ACHENI KAZI IENDELEE NA RAIS #SAMIA Naa
YonaPAVEA
Nimeona malalamiko mengi Mitandaoni hasa kwa Veronica France Nginja Sham
Kimsingi Lazima tujiulize je waziri mkuu amepata wapi hiyo ripoti?
Maake Waziri wa Fedha ameteuliwa Juzi juzi tu na ameapishwa tarehe 01/04/2021 na kwa kuwa wizi umefanyika kipindi hicho labda wezi walitumia uchochoro huo wa Mabadiliko kuiba, na ndo kwanza waziri ameingia ofisini na Waziri mkuu tumemuona na ripoti ya pesa kutolewa haraka haraka mwezi wa nne mpaka wa tano, Lazima wenye Akili tujiulize nani amempa ripoti na nani alimuita pale?
Mimi naamini waziri mkuu anafanya kazi kubwa kama msaidizi wa Karibu wa Rais wetu Mama Samia na ndo Maana tulimuona Mama anamsifia kwa Kazi nzuri hasa Kuhusu magari ya mwendo Kasi UDART.
Na tutambue kila Kiongozi Ana approach yake kiutawala, yawezekana JPM alikuwa akisikia Kitu anachukua Hatua hapo hapo, ila yawezekana Mama #SSH yeye approach yake Ni kujipa siku kadhaa anachukua Hatua, jiulize siku ile waziri mkuu alipofika makao makuu ya UDART UDART akakuta madudu, ila Rais Mama Samia alijipa muda kutafuta Mkurugenzi mpya na leo Mhede kapelekwa pale.
Mama #Samia Ni Mama na Mama hawezi wapatia watoto wake Sumu.
Nasema na namalizia utendaji wa Rais wetu Mpendwa Mama Samia Ni utendaji mzuri na Ni Ule Ule wa Hayati mpendwa wetu JPM, Lakini tambua hatacopy na kupeste kila kitu, atatumia approach nzuri Zaidi kutufikisha Watanzania Kwenye Maendeleo yaliyopiganiwa na watangulizi wake, tena yeye Ana uwanja wa kuchukua kwa woote Mazuri na akaongeza na mengine Mazuri.