Watibeli Hatupigagi Wake Zetu, na Binti zetu hawapigwi

Watibeli Hatupigagi Wake Zetu, na Binti zetu hawapigwi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
WATIBELI HATUPIGI WAKE ZETU, na BINTI ZETU HAWAPIGWAJI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Sisi Watibeli bhana ukiishi na Sisi unaweza fikiri hatuna hasira. Yaani mambo yetu tunayasuluhisha simple simple tuu. Yaani mpaka ugombane na Taikon basi ujue umemchokoa Sana, tena Sana. Hii ni Kwa sababu Watibeli ni Watu wa Amani. Tunapenda Amani na tunajiepusha na Shari.

Ni ngumu Mwanamke kuishi na Mtibeli akakosa Furaha. Hiyo haijawahi kutokea, tunasubiri siku itakapotokea tuite siku hiyo siku ya maajabu ya Dunia.

Watibeli hatuwapigi Wake zetu, na pia tumefundisha Binti zetu kutokupigwa. Vijana wakiume tumewafundisha kutowapiga Wanawake watakaowaoa.

Hakuna sababu hata Moja itakayomfanya Mtibeli ampige MKE wake, hata sababu Moja hakuna.
Mwanamke akiwa mkaidi Sana Watibeli tunamuacha, yaani Sisi kuandika Talaka ni dakika moja tuu.
Hatuna mioyo mizito katika utoaji wa Talaka. Kuliko umpige Mtu ni akheri kuachana. Hivyo ndivyo tulivyo.

Kwanza Sisi wenyewe hatupendi kupigwa. Ndio maana tunaitwaga Mr. Perfect Kwa sababu tunapenda ukamilifu(ingawaje sio wakamilifu) tunapenda kufanya mambo Kwa usahihi ili tusimkere yeyote.
Lolote ambalo hatutaki kufanyiwa hatuwezi kuwafanyia wengine. Ndio maana hatupigi wake zetu Kwa sababu Sisi wenyewe hatupendi kupigwa.

Na kamwe hatutamvumilia yeyote atakayethubutu kutupiga.

Ni marufuku na mwiko Kwa Binti zetu kupigwa hata Kofi moja Kwa kisingizio chochote kile. Hatunaga kitu inaitwa Msamaha kwenye kosa kama Hilo. Hakika lazima mpigaji awajibishwe kisheria, na kama sheria itakuwa inalegalega basi Kwa namna nyingine ambayo itamfanya mpigaji asitudie tena hata Kwa Watu wengine.

Watibeli wanapigana Kwa sababu kuu zifuatazo;
1. Umiliki wa Ardhi iwe ya familia, au Taifa Lao.
2. Familia kuguswa na maadui

Watibeli Sisi hakuna tofauti ya mtoto wa kiume na mtoto wa kike. Watoto wote NI sawasawa tuu. Ukioa Binti ya Tibeli basi jua umeolewa na huyo mtoto atakuwa ni Mtibeli upende usipende. Ukoo utatoka Kwa Watibeli. Atakuwa Mkeo na atakuhudumia kama MKE lakini elewa familia yenu itatambulika kama ukoo wa Tibeli.

Huwezi mpiga MKE wako hasa akiwa Mtibeli ukachekewa, hautachekewa asilani. Utawajibika Kwa namna ambayo haitafurahisha kama ulivyofanya.

Kumpiga mtu NI kosa la jinai. Ni udhalilishaji, ni dharau kubwa. Na kamwe huwezi mdharau Binti ya Watibeli Wakati Ndugu zake wapo.

Ndio maana Binti zetu tunawafunza kujiheshimu Kwa kujitegemea kisha kuheshimu wa Waume zao Kwa kuwa Wasaidizi. Na kamwe hatujawafundisha kuwa misukule na Watumwa.

Taikon nimemaliza, mwenye swali aweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
We hujawahi kubinywa naniliu wewe utampiga tu

Siwezi OA Mwanamke mpumbavu atakayefanya nimpige hiyo ni moja, pili, sheria na miiko yangu kama Mtibeli hainiruhusu kumpiga MKE wangu, kama amekuwa mkaidi tunafukuza pasipo vikao
 
Askari hawawezi nifanya kitu, sana sana Shitaka litafunguliwa afu litaishia hapohapo.

Uzuri sipigi kuua au kujeruhi

😀😀
Nakuambia hata Kofi moja tuu litatosha kuadabishwa na Askari waliosomea hizo kazi. Na ukitoka usipokuwa na adabu unakutana na kitu kizito cha Talaka
 
[emoji3][emoji3]
Nakuambia hata Kofi moja tuu litatosha kuadabishwa na Askari waliosomea hizo kazi. Na ukitoka usipokuwa na adabu unakutana na kitu kizito cha Talaka
Askari haruhusiwi piga mtuhumiwa.
Nyie wapare ondoeni ushamba
 
Leeni watoto wenu vizuri
Waelekezeni heshima
 
Back
Top Bottom