Watoto 300+ Dodoma kulishwa wali wenye virutubisho kutoka USAID

Misaada kama hii niliishuhudia miaka ya 60/70 nikiwa mtoto, naelewa wakati huo tulikuwa tumepata uhuru lakini hatukuwa na pesa za kuendesha nchi. Lakini wananchi walikuwa na uwezo wa kuzalisha chakula kwa ajili ya familia zao na kusaza.....Naona aibu na nashindwa kuelewa, msaada huu wa chakula wanapewa akina nani wenye njaa nchi hii?

Hivi kweli tumefikia hatua ya kuomba na kupokea misaada ya chakula wakati mkoa wa Kigoma pekee, bila kutaja Rukwa, Mbeya na Songea una uwezo wa kuzalisha chakula kinachoweza kutosha kulisha mikoa yenye shida ya chakula?😡
 
Wanaweza hata kupandikiza mambo ya ajabu humo kweli umasikini ni mbaya.
Mnapojadili haya mambo kwa namna hii mnajidhihirisha jinsi mlivyo mbumbumbu kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia. Bahati mbaya ni kwamba hata vijana wetu huko sekondari na vyuoni hawafanyi vizuri kwenye sayansi. Turudi kwenye mada, hivi ni nani asiyejua kwamba mbegu za mazao kama mahindi, maharage, mpunga nk kupitia programu za seeds improvement huwa zinaboreshwa ili kuongeza uzalishaji, ubora, virutubisho, kuhimili magonjwa nk? Nyie hamjasoma genetics vyuoni? Mbona pale SUA kuna Dr mmoja tena mwanamke aliboresha mbegu ya maharage ikawa bora zaidi? Je hamjaona mbegu za kisasa za mahindi, michungwa, maembe, korosho, minazi nk nk?? Jambo la pili je Tanzania hakuna mikoa inayoongoza kwa utapiamlo unaotokana na lishe duni na chache? Tatu je Tanzania hakuna shule za msingi ambazo watoto shuleni hata uji hawapati? Je wewe mleta mada umeshawahi walau kupeleka unga kilo 50, mafuta lita 5 na sukari kilo 5 kwenye shule iliyoko mtaani kwako ili wanafunzi wapate walau uji? Je hakuna wazazi ambao wakiambiwa walipe pesa za chakula ili watoto wao wapate chakula shuleni lakini wanagoma katakata? Mwisho niwaombe kwamba badala ya kukimbilia kupinga kila kitu, tutumie huu muda kuhamasisha na kuchangia watoto wetu wapate chakula shuleni. Kuna miaka ya nyuma nchi iliokolewa na unga wa Yanga (mahindi ya njano) ambao ulikuwa ni msaada kutoka Marekani, na watu walikuwa wanagombania.
 
Tuendeleee kuipongeza sri kali
 
Ungepelekwa tu sehemu zenye uhitaki mkubwa wa chakula kama Ethiopia, Madagascar na kwingine. Sasa bongo Michele yote hii na maharage Kila Kona kweli? Ama kunalingine?
 
Kuna ulazima sana kwa watawala wa kiafrika hususani watawala weusi na watu weusi (black people) kufanya kila namna wapate nakala zote za hotuba za watawala wa nchi ya Afrika ya Kusini chini ya Uongozi wa Wazungu wachache (Makaburu),. Hotuba hizo pamoja na nyaraka zingine mbalimbali za kiofisi za utawala wa Makaburu zina TAARIFA NYETI SANA na muhimu kwa watu weusi kuzijua taarifa hizo, watu weusi ni lazima tupate documents hizo na tuzisome na kuzielewa vyema kama kweli tunajitakia mema sisi pamoja na vizazi vyetu vijavyo.
Documents hizo zimekuwa zinaeleza kwa uwazi kabisa kuhusu haya mambo yanayoendelea kutokea hapa duniani, hususani kuhusu maisha ya watu weusi.
 
hizo ni kazi za historians, wacha wadeal nazo.
Mambo ya kiutawala ni mengi, mahitaji muhimu zaidi ya wanainchi ni mengi mno acha na wao pia wadeal na hayo yao 🐒
 
hizo ni kazi za historians, wacha wadeal nazo.
Mambo ya kiutawala ni mengi, mahitaji muhimu zaidi ya wanainchi ni mengi mno acha na wao pia wadeal na hayo yao 🐒
Siyo kazi ya historians, nilichoandika ninamaanisha na ninakielewa vyema sana, sijakurupuka kueleza Jambo hili kwenye mada hii iliyopo mezani.Je, una hanari kwamba utawala wa Makaburu ulianzisha mipango maalumu ya Siri kubwa katika kudhibiti rate ya kuzaliana kwa watu weusi nchini Afrika ya Kusini?Unayo habari hii? Clinics za Siri za kutekeleza mradi huo bado zipo hadi leo hii, unalijua Jambo hili?
Vile vile, walianzisha project nyingine ya Siri kuhusu introduction ya homosexuality kupitia njia ya chanjo (vaccination) na food production and supply chain.
Kumbuka: Projects zote hizi pamoja na nyinginezo walizoanzisha zilifanikiwa pakubwa sana na ufanisi wake upo juu hadi leo hii.
 
NI kweli uko sahihi kwa upande fulani lakini hawa wenzetu walio endelea ndio watunga sera za kuongoza Dunia.. wanaweza fanya chochote kile kutekeleza matakwa yao.
 
Sasa hivi Mambo si Mambo tena kwenye virutunisho wanaweza weka ata hormones zinazo pelekea mapenz ya jinsia Moja na kuongeza idadi ya watu hao nchini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…