Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Watoto watano wa familia moja wakazi wa kijiji cha Mswakini wilayani Monduli, Mkoa Arusha nchini Tanzania wamefariki dunia kwa ugonjwa ambao bado haujatambulika baada ya kusumbuliwa na maumivu ya tumbo na matumbo kujaa.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Julai 19,2022, Dwani wa Mswakini (CCM), Nanga Lenasira Mollel amesema vifo vya watoto vimetokea kwa nyakati kuanzia Julai 5 hadi leo ambapo amefariki mtoto mwingine aliyekuwa mgonjwa baada ya kubaki pekee Hospitali ya Mkoa Arusha ya Mount Meru Arusha
Amesema mtoto wa kwanza Bosi Nyangusi alifariki Julai5, 2022 kutokana na kusumbuliwa na tumbo.
Mollel amesema baada wanzake wanne walipelekwa hospitali ya TMA Monduli na wakapata matibabu na kuruhusiwa ila wakiwa njiani walizidiwa na kupelekwa Mout Meru, ambapo Julai 16 alifariki Saimalie.
Amesema baadae watoto wawili walifariki Julai 17 ambao ni Lemali na Sophia.
Diwani huyo amesema leo Jumanne mtoto aliyekuwa amebaki amelazwa hospitali ya Mount Meru amefariki dunia ambaye ni Veronica aliyekuwa anasoma darasa la tatu Mswakini.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mswakini, Nanga Karani amesema tangu kifo cha kwanza wamekuwa wakifuatilia chanjo bila kujua.
"Hawa watoto walikuwa wanalalamika kuumwa matumbo ambayo yalikuwa yanavimba, tumeuliza familia wamekula nini kibaya hawajui," amesema
Mmoja wa wanafamilia Lesono Lendoya amesema hawajui watoto walikula nini.
"Tunaomba uchunguzi wa hili jambo kwani linatushangaza," amesema
Mwananchi