Water tanks na kutengeneza kisima

Water tanks na kutengeneza kisima

LadySwa

Member
Joined
Jan 25, 2009
Posts
77
Reaction score
6
Wakuu salaamaleikum.Naomba msaada wa hili.kwa wanaokaa Dar mwenye uzoefu atusaidie
kipi nafuu Kutengeneza kisima cha maji au kununua Water tanks.Karibuni
 
Ukinunua Water Tanks, maji utayapata wapi?
Kuchimba kisima kunategemea upatikanaji wa maji eneo ulilopo. Je umeshapima maji chini ya ardhi yanapatikana mita ngapi? Kila mita itakugarimu hadi laki moja kuchimba, je gharama umizifikiria?
Wengine watakushauri zaidi.
 
Lady Siwa:
Naona maelezo yako ni tata lakini nafikiri unataka kujua kuhusu masuala ya gharama za ujenzi wa kisima ( kwa minajili ya kuvuna maji ya mvua au kuifadhi maji kwa muda mrefu) kwa kulinganisha na gharama za kununua tenki la maji (liwe la chuma au la plastic).

Wasalaam,

Shadow.
 
Wenye uzoefu watujuze tafadhali, hasa kwa suala la gharama za ujenzi wa kisima cha lita 10,000 au Mapipa 2 ya SIm tank ya ujazo wa lita 5000 kila moja ambayo nafikiri yatagharimu tshs 2m hivi.
 
Fafanua kidogo, unaweza ukajenga kisima kwa ajli ya kuvuna maji ya mvua kwa matumizi ya muda mrefu au unaweza kuchimba kisima (drilling) kwa ajili ya kupata maji chini ya ardhi, wewe hapa ni kipi unahitaji kufanya?
 
Naona ametupia thread akatimka zake. Subirini akirudi afafanue
 
mbona yuko wazi!!

hapa anamaanisha kisima cha kuhifadhia maji ya mvua au maji ya kununu ili alinganishe gharama za kununu simtank na za ujenzi wa hicho kisima!
 
hapa maneno ndiyo yanayochanganywa

kisima- water well ; hichi ni chanzo cha maji

reserviour tank/storage tank; hii hutumika kuhifadhi maji kutoka kwenye chanzo chochote kile inaweza kuwa maji ya kuchotwa au mvua, pia reserviour/storage tank inaweza kujengwa kwa kuchimba chini, katika ground level au ikawa suspended (juu)

reserviour/storage tank yaweza kuwa ya concrete blocks, reinforced concrete, galvanized steel au UPVC (poly plastic)

mdau anataka kujua ajenge reserviour/storage tank ya kuchimba chini either kwa blocks au reinforced concrete, la au anunue poly tank kama vile simtank

ushauri, kama una source ya maji ya bomba au unaleta na water boozer na unahitaji kuingiza maji ndani ya nyumba na kuyatumia kwa water tapes, nunua poly tank halafu suspend it kwa kuijengea stand ili maji yaingie ndani kwa gravity,

gharama zinaweza kuwa alittle bit plus or minus equal, ila tank la kuchimba na kulijenga ni durable zaidi, kama una uwezo unaweza kujengea chini na ku install water pump ili maji yaingie ndani ya nyumba
 
Ukinunua Water Tanks, maji utayapata wapi?
Kuchimba kisima kunategemea upatikanaji wa maji eneo ulilopo. Je umeshapima maji chini ya ardhi yanapatikana mita ngapi? Kila mita itakugarimu hadi laki moja kuchimba, je gharama umizifikiria?
Wengine watakushauri zaidi.
laki moja kuchimba kisima? au ni typing error?Sina hakika muuliza swali una maanisha kisima chenye chemchem ya maji au just kujengea tanki la kuhifadhi maji ya bomba aridhini.kama ni deep well kwa sasa gharama ya uchimbaji ni kati ya 4M hadi 8M,inaweza ongezeka au kupungua kidogo kutokana na mahali ulipo. kama una maji yanatoka atleast once per week, kununua tank ni economical.but kua na kisima ni wazo jema kwa wasio na mabomba ya maji.
 
Ukinunua Water Tanks, maji utayapata wapi?
Kuchimba kisima kunategemea upatikanaji wa maji eneo ulilopo. Je umeshapima maji chini ya ardhi yanapatikana mita ngapi? Kila mita itakugarimu hadi laki moja kuchimba, je gharama umizifikiria?
Wengine watakushauri zaidi.

Mkuu kwenye nyekundu siyo sahihi hata kidogo, vinginevyo watu wachache sana wangemudu gharama za kuchimba visima. Nina quotation ya kuchimbiwa kisima cha mita 80 kwa mil. 2.9 tu jijini DAR. Kwa maana hiyo kila mita ni Tshs.36,250 tu.
 
Ningependa kufahamu bei ya poly tank.tafadhali lita 5000.na lita 10000
 
Mkuu kwenye nyekundu siyo sahihi hata kidogo, vinginevyo watu wachache sana wangemudu gharama za kuchimba visima. Nina quotation ya kuchimbiwa kisima cha mita 80 kwa mil. 2.9 tu jijini DAR. Kwa maana hiyo kila mita ni Tshs.36,250 tu.

Kaka ni quotation ya kampuni gan? Nisaidie contact zao katika pm, nataka kuchimba kisima next month
 
Wakuu salaamaleikum.Naomba msaada wa hili.kwa wanaokaa Dar mwenye uzoefu atusaidie
kipi nafuu Kutengeneza kisima cha maji au kununua Water tanks.Karibuni

Jitose tu mkuu ujipinde na uite wataalam wapime na ku drill wachomeke bomba!! maji safi na unakuwa huna bugdha na mtu. sana jirani atakuomba aunge bomba yake. na hapo unajua mwenyewe nini kinafuata. kila la kheri
 
Chonde chonde usije chimba kisima bila kuwasiliana na jamaa wa Ubungo maji pale bse watakushauri kama kuna chumvi etc
Kuna jamaa alichimba maeneo ya tabata full chumvi kila baada ya mda lazima abadili pump zile submersible which cost almost 1mil.
Kama una source ya uhakika ya maji kheri nunua SIMTANK sio POLYTANK bse nina uzoefu wa kutumia hayo matank for 10 years now.Kama una lolote kwenye iyo fani npm as nina kisima sasa kina mwaka wa kumi in operation!
 
polytank lita 5000 nimenunua kwa sh 750,000/= last year mwezi wa desemba pale mwenge

Hilo ndio tatizo letu wabongo.. tunapenda kununua vitu sehem za kisharobaro ukitaka tank wewe nenda buguruni kwenye wauzaji wakubwa wanaonunua mojakwa moja toka kiwandani. kwa tanki lako la 5000 lt unaweza uka-save hadi sh 150,000 na wakati usafiri gharama itaongezeka kwa sh 10,000 tu
 
Ndugu yangu ungesema hilo mapema nisingeuliza mara 2,Buguruni sehemu gani na hiyo ya lita 5000 wanauzaje?
 
hii bei ya mwaka gani jamani.

2007, RC rig ilikuwa inachimba mita 1 kwa USD40, au hawa wanatumia nini kuchimba?

Back
Top Bottom