Watibeli tunaapa kwa Mungu pekee na haki; hatunaga kiapo kingine. Ukifuata Haki tutakulinda na kukutetea.

Watibeli tunaapa kwa Mungu pekee na haki; hatunaga kiapo kingine. Ukifuata Haki tutakulinda na kukutetea.

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Habari za Ijumaa!

Moja ya vitu vinavyotutofautisha Watibeli na watu wengine ni pamoja na hili.

Sisi hatunaga cha mzazi.
Hatunaga cha Mke/mume
Hakunaga cha Mtoto
Hatunaga cha Sijui Boss, sijui Mkurugenzi.
Hatunaga cha sijui Rais, sijui Rais, sijui Waziri.

Hatunaga cha Sijui kamanda wa jeshi, sijui Nani.

Vyeo hivyo vinafanya KAZI ikiwa wewe ni mpenda Haki. Mchamungu.
Na bahati nzuri wachamungu ni tofauti na wanadini.
Unaweza ukawa mwanadini lakini usiwe Mchamungu.

Hatunaga kiapo cha kulinda Mashetani hata siku moja.
Ukishakuwa kinyume na Haki Sisi watibeli hatunaga viapo na wewe.

Hata utupe Katiba,
Hata utupe Biblia,
Hata utupe Msahafu
Au kitabu chochote au kitu chochote tutumie kama ishara ya kiapo. Sisi hatunaga kiapo cha kutetea dhulma.

Kutetea na kulinda wenye dhulma ya wazi, tena walioamua kuwa wadhulmati.

Sisi watibeli, hata awe Mtibeli Mmoja hawezi kutishwa kutiii amri za maelfu ya watu hata wenye silaha lakini wanaamrisha dhulma.
Amri hizo ni batili. Na kamwe hatufuati.

Tutakubali kuishi Maskini.
Tutakubali kuishi gerezani.
Tutakubali maisha yoyote lakini kamwe hatuwezi kuwa upande wa dhulma. Kamwe.
Hasa dhulma iliyopitiliza.

Heshima yetu inatoka ndani yetu na sio nje.
Heshima ya kweli ni kutenda Wema na kufanya Haki.

Hatuhitaji na hatuwi proud kwa MTU yeyote, na hatuhitaji utukufu kwa yeyote zaidi ya Haki, kweli, na upendo.

Kwetu tunamheshimu muadilifu Maskini kuliko Tajiri asiyemuadilifu.
Tunaheshimu MTU wa chini kuliko kiongozi mkubwa asiye muadilifu.

Hivyo ndivyo tulivyo, tumezaliwa hivyo, na hakuna cha kutubadilisha.

Namaliza kwa kusema, Haki ituongoze, na kuwalinda Wote.

Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom