Wateule wa Rais: Je, wanafanana? Kuna wengine kama wameokotwa tu, na wengine ni wapakwa mafuta Msijilinganishe

Wateule wa Rais: Je, wanafanana? Kuna wengine kama wameokotwa tu, na wengine ni wapakwa mafuta Msijilinganishe

Kuna harufu nimenusa hapa! Jiwe anamnyoosha dogo inaonekana anajipromote mno! Unaingizaje msaada serikalini kwa jina binafsi? Pia kulikuwa na dalili za upigaji hapa kwanini makontena mengine yazuiliwe na mengine yaruhusiwe? Halafu ukiangalia jmn nadhani wenye nia njema ni watoa vifaa ila huyu dogo anatafuta misifa tuu! Ukimsaidia mwalimu/mtu kwa kutaka kuonekana hakuna baraka zozote kwa Mungu! Natamani ktk hili anyooshwe ili turudi kwenye mstari! 2020 sio mbali mkuu kajipambanua!!
 
Ukimsikiliza waziri mwenye dhamana, naona kama kuna contradiction ya ndani kwa ndani kama unatowa bn 20 kwanjiri ya shule hizo hizo, na umeakiki hizi samani nimisada na pia zinaenda pale pale unako paleka bn 20 kwanini unazikataza......hapo tatizo liko personal hataki mtoto teule aendelea kupata popularity nakupendwa na baba. Waziri kazi yake ingekua simple tu ni kusimamia kuona kwamba vinaenda kwa walengwa tu... aache kubishana na ujinga kasha boronga uchumi anafikiri watzn watampenda anajaribia kama alivo fanya kwenye korosho......watu wengine hawanaga maona anasema sheria ila azisomi zina sema je kuhusu misada kwajiri ya umma? Viongozi wa Africa wakipata madaraka wanakosa logic.

Sent using Jamii Forums mobile app

Prove kama ule ni msaada, au umekuwa msaada baada ya kuzuiwa bandarini?waziri anasimamia sheria alizoapa atazilinda, sasa asiposimamia anatumbuliwa kama akisimamia akitumbuliwa basi na iwe hivyo maana hata yesu aliteswa sana kwa sababu ya kusema yeye ni mwana wa mungu
 
Siongei kitu hapo,
ila ebu acha niongee kidogo hapa nadhani wote wako sahihi ila Makonda inabidi ajitahidi kufuata sheria kidogo,msamaha wa kodi ni ombi sio lazima kwamba unapewa tu kila unapohitaji. NA URAFIKI WA MAKONDA NA WAARABU NAO NI QUESTIONABLE PIA na wao tunajua wako kwny hiyo industry pia.Lkn kwa vile CCM ni chama kikongwe chenye wazee sidhani kama kuna kitu kitaharibika tofauti na ingekuwa ni ACT ambapo kukiwa na mgogoro kidogo tunaskia mbunge kapata ajali ndogo wakati akitokea Dodoma kwenda Dar na amefariki wakati dereva wake hata kucha moja haijatoka.
Kaka umeanza vizuri na kuharibu mwishowe. Hivi vyama na ulumumba/ufipa kina mahali hauhitajiki kabisa. Kama Uzi huu. Hatutafika kwa mtindo huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Pascal Mayalla naona na wewe unamshambulia waziri Mpango tena kwa maneno yenye ukakasi mkubwa. Mkuu kupitia kwenye mabandiko yako nafahamu kwamba umesoma sheria na umeelimika na kama wanavyoitana wanasheria basi huenda wewe ni learned brother. Kinachonishangaza hapa kwenye bandiko lako ni kuona kwamba unataka sheria zikiukwe! Mwanasheria anayetaka sheria zikiukwe ananipa wasiwasi mkubwa. Kwamba sheria zikiukwe kwa kuwa mmoja ni mpakwa mafuta na mwingine kaokotwa, kweli Pascal? Unataka impunity kwa wapakwa mafuta? Unataka sheria ifanye kazi kwa wengine ila si kwa wapakwa mafuta? Ninavyofahamu mimi sheria haina mpakwa mafuta wala mpakwa maji, bali ni msumeno.

Katika kuwafahamu kwangu wanasheria najua kwamba watakuwa wa mwisho kutaka sheria zikiukwe, hata kama ni sheria mbaya yaani bad laws, hadi hapo hizo sheria zitakapobadilishwa kwa kufuata sheria.

Nilitegemea utusaidie kwa kutuambia kwamba Waziri Mpango angetumia kifungu fulani cha sheria ili kusamehe kodi ya hizo samani badala ya kumdhihaki waziri anayesema sheria zifuatwe.
 
Prove kama ule ni msaada, au umekuwa msaada baada ya kuzuiwa bandarini?waziri anasimamia sheria alizoapa atazilinda, sasa asiposimamia anatumbuliwa kama akisimamia akitumbuliwa basi na iwe hivyo maana hata yesu aliteswa sana kwa sababu ya kusema yeye ni mwana wa mungu
Mkuu waziri angesema kwamba sio msada msililize vzr.....ajakanusha kama sio msada, sikiliza hiyo clip

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu hawawezi kuelewa unachozungumza hapa. Ni ngumu kuelewa sababu ya mfumo wetu wa kufikiri umetaifishwa,hatupendi kusoma na kuelewa mambo ya msingi. There are so many points in this thread but only who can see it will understand.others will never no matter what.watu wanapaswa kujua hili jambo si dogo hasa baada ya makonda kuamua kumshtaki kwa "mungu" wake.
 
Mkuu Pascal Mayalla hongera sana kwa hii makala, hakika wewe ni resource muhimu ndani ya jamii na JF.
Kiuhalisia, Mh. Mpango kaingia chaka sana ktk kulishughulikia hili suala.
Na kibaya kajibambanua kusema haogopi? Eti haogopi? Haogopi nini? Hamuogopi rais? Au?
Suala la walimu kwa Tanzania ni tete sana, lina maslahi mapana sana hasa kwa wapiga kula na zoezi la upigaji kura.
Mh. Mpango hajui iwapo hayo makontena yatapigwa mnada na walimu wakakosa hizo thamani maana yake itakuwa ni kete ya wapinzani kusema "walimu serikali haiwajali".
Mh. Mpango nadhani anajipalia makaa ya moto, very soon Naibu wake anakuja kuwa Waziri kamili wa Fedha!
 
Mkuu waziri angesema kwamba sio msada msililize vzr.....ajakanusha kama sio msada, sikiliza hiyo clip

Sent using Jamii Forums mobile app

Anasema ni msaada according to bill of lading ambayo inaweza kuwa kweli imeandikwa ni msaada lakini mwenye mzigo kafanya hivyo ili apitishe bila kodi.Hivi wew bashite humjui!? Ni kipi alichotamka kika materialize, usafi dar kila mwisho wa mwezi umemshinda akaja na ngonjera ya jkt watasimamia sasa ni mwezi hawapo mtaani na mengine mengi yard za magari zimejaa tele kila kona na huko kigamboni haendi mtu, uchawi wake utafika mwisho tu.
 
Mkuu Pascal Mayalla hongera sana kwa hii makala, hakika wewe ni resource muhimu ndani ya jamii na JF.
Kiuhalisia, Mh. Mpango kaingia chaka sana ktk kulishughulikia hili suala.
Na kibaya kajibambanua kusema haogopi? Eti haogopi? Haogopi nini? Hamuogopi rais? Au?
Suala la walimu kwa Tanzania ni tete sana, lina maslahi mapana sana hasa kwa wapiga kula na zoezi la upigaji kura.
Mh. Mpango hajui iwapo hayo makontena yatapigwa mnada na walimu wakakosa hizo thamani maana yake itakuwa ni kete ya wapinzani kusema "walimu serikali haiwajali".
Mh. Mpango nadhani anajipalia makaa ya moto, very soon Naibu wake anakuja kuwa Waziri kamili wa Fedha!
hajasema hamjali rais bali hamjali makonda mbele za mungu, hata kama hamjali rais pia hakumleta duniani ila ana uwezo wa kumuondoa na akimuondoa sii shida maana siku ikifika ataondoka sii kwa sababu ya bashite wala rahisi
 
Mkuu Kimbunga hebu leteni sheria ya misamaha ya kodi inasemaje?
Kwa uelewa wangu, rais anayo mamlaka ya kusamehe kodi, na suala kama hili Mh. Mpango alipaswa kushirikiana na Mh. Makonda, kuandika hiyo proposal na kuipeleka kwa Mh.Rais ili aone jinsi ya kulitatua na siyo alivyofanya Mh. Mpango. Refer kwenye kauli ya rais juu ya ushuru wa mazao, alishasema wananchi chukueni mazao kidogo kidogo ili mkwepe ushuru, sembuse hili! Ndiyo maana Mh. Mpango ajiandae kurudi huko alikokuwa, kama ni UDSM basi arudi huko huko, ana chuki na waalimu.
 
Naona we ni mtu uliejaa ukabila unamtetea ngosha mwenzio anaeonyesha kiburi badala ya busara misamaha ina taratibu zake angeifuata angepata msamaha ila kiburi kilitamalaki kwani hakuna alie juu ya sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom