Wateule wa Rais: Je, wanafanana? Kuna wengine kama wameokotwa tu, na wengine ni wapakwa mafuta Msijilinganishe

Wateule wa Rais: Je, wanafanana? Kuna wengine kama wameokotwa tu, na wengine ni wapakwa mafuta Msijilinganishe

Siku Ninapoteuliwa Najua Nitatoka kwa kumaliza kazi yangu ama kwa mteuzi wangu (Rais) atakapomaliza muda wake ingawa pia hata anayemfuata anaeza kuniona nafaa zaidi akaniacha kwa nafasi hiyo hiyo ama kunipandisha (mfano wa haraka haraka ulishautoa wewe hapo juu ...PMakinda aliteuliwa na JK kuwa dc JPM aliingia na akamuacha kwa nafasi hiyo hiyo hadi alipompandisha kuwa RC,) Pia naweza kufukuzwa/ kutumbuliwa ama kupangiwa kazi nyingine.

Ni uzuzu kimba kuogopa kufanya kazi yako na kutekeleza majukumu yako, kusimamia sheria just because unaogopa kutumbuliwa because of being classified "wakupakwa mafuta /wakuokotwa" Mtu yeyote mwenye uelewa na anaejua kazi yake hayumbishwi, wala hateterekei uamuzi utakaomfuata baada ya kusimamia majukumu yake. Ndio maana kuna kufukuzwa, kujiuhuzuru pia zote hizi ni njia za kuonyesha uwajibikaji, n some of them became heroes! Usimhurumie sana Nape, sometimes in life you have to pass through a lot to conquer. Ni dhahiri hata coach wa team ya kandanda akitofautiana na mchezaji one of them should depart ila heshima hubaki palepale (kwa wapenzi wa kandanda refer Etoo na Pep pale Catalunya) Vyeo/ Cheo sio Utu. maisha hayasimami, hata kama nimepakwa mafuta kama Sauli wa kwenye biblia, Nina mwisho. kiongozi yeyote aliyekamilika hana mawazo mtepeto kama hayo.

NI KOSA TENA HAIFAI KUSHADADIA uvunjaji wa sheria kwa kiongozi. Huwezi kuamua kuvunja sheria unayoijua kwa kuwa una upako wa mafuta na upenyo wa kutoa msaada. msaada ni suala pana sana sio kama tunavyofikiria. KUNA UTARATIBU UFUATWE. sio crisis ni situational.
Mpakwa mafuta ndio,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mkuu umeyaona yale masofa, daah sipati picha mwalimu mkuu anavyojiegemeza huku anafanya majukumu yake ya kikazi, jitihada nzuri km zile ni mbaya sana kuzibeza, Makonda kaenda kuleta msaada wa makochi ya hadhi ya hotelini tutumie mashuleni, ili walimu wajiskie vizuri wakiwa wanapiga kazi zao, afu mtu anasema yale yauzwe kweli, sio uonevu huu

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
images (2).jpeg

DC sabaya
 
Wanabodi,
Waziri Mpango alivyojibu.


Wito wangu kwa hawa wateule wa rais, wasijilinganishe wakajidhania wako sawa!. Wengine wameokotwa tuu na wengine ni wapakwa mafuta!, msifanye kabisa mchezo wa kushindana na wapakwa mafuta hawa, au kujifanya kutunishiana nao misuli, mtaumia!.

Hamjifunzi tuu kwa kilichomkuta Nape, alikuwa ni waziri aliyefiti sana vizara ile ambayo kwa maoni yangu, hadi sasa bado imepwaya, Nape alipo bonyeza tuu a wrong button, alikwenda na maji!. Sasa Dr. Mpango ndio anatikisa kiberiti kukipima kama kimejaa kwa kumchezea simba sharubu...!.

Mwacheni Mungu, aitwe Mungu!.

P.

Kwa kweli ni muhimu sana kijifunza kuweka akiba ya maneno, mtu unayemponda leo, huwezi jua kesho atakuwa nani!.

Hongera Dr. Mpango kuwa Makamu wa Rais na JMT.
Paskali
 
Kwa kweli ni muhimu sana kijifunza kuweka akiba ya maneno, mtu unayemponda leo, huwezi jua kesho atakuwa nani!.

Hongera Dr. Mpango kuwa Makamu wa Rais na JMT.
Paskali
Hongera kiongozi Kwa kulitambua Hilo
Tunashauriwa kushindana Kwa hoja na si Kwa ubinafsi WA MTU alivyo
 
Wanabodi,
Declaration of Interest.
Paskali ni raia mwema wa nchi hii, na kila raia mwema wa nchi yake, atahitaji kuona sheria, taratibu na kanuni zikifuatwa ikiwemo ulipwaji kodi ambazo ndizo fedha za kuendesha serikali, hivyo hili sio bandiko la kuchochea ukwepaji kodi!. Tena mimi nimejibanisha kuwa mzalendo wa kweli wa taifa langu, sio tuu kwa kuhamasisha zile kodi tuu zilizopo kwa mujibu wa sheria ndio zilipwe, bali nimehamasisha hata wale wanaokingwa na sheria wasilipe kodi, nimehamasisha sheria zibadilishwe, kila Mtanzania alipe kodi without exception Kuepuka Double Standards ya Kodi, Nashauri Rais Uongezwe Mshahara, Ili Alipe Kodi, Wote Tulipe Kodi! - JamiiForums

Hili sakata la makontena ya Makonda, kiukweli kabisa, linaweza kuja kuishia kwa kuwagharimu baadhi ya viongozi wetu waadilifu kama Waziri Dr. Mpango na watendaji wa TRA, kwa kuinflate kiwango cha kodi kwa samani used items, ili kumkomoa Makonda kwa kumkwamisha!.

Kitawacost sio kwa kutumbuliwa, bali kitawacost kwa kuumbuka na aibu ya makontena hayo kushindwa kuuzika!. Makontena ni 20, ushuru uliokadiriwa ni 1.2 billion, hii maana yake kwa rough estimates, kila container limekadiriwa ushuru wa TZS milioni 60!. Tumeona baadhi ya makontena yamefunguliwa na kushuhudia kilichomo, tuambizane ukweli, kuna mtu kweli wa kulipia milioni 60 kwa zile samani?!. Labda kama kuna baadhi yana Landrover Range Rover Sports hatukuonyeshwa, lakini kwa kile tulichoonyeshwa, hakuna mnada wowote wa kweli pale, labda ni procedures tuu kuhalalisha kuyataifisha, kisha yakagawiwe popote ikiwemo jimbo la Manyovu!.

Angalizo jameni, msiwachezee wapakwa mafuta, watu wanaweza kuja kuwajibishwa kwa jinsi ile ile lile sakata la uvamizi wa Clouds Media lilivyo mgharimu Waziri wetu muadilifu na mchapakazi Nape!.

Kama huko nyuma tumewahi kutoa misahaha ya kodi ya ajabu kabisa!, kwa nini tushindwe kusemehe samani hizi za waalimu masikini wa Dar es Salaam?!.

Nimeshuhudia baadhi ya viongozi ambao wote ni wateule wa rais, wakitunishiana misuli ya kuonyeshana nani zaidi kwa kisingizio cha kufuatwa kwa sheria, taratibu na kanuni!. Sijui nani kawaeleza kuwa Awamu ya Tano kila kitu ni sheria, taratibu na kanuni?!, labda kama ndio waanze sasa na kuanzia kwenye makontena ya Makonda!.

Hili ni bandiko la swali kuhusu wateule wa rais, kwa vile wote wanateuliwa kushika nyadhifa mbalimbali kwa sifa tofauti tofauti, na mteuzi ni yule yule mmoja ambaye ni rais wa JMT, sasa kuna baadhi ya wateule wameanza kujisahau na kuanza kuota pembe kwa kujiona kwa vile wote ni wateule, then wote wako sawa mbele ya mteuzi, kumbe sivyo!.
Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote! - JamiiForums

Kuna wateule na wateule!. Swali ni jee wateule wote wanafanana?, au kuna wateule ni kama wamefanywa kuokotwa tuu kutokana na impressive CV zao, au track records zao za nyuma, hivyo rais amewateua kwa merits za CV zao tuu, na wasipo prove by performance, wanatenguliwa au kutumbuliwa bila huruma.

Lakini kuna wateule, ambao hawa ni wapakwa mafuta na Bwana mwenyewe ambao wamepata uteuzi kutokana na nyota zao kung'aa baada ya ku prove ku delivery by performance, hawa kazi yao ni delivers the results not necessarily kufuata sheria inasemaje, na hata wakifanya makosa gani, hawa watavumiliwa, au ikibidi kubembelezwa wajiuzulu!.
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam - JamiiForums

Sasa wanapotokea viongozi wa kama ni wa kuokotwa ambao ni wafuata sheria, taratibu na kanuni, kushindana na wapakwa mafuta hawa wa Bwana, wanao delivers bila kujali sheria, taratibu na kanuni, automatically wakuokotwa wataumia!.
Je, Tanzania tunahitaji viongozi gani?. wajinga wachapakazi, au mangi meza wenye vyeti?. - JamiiForums

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, ni mmoja wa wapakwa mafuta hawa, kazi yake ni ku delivers regardless sheria zinasemaje. Hata afanye makosa vipi, atavumiliwa tuu na kuzumzwa kwa upole na unyenyekevu!.
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni - JamiiForums

Makonda ameyaona mateso ya waalimu wa nchi nzima wanavyoteseka na hali duni, akaguswa na mateso yao. Kwa vile mandate yake na jurisdiction yake ni jiji la Dar es Salaam tuu, akaanzisha kampeni ya ujenzi wa decent offices za waalimu, ikaitikiwa vizuri. Akazunguka dunia nzima kutafuta wafadhili wa vifaa vya ofisi hizo, wakapatikana, Watanzania waishio Marekani, wakaitikia vizuri, wito huo, wakajitoa, wakanunua vifaa vipya na kukusanya used na kuvisunda kwenye containers 36 na kuvituma Tanzania kwa jina la Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.

Containers 20 ndio hizi zimetangulia na hadi sasa zimekwama kwa hoja ya lazima zilipiwe ushuru wa bilioni 1.2!, kisa zimeandikwa Paul Makonda!, sasa zinauzwa kwa mnada, zisiponunuliwa, serikali inazitaifisha na kuzigawa bure shule zozote. Jee hizo containers 16 zilizobaki zitakuja?. Huku sii kuwakatisha tamaa wana Diaspora waliojitolea kuchanga kuisaidia Tanzania?!.

Hizi samani ni zawadi, tumesaidiwa na zilikuwa zigawiwe bure!, ushuru wa nini?!. Kwa vile Makonda ameilikabidhi jambo hili madhabahuni na kutoa laana, kama ni mpakwa mafuta wa kweli na Bwana mwenyewe, then ni kweli containers hizi hazitauzika!, na zikiuzwa kweli, atakayenunua yatamfika ya kumfika, na hata zikigawiwa bure, hizi tayari ni cursed items!, mpeni Makonda makontena yake, vinginevyo..., msije kusema hamkujua!, you were warned!.

Serikali inajinasibu kutoa billion 20 kila mwezi za elimu bure, unampa mwalimu aliyekalia vumbi, anafundishia kwenye ukuta hakuna ubao!, anajitokeza msamaria anajitolea meza, viti na ubao bure, mpe mwalimu ajisikie unamjali, wewe serikali hiyo hiyo inazuia!. Yaani serikali inazuia samani za bure kwa madai ya kodi ya bilioni 2!, alafu inatoa bilioni 20 kununulia samani za ndani zilizolipuliwa!, hapa tukiita serikali yetu ni serikali ya ajabu!, tutakuwa tumeionea?.

Makonda ameshitaki kwa Mungu, msililize hapa Waziri Mpango alivyojibu.


Wito wangu kwa hawa wateule wa rais, wasijilinganishe wakajidhania wako sawa!. Wengine wameokotwa tuu na wengine ni wapakwa mafuta!, msifanye kabisa mchezo wa kushindana na wapakwa mafuta hawa, au kujifanya kutunishiana nao misuli, mtaumia!.

Hamjifunzi tuu kwa kilichomkuta Nape, alikuwa ni waziri aliyefiti sana vizara ile ambayo kwa maoni yangu, hadi sasa bado imepwaya, Nape alipo bonyeza tuu a wrong button, alikwenda na maji!. Sasa Dr. Mpango ndio anatikisa kiberiti kukipima kama kimejaa kwa kumchezea simba sharubu...!.

Naoina ziara fulani ya kushtukiza ikifanyika bandarini hapo, na amri ya kimya kimya kuyaachia makontena yote ya Makonda ili tuu watu wasiaibike.

Pamoja na kutofautiana na Makonda katika baadhi ya maeneo, lakini kwenye hili la makontena ya samani za waalimu, nasimama nae!. Serikali inatoza kodi ya nini kwa kitu ilichopewa bure ambacho ingeigharimu mamilioni kukinunua?.

Mwacheni Mungu, aitwe Mungu!.

P.

Huu ni uzi wa swali la zamani, ila ni uthibitisho wateule hawafanani!.
Wanabodi, kwenye bandiko hili Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... nilishauri
Wanabodi,

Hili ni bandiko la kuhamasisha a mass mobilization ya kupata kundi kubwa la watu, kuunga mkono kwa dhati, juhudi kubwa zinazofanywa na Mkuu Mhe. Paul Christian Makonda, katika vita mbalimbali,

Hivyo hili ni bandiko la wito kwa kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki wa dhati, wanaomjua Makonda kwa karibu na kwa ukweli, njooni tujitokeze kwa wingi, kumtetea Makonda tunayemfahamu dhidi ya uongo na uzushi unaozushwa na kusambazwa na mapapa wauza unga

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Tujitokeze Kwa Wingi Kumtetea Makonda
Paskali.
Hata baada ya kuteuliwa kuwa Mwenezi wa CCM, Paul Makonda bado anapigwa vita na wasiomtakia mema, wasioitakia mema CCM na wasio itakia mema Tanzania.

Japo Tanzania ni nchi ya vyama vingi, na kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mamlaka kuu ya nchi ni wananchi, kupitia katiba, serikali ya CCM ilifanya mabadiliko ya katiba kinyume cha katiba na kupoka ukuu wa mamlaka kuu ya wananchi, na kuikakabidhi kwa chama cha siasa, ambapo sasa mamlaka Kuu ya nchi ni chama tawala, CCM ndio imeshika hatamu kuongoza serikali, hivyo katika ukuu wa chama, CCM ndio kila kitu, hivyo Makonda kama msemaji wa CCM, kikao cha CCM kinaweza kumwagiza Rais wa JMT atekeleze jambo lolote lililoelekezwa kwenye ilani ya CCM, Katibu Mwenezi ndie msimamizi wa ilani ya CCM, ana mamlaka yote ya kumuamrisha hadi Rais wa JMT, atekeleze ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo Makonda yuko very right kumuamrisha Waziri Mkuu na kumpa ultimatum ya miezi 6 kumaliza migogoro yote ya ardhi ya nchi hii.

Na baada ya miezi 6, kama Waziri Mkuu, Majaliwa Kasim Majaliwa atashindwa kuitatua migogoro yote ya ardhi, atakuwa ni ameshindwa kazi, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi, itakutana na kumuagiza Rais wa JMT, kumuondoa Waziri Mkuu, kwa kushindwa kazi na kumteua Waziri Mkuu mwingine mwenye uwezo.

Hata ikitokea Rais Samia ameshindwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, chama kinaweza kumfuta uanachama na hivyo kupoteza urais!, hivyo Mwenezi wa CCM ni mtu mkubwa sana, kuliko serikali yote ya Tanzania, na hii ndio maana halisi ya Party Supremacy, CCM ndio imeshika hatamu za kuiongoza serikali ya Tanzania .

Hongera sana Mwenezi mpya wa CCM, Paul Makonda, kuiheshimisha CCM, endelea kutoa maagizo na ultimatum kwa viongozi wote kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, wewe ndiye msimamizi wa ilani ya CCM!.

Angalia ilani ya CCM imeelekeza nini kuhusu Bunge la JMT, toa maelekezo kwa Spika with ultimatums, Spika akishindwa kutekeleza Spika anaondolewa!, enzi za Spika Sitta, aliponea chupu chupu kuondolewa, kuna mtu mmoja very powerful ndani ya CCM aitwae "The King Maker" ndie alimuokoa Spika Sitta kwa kumpa maelekezo Mwenyekiti wa CCM, JK, na hii ndio salama yake!.

Makonda angalia ilani ya uchaguzi ya CCM inasema nini kuhusu mhimili wa Mahakama, toa maagizo with ultimatum kwa Jaji Mkuu atekeleze.

Angalia ilani ya uchaguzi inasema nini kuhusu majeshi, ulinzi na usalama, toa maelekezo with ultimatum kwa Amiri jeshi Mkuu na kwa Mkuu wa majeshi, IGP , etc.

Ila kwa nafasi ambazo sio za kichama kama Jaji Mkuu, Mkuu wa Majeshi, CAG, Mwenyekiti wa NEC, Msajili wa Vyama vya Siasa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi, Mwenyekiti wa Tume ya Utawala Bora na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma ambao ni wateule wa rais, Paul Makonda anaweza kuwapa maelekezo bila ultimatums kwasababu hawa chama hakiwezi kuwafanya chochote, na badala yake, chama kitampa maelekezo mamlaka yake ya uteuzi ambaye ni Rais wa JMT, awaondoe!.

Kiukweli ninamkubali sana Paul Makonda!, Tangu nilipoanza kumkubali Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
He has never let me down!. Tena niliwahi kushauri Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... ushauri huu still stands, kwasababu miaka hii 4 ya Mama ni kumalizia awamu ya Magufuli, awamu ya baada ya Magufuli inaanza 2025, ila Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke hivyo you never know with politics, everything is possible!.

Paul Makonda kanyaga mwendo, chapa kazi, kazi iendelee!.
Paskali.
 
Back
Top Bottom