Watendaji wa Taasisi 20 Nchini wasimamishwa kazi kwa kukiuka Sheria za manunuzi

Watendaji wa Taasisi 20 Nchini wasimamishwa kazi kwa kukiuka Sheria za manunuzi

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Serikali ya Tanzania imewasimamisha kazi watendaji 20 wa taasisi mbalimbali kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Akizungumza leo Jumatano Novemba 27, 2019 katika jukwaa la 12 la ununuzi wa umma la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema watumishi hao walikiuka sheria na taratibu za ununuzi wa umma hali inayorudisha nyuma mfumo wa ununuzi mitandaoni.

Dk Kijaji amesema taasisi ambayo haitatumia mfumo wa ununuzi kwa njia ya mtandao itafutiwa usajili wake kwa maelezo kuwa lengo la Serikali ni kuongeza thamani halisi ya fedha kupitia EAC.

"Sekta ya manunuzi imejaa rushwa kutokana na baadhi ya watendaji kutofuata sheria za manunuzi ya umma kwani tukijadiliana kwa pamoja na kubadilishana uzoefu tutaweza kutambua changamoto za manunuzi kwa umma," amesema naibu waziri huyo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alizungumzia utalii mkoani humo, “kupitia vyanzo hivi Mkoa wa Arusha huchangia mapato yake zaidi ya asilimia 15 katika sekta ya utalii. Wageni mnakaribishwa kutalii pia kwa wakazi wafanye utalii wa ndani ili kuendelea kukuza uchumi katika mapato na manunuzi kwa umma.”

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom