Watoto hawana faida, hasa kwa masikini. Kuzaa watoto ni mateso ya kujitakia tu

Watoto hawana faida, hasa kwa masikini. Kuzaa watoto ni mateso ya kujitakia tu

kwaiyo sasa bosi mbona haujasema yupi kati ya hao uliowatag apo ndo ana kidonda sirini? au basi nimekumbuka hayanihusu.
Yaan ni hivi Mwanamke akikwambia Mimi ni mwanakwaya bro toka nduki Mwanamke akikwambia Mimi ni mlokole bro hio ni hatari toka nduki akikwambia Mimi nina kidonda cha Siri bro Wewe sio Dakota acha kumwonea huruma toka nduki,
 
Miaka ya 1980 kurudi nyuma watoto walikuwa sehemu ya nguvu kazi ya familia. Hivyo mtu akiwa na watoto wengi alihesabika kana kwamba anamiliki matrekta kadhaa ya kumsaidia ktk kilimo.

Siku hizi mambo yamebadilika. Watoto hawana thamani tena, sana sana wamegeuka kuwa sawa na kujitwisha zigo la misumari kichwani. Watoto wanateseka na mzazi anateseka.

Kuzaa tuwaachie matajiri ambao wana mali za kurithisha watoto wao. Wewe mwenye kajumba kamoja na gari lako la mkopo acha kuzaa, utatujazia vibaka na wadangaji mitaani.

Si mnaona mlundikano wa vijana ambao ni vibaka na madadapoa mijini na vijijini siku hizi? Au mnadhani hao vijana walijizaa?

Obama ana watoto 2.
W. Bush ana mtoto 1.
Clinton ana mtoto 1.
.
Wewe masikini unapata wapi ujasiri wa kuzaa watoto?
Pesa sina,hata watoto nikose hapana Haiwezekan
 
Watu wanazaa watoto sio sababu wana faida. Bali sababu wanataka familia. Familia ni kitu muhimu kwa binadamu kuhakikisha bado ni mzima kiakili. Ili waishi maisha kwa "sababu" na furaha wakiwa pamoja. Na mwisho wa siku wasife peke yao. Otherwise maisha hayana maana.

Wewe wazazi wako waliamua tu kukuzaa kwa sababu hizo nilizozisema ila bila kujua. Kama walikuzaa ili uje kuwa faida kwao basi ni sahihi wewe kuja na statement ya kipuuzi kama hii. Because it means you're a brainless pig. A literal pig. I mean it.

Personally nataka nipate watoto kama wanne hivi, na nataka nihakikishe tunaishi the best life on this planet. Na sio sababu nataka faida kutoka kwao.

Ukijiona hutaki kuja kuwa na familia basi wewe sio mzima kiakili au kimwili. Na pia kuna uwezekano utakuwa wale wanachama wa upinde wa mvua. Wale viumbe ni walishakufa kitambo imebaki miili yao inayonuka na kuchafua hali ya hewa duniani.

Wewe mleta mada utakuwa mmoja kati ya hayo.
 
Kwa dunia ya sasa ni kweli mkuu watoto hawana faida yoyote sana sana ni mitihani tu Mungu atuepushe nayo.

Vijana tunakufa tukiwa wadogo sio rahisi tena vijana wa sasa kuja kushuhudia mafanikio ya watoto wao.

Binafsi nimeshazika wazazi wangu wote wawili kwa nyakati tofauti na hakuna ata mzazi wangu 1 alieshuhudia mafanikio yangu ama kuyafaidi.

Kwa hatua kama iyo utasema kuzaa kuna faida gan mkuu ?
Tatizo tunazaa watoto wengi hata uwezo wa kulea hatuna hata kuwasomesha na kuwapa mitaji ya kibiashara mtu anataka azae watoto 8 pia hata wawili hana uwezo wa kuwatengenezea njia zuri za maisha hana, haya matatizo yako afrika sana.
 
Nakupa hii

Tunapoongelea swala la kuzaa kijiografia ni ongezeko la watu. Ongezeko la watu hutofautia baina ya nchi na nchi. Mfano kuna nchi zinauhitaji wa ongezeko la watu na kuna nchi inapaswa kupunguza au kudhibiti ongezeko la watu alkadhalika kuna nchi yenyewe inahitajika Just ku-balance tu ongezeko la watu na mfano wa nchi hizo ni za africa.
So nikirudi upande wako umuhimu wa kuzaliana kwa nchi yenye jiografia kama yetu bado upo. Wana demographic wanakwambia kuna nchi bado zipo katika hali nzuri kana kwamba wanaouwezo wa kuzalia hata watoto 12 na isiwe shida.

Issue ipo kwa watu binafsi, Serikali pamoja na mwiilngiliano kutoka mataifa ya magharibi.
Unaweza kuzaa watoto hata 30. Kama unawezo wa kuwamudu upo kuliko kuzaa watoto wengi hata kuwapa shibe huwezi hii ndo mwanzo wa kuzalisha
 
Kwa dunia ya sasa ni kweli mkuu watoto hawana faida yoyote sana sana ni mitihani tu Mungu atuepushe nayo.

Vijana tunakufa tukiwa wadogo sio rahisi tena vijana wa sasa kuja kushuhudia mafanikio ya watoto wao.

Binafsi nimeshazika wazazi wangu wote wawili kwa nyakati tofauti na hakuna ata mzazi wangu 1 alieshuhudia mafanikio yangu ama kuyafaidi.

Kwa hatua kama iyo utasema kuzaa kuna faida gan mkuu ?
Watoto hawana FAIDA kama wewe ulivyo hauna FAIDA Kwa taifa na wazazi wako maana na wewe ni mtoto wa mtu pia ....
 
Angalau tunakubaliana jambo moja kwamba watoto ni MUHIMU kwasababu ili binadamu waendelee kuwepo duniani ni lazima wazaliane

Utazaa wangapi na utawatunza na kuwaachia nini ni jambo la pili ambalo linajadilika kulingana na mtazamo wa mtu

Baba yangu alikua mtumishi wa umma alitutunza watoto 7 kwa kadiri ya kipato chake tukasoma shule za kayumba, hadi siku anafariki aliacha nyumba tu

Kabla hajafariki alipata changamoto ya magonjwa ya uzeeni lakini kwakuwa watoto wake watano tulikua tumekwishaanza kujitegema tulimuuguza kwa kadiri ya mahitaji yake yote hadi siku anafariki
Mama yetu bado yupo hai ni mzee lakini anapata matunzo stahiki kutoka kwa watoto wake wote tunafanya kazi zetu na tunajimudu kimaisha ingawaje sio matajiri

Japokua Baba yangu aliacha nyumba tu ambayo hadi leo ipo, sijawahi hata siku moja kuwaza kwamba Baba yangu alifanya KOSA kutokutuachia mali za kurithi...... NEVER
Malezi na elimu aliyonipa ilitutosha kabisa watoto wake wote kujimudu kimaisha

Haya ndio maisha ya waTz kwa kiasi kikubwa na haswa watumishi wa umma, urithi pekee wa MALI wanaoweza kuuacha ni nyumba gari na mashamba tu

Mkuu mtu hachagu pa kuzaliwa, ukijikuta umezaliwa na baba kuli mbeba mizigo kariakoo au konda au bodboda usipoteze muda kumlaumu baba yako kwasababu mfumo wa dunia unafanya lazima wawepo wafanya kazi hizo, nijukumu lako kupambana badala ya kutaka baba yako angekua kama Baba yake Mo Dewji aliemrithisha mwanae mabilioni

Na ondoa kabisa fikra kwamba eti kuli huyo hana HAKI ya kuzaa watoto kwa sababu ya umasikini wake...... maisha hayajawai kuwa fair hayapo fair na hayatakaa yaje kuwa fair kama tunavyotamani yawe

Hata kwa mujibu wa hekaya za Bibilia masikini walikuwepo na walitajwa kama wacha Mungu, wengine walikua watumwa na vijakazi kwa manabii, wengine walitoa senti zao za mwisho na sadaka zao zikawa kubwa kuliko matajiri nk nk

So kama wewe unapigania maisha ili wanao waje kurithi mali ni jambo jema pia...... lakini hii ni ngumu kwa watu wengi kama konda, bodaboda, shamba boy nk.
Lakini kwa walio wengi ni malezi elimu na kumrithisha spirt ya kupambania maisha yake kwa sababu wengi pia wanarithi mali ambazo zinakuja kuyayuka na kuja kuishi kwenye ufukara mbaya zaidi pengine kwasababu hawakuandaliwa kupambana
Mimi Nina mtazamo wangu nawewe una mtazamo wako, tuishi humo. Nimekulia familia duni mzee alifariki mapema hali kadharika na bi mkubwa pia. Kitendo cha mimi Leo kuweza kufanya mambo yangu freely, kuwapeleka watoto shule yenye ahueni na sio kayumba kwangu ni ushindi. Ila along the way ndio nikagundua kuzaa zaa hovyo ukiwa huna pesa ni umasikini zaidi. Tuishi
 
Unaweza kuzaa watoto hata 30. Kama unawezo wa kuwamudu upo kuliko kuzaa watoto wengi hata kuwapa shibe huwezi hii ndo mwanzo wa kuzalisha
Zaa kadri ya uwezo wako wa kuwahudumiaa!! Usisumbue wenzio kwa kuwakopa kuwa mara Leo unadaiwa ada, kesho chakula hakuna nyumbani watoto watalala njaa.....
 
Miaka ya 1980 kurudi nyuma watoto walikuwa sehemu ya nguvu kazi ya familia. Hivyo mtu akiwa na watoto wengi alihesabika kana kwamba anamiliki matrekta kadhaa ya kumsaidia ktk kilimo.

Siku hizi mambo yamebadilika. Watoto hawana thamani tena, sana sana wamegeuka kuwa sawa na kujitwisha zigo la misumari kichwani. Watoto wanateseka na mzazi anateseka.

Kuzaa tuwaachie matajiri ambao wana mali za kurithisha watoto wao. Wewe mwenye kajumba kamoja na gari lako la mkopo acha kuzaa, utatujazia vibaka na wadangaji mitaani.

Si mnaona mlundikano wa vijana ambao ni vibaka na madadapoa mijini na vijijini siku hizi? Au mnadhani hao vijana walijizaa?

Obama ana watoto 2.
W. Bush ana mtoto 1.
Clinton ana mtoto 1.
.
Wewe masikini unapata wapi ujasiri wa kuzaa watoto?
Nakazia
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Back
Top Bottom