!

Ikiwa hawakuwa askari wa Jeshi la Polisi, walitoa wapi pingu? Siku hizi zinauzwa "Kariakoo"?

.
1731505074277.jpg
 
Huo mtaa inaonekana wanokaa hapo wote wanawake
 
Hujaelewa mkuu hebu soma tena.

Angekuwa kimbaumbau kama mimi sasa hivi si tungekuwa tunaongea mengine?
Si sabb ya unene wa mwili vimefanya wamuache..mbona walishamuweka pingu mkono mmoja? Mungu amempa ujasiri na nguvu kupambana nao..ukiwa kwenye hatari ya namna hii unaweza kupata nguvu ukawashinda hata watu 4 wenye nguvu kukuzidi, mwili umeumbwa kujilinda wakati wa hatari bila kujali umbo ulilo nalo.
 
Serikali itoe tamko rasmi kwamba askari yeyote asiye na uniform iwe halali ya wananchi kwasababu atakuwa amekiuka sheria na taratibu za kazi. Tumechoka kusikia UTEKAJI NA MAUAJI.
Sidhani kama kuna ulazima wa kusubiri hadi serikali kutoa tamko. Ni raia wenyewe tu kujiongeza na kufanya kile wakifanyacho kwa vibaka wanaokamatwa na kuchomwa moto. Hao wakamataji wasiofuata taratibu sahihi za ukamataji raia waseme nao kwa vitendo kama wafanyavyo kwa vibaka ili kukomesha tabia hii iliyokwishaota mizizi.
 
Unashangaa pingu?

Wana hadi gari za PT
Siku hizi gari za jeshi zinaandikwa "TANZANIA MILITARY" hawataki. tena jina la JWTZ

Tunaisubiria siku "Tanzania Military"na JWTZ waki corride kama kule sudan
 
Nilikuwa nikifikiri pingu zinapatikana Polisi tu, lakini kumbe hata "watu wengine" wanaweza kuwa nazo!

"Watekaji" waliomteka marehemu Ally Kibao na hatimaye "kumpoteza", walikuwa na pingu. Lakini Jeshi la Polisi lilikana kuwatambua, kwa hiyo "hawakuwa" askari Polisi.

Waliojaribu kumteka Deogratius Tarimo nao walikuwa na pingu, lakini Jeshi la Polisi limedai haliwatambui!

Ikiwa hawakuwa askari wa Jeshi la Polisi, walitoa wapi pingu? Siku hizi zinauzwa "Kariakoo"?

Tatizo lao wanafikiri wananchi wote ni form four failure kama wao.
 
Jiongeze Mkuu!!
Unaamini kuwa serikali haijui watekaji ni kina nani!?

Unaamini kuwa hatuko salama kiasi hicho kuwa Serikali haijui watesi wetu!!!?

Serikali ndio WATEKAJI WENYEWE!!
 
Badala ushangae watu wana smg 56typ ya polisi vilevile pamoja chines pistol za polisi..

Watu wako na I'd za polisi watu wanamilik kuanzia Og jungle comofleg kombat......

Achana na radio call 😂
Dunia imechafuka majirani kenya nao wanadai saivi mtu anakamatwa (kutekwa) kabisa mchana na hamumuoni tena
 
Jiongeze Mkuu!!
Unaamini kuwa serikali haijui watekaji ni kina nani!?

Unaamini kuwa hatuko salama kiasi hicho kuwa Serikali haijui watesi wetu!!!?

Serikali ndio WATEKAJI WENYEWE!!
Sahihi lazima inawajua, lakini kwanini wananchi tufanyiwe haya ikiwa ni nchi yenye misingi ya sheria ambayo wanadai kuisimamia
 
Back
Top Bottom