Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Wanabodi,
Declaration of Interest.
Paskali ni raia mwema wa nchi hii, na kila raia mwema wa nchi yake, atahitaji kuona sheria, taratibu na kanuni zikifuatwa ikiwemo ulipwaji kodi ambazo ndizo fedha za kuendesha serikali, hivyo hili sio bandiko la kuchochea ukwepaji kodi!. Tena mimi nimejibanisha kuwa mzalendo wa kweli wa taifa langu, sio tuu kwa kuhamasisha zile kodi tuu zilizopo kwa mujibu wa sheria ndio zilipwe, bali nimehamasisha hata wale wanaokingwa na sheria wasilipe kodi, nimehamasisha sheria zibadilishwe, kila Mtanzania alipe kodi without exception Kuepuka Double Standards ya Kodi, Nashauri Rais Uongezwe Mshahara, Ili Alipe Kodi, Wote Tulipe Kodi! - JamiiForums
Hili sakata la makontena ya Makonda, kiukweli kabisa, linaweza kuja kuishia kwa kuwagharimu baadhi ya viongozi wetu waadilifu kama Waziri Dr. Mpango na watendaji wa TRA, kwa kuinflate kiwango cha kodi kwa samani used items, ili kumkomoa Makonda kwa kumkwamisha!.
Kitawacost sio kwa kutumbuliwa, bali kitawacost kwa kuumbuka na aibu ya makontena hayo kushindwa kuuzika!. Makontena ni 20, ushuru uliokadiriwa ni 1.2 billion, hii maana yake kwa rough estimates, kila container limekadiriwa ushuru wa TZS milioni 60!. Tumeona baadhi ya makontena yamefunguliwa na kushuhudia kilichomo, tuambizane ukweli, kuna mtu kweli wa kulipia milioni 60 kwa zile samani?!. Labda kama kuna baadhi yana Landrover Range Rover Sports hatukuonyeshwa, lakini kwa kile tulichoonyeshwa, hakuna mnada wowote wa kweli pale, labda ni procedures tuu kuhalalisha kuyataifisha, kisha yakagawiwe popote ikiwemo jimbo la Manyovu!.
Angalizo jameni, msiwachezee wapakwa mafuta, watu wanaweza kuja kuwajibishwa kwa jinsi ile ile lile sakata la uvamizi wa Clouds Media lilivyo mgharimu Waziri wetu muadilifu na mchapakazi Nape!.
Kama huko nyuma tumewahi kutoa misahaha ya kodi ya ajabu kabisa!, kwa nini tushindwe kusemehe samani hizi za waalimu masikini wa Dar es Salaam?!.
Nimeshuhudia baadhi ya viongozi ambao wote ni wateule wa rais, wakitunishiana misuli ya kuonyeshana nani zaidi kwa kisingizio cha kufuatwa kwa sheria, taratibu na kanuni!. Sijui nani kawaeleza kuwa Awamu ya Tano kila kitu ni sheria, taratibu na kanuni?!, labda kama ndio waanze sasa na kuanzia kwenye makontena ya Makonda!.
Hili ni bandiko la swali kuhusu wateule wa rais, kwa vile wote wanateuliwa kushika nyadhifa mbalimbali kwa sifa tofauti tofauti, na mteuzi ni yule yule mmoja ambaye ni rais wa JMT, sasa kuna baadhi ya wateule wameanza kujisahau na kuanza kuota pembe kwa kujiona kwa vile wote ni wateule, then wote wako sawa mbele ya mteuzi, kumbe sivyo!.
Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote! - JamiiForums
Kuna wateule na wateule!. Swali ni jee wateule wote wanafanana?, au kuna wateule ni kama wamefanywa kuokotwa tuu kutokana na impressive CV zao, au track records zao za nyuma, hivyo rais amewateua kwa merits za CV zao tuu, na wasipo prove by performance, wanatenguliwa au kutumbuliwa bila huruma.
Lakini kuna wateule, ambao hawa ni wapakwa mafuta na Bwana mwenyewe ambao wamepata uteuzi kutokana na nyota zao kung'aa baada ya ku prove ku delivery by performance, hawa kazi yao ni delivers the results not necessarily kufuata sheria inasemaje, na hata wakifanya makosa gani, hawa watavumiliwa, au ikibidi kubembelezwa wajiuzulu!.
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam - JamiiForums
Sasa wanapotokea viongozi wa kama ni wa kuokotwa ambao ni wafuata sheria, taratibu na kanuni, kushindana na wapakwa mafuta hawa wa Bwana, wanao delivers bila kujali sheria, taratibu na kanuni, automatically wakuokotwa wataumia!.
Je, Tanzania tunahitaji viongozi gani?. wajinga wachapakazi, au mangi meza wenye vyeti?. - JamiiForums
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, ni mmoja wa wapakwa mafuta hawa, kazi yake ni ku delivers regardless sheria zinasemaje. Hata afanye makosa vipi, atavumiliwa tuu na kuzumzwa kwa upole na unyenyekevu!.
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni - JamiiForums
Makonda ameyaona mateso ya waalimu wa nchi nzima wanavyoteseka na hali duni, akaguswa na mateso yao. Kwa vile mandate yake na jurisdiction yake ni jiji la Dar es Salaam tuu, akaanzisha kampeni ya ujenzi wa decent offices za waalimu, ikaitikiwa vizuri. Akazunguka dunia nzima kutafuta wafadhili wa vifaa vya ofisi hizo, wakapatikana, Watanzania waishio Marekani, wakaitikia vizuri, wito huo, wakajitoa, wakanunua vifaa vipya na kukusanya used na kuvisunda kwenye containers 36 na kuvituma Tanzania kwa jina la Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Containers 20 ndio hizi zimetangulia na hadi sasa zimekwama kwa hoja ya lazima zilipiwe ushuru wa bilioni 1.2!, kisa zimeandikwa Paul Makonda!, sasa zinauzwa kwa mnada, zisiponunuliwa, serikali inazitaifisha na kuzigawa bure shule zozote. Jee hizo containers 16 zilizobaki zitakuja?. Huku sii kuwakatisha tamaa wana Diaspora waliojitolea kuchanga kuisaidia Tanzania?!.
Hizi samani ni zawadi, tumesaidiwa na zilikuwa zigawiwe bure!, ushuru wa nini?!. Kwa vile Makonda ameilikabidhi jambo hili madhabahuni na kutoa laana, kama ni mpakwa mafuta wa kweli na Bwana mwenyewe, then ni kweli containers hizi hazitauzika!, na zikiuzwa kweli, atakayenunua yatamfika ya kumfika, na hata zikigawiwa bure, hizi tayari ni cursed items!, mpeni Makonda makontena yake, vinginevyo..., msije kusema hamkujua!, you were warned!.
Serikali inajinasibu kutoa billion 20 kila mwezi za elimu bure, unampa mwalimu aliyekalia vumbi, anafundishia kwenye ukuta hakuna ubao!, anajitokeza msamaria anajitolea meza, viti na ubao bure, mpe mwalimu ajisikie unamjali, wewe serikali hiyo hiyo inazuia!. Yaani serikali inazuia samani za bure kwa madai ya kodi ya bilioni 2!, alafu inatoa bilioni 20 kununulia samani za ndani zilizolipuliwa!, hapa tukiita serikali yetu ni serikali ya ajabu!, tutakuwa tumeionea?.
Makonda ameshitaki kwa Mungu, msililize hapa Waziri Mpango alivyojibu.
Wito wangu kwa hawa wateule wa rais, wasijilinganishe wakajidhania wako sawa!. Wengine wameokotwa tuu na wengine ni wapakwa mafuta!, msifanye kabisa mchezo wa kushindana na wapakwa mafuta hawa, au kujifanya kutunishiana nao misuli, mtaumia!.
Hamjifunzi tuu kwa kilichomkuta Nape, alikuwa ni waziri aliyefiti sana vizara ile ambayo kwa maoni yangu, hadi sasa bado imepwaya, Nape alipo bonyeza tuu a wrong button, alikwenda na maji!. Sasa Dr. Mpango ndio anatikisa kiberiti kukipima kama kimejaa kwa kumchezea simba sharubu...!.
Naoina ziara fulani ya kushtukiza ikifanyika bandarini hapo, na amri ya kimya kimya kuyaachia makontena yote ya Makonda ili tuu watu wasiaibike.
Pamoja na kutofautiana na Makonda katika baadhi ya maeneo, lakini kwenye hili la makontena ya samani za waalimu, nasimama nae!. Serikali inatoza kodi ya nini kwa kitu ilichopewa bure ambacho ingeigharimu mamilioni kukinunua?.
Mwacheni Mungu, aitwe Mungu!.
P.