Watoto hawana faida, hasa kwa masikini. Kuzaa watoto ni mateso ya kujitakia tu

Watoto hawana faida, hasa kwa masikini. Kuzaa watoto ni mateso ya kujitakia tu

Kwa dunia ya sasa ni kweli mkuu watoto hawana faida yoyote sana sana ni mitihani tu Mungu atuepushe nayo.

Vijana tunakufa tukiwa wadogo sio rahisi tena vijana wa sasa kuja kushuhudia mafanikio ya watoto wao.

Binafsi nimeshazika wazazi wangu wote wawili kwa nyakati tofauti na hakuna ata mzazi wangu 1 alieshuhudia mafanikio yangu ama kuyafaidi.

Kwa hatua kama iyo utasema kuzaa kuna faida gan mkuu ?
Mkuu kama wewe ni mkristo na unaamini katika maandiko, moja ya mstari katiba biblia unasema, Mithali 13:22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki. Mwisho wa kunukuu.

Agizo la kwanza la Mungu kwa wanadamu alipowaumba na kuwaweka katika uso wa nchi ni wazae na kuijaza dunia, lakini pia Mungu huyo huyo anataka uwaachie wajukuu zako urithi, yani uwape watoto wako mali na hadi wajukuu uwaachie urithi. Sasa mzazi asipotimiza wajibu wake ndio mambo yanakuwa hivyo. Tunaacha kujitafuta toka tuko watoto sababu wazee wetu wengine walikula bata sana hadi wanaondoka wanaacha laana na madeni.
Kwahiyo kwa mujibu wa Bibilia “maneno matakatifu ya Mungu” yanaelekeza masikini wasio na uwezo wa kuachia urithi hadi wajukuu basi wasizae watoto?

Mkuu watu wamekua soft sana siku hizi kwa kudhani ujinga na uzembe wao wa kupambania maisha yao ni jukumu la wazazi wao....... haujazaliwa na wazazi wako ili uje kurithi mali zao, umezaliwa ili uje KUISHI swala la utaishi namnagani ni juhudi zako

Uvivu unawafanya watu wanatengeneza maisha ya kufikirika ambayo hayapo kwamba wazazi wote wanapaswa kuwa matajiri na wakifa waache urithi kwa watoto wao....... hipo dunia ya namni hii
 
Miaka ya 1980 kurudi nyuma watoto walikuwa sehemu ya nguvu kazi ya familia. Hivyo mtu akiwa na watoto wengi alihesabika kana kwamba anamiliki matrekta kadhaa ya kumsaidia ktk kilimo.

Siku hizi mambo yamebadilika. Watoto hawana thamani tena, sana sana wamegeuka kuwa sawa na kujitwisha zigo la misumari kichwani. Watoto wanateseka na mzazi anateseka.

Kuzaa tuwaachie matajiri ambao wana mali za kurithisha watoto wao. Wewe mwenye kajumba kamoja na gari lako la mkopo acha kuzaa, utatujazia vibaka na wadangaji mitaani.

Si mnaona mlundikano wa vijana ambao ni vibaka na madadapoa mijini na vijijini siku hizi? Au mnadhani hao vijana walijizaa?

Obama ana watoto 2.
W. Bush ana mtoto 1.
Clinton ana mtoto 1.
.
Wewe masikini unapata wapi ujasiri wa kuzaa watoto?
Mi nitakuuliza: Unataka watoto wawili kwani wewe ni OBAMA?
 
Hiyo tafsiri ni mbovu kumbuka hata iweje hatuwezi kuepuka uwepo wa vibaka mjini hata vijijini, kwan binadamu hatupo sawa ,lakin hii pia imekuja kutupatia maana halisi ya kutegemeana,je kungekua hakuna vibaka polisi wangekua na kazi gani?
Hapo siyo kuacha kuzaa lakin tunatakiwa kuona namna gani mzuri ya kuwafanya hao watoto wapite kwenye njia sahihi ambazo watoto wa miaka 1980 walikua wanapita.

Wanapambaji wengi ambao wanatamba kwa sasa ni watoto wa masikini mfano hansrafael,hamornize,diamond na wengine wengi.
 
Tuzae watoto tunaoweza kuwahudumia sio kuzaa zaa tu kisa kizazi kipo. Huwa naona huruma unakuta vitoto vimepangana kama ngazi maisha magumu kusoma kwenyewe kwa tabu, chakula hawali wakashiba alafu mtu aje aseme zaa tu wakati ukijicheki wewe mwenyewe kujihudumia ni kisanga, haijakaa sawa.
Kabisakabisa
 
Mafundisho yadanganyayo Kwa sisi tunaosoma bible tu akuona kabisa kama unatekeleza agenda ya mpinga kristo kuwa watu wasioe hivyo wawakiane tamaa maana matokeo ya kuoa ni kuzaa hivyo unapingana na agizo la mungu kuwa zaeni muongezeke na kuijaza nchi.

Hivyo tamko lako Lina laani uumbaji wako mwenyewe na kukosoa hadi wazazi wako na kuvunja heshima ya wazazi wako( waeshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na bwana mungu wako)
Hivyo kijana umekwisha kuyatimba autaiona sasa laana inayoanza kukuandama ila nakusihi tubu na ulejee miguuni pa muumba wako na makosa yako yatasamehewa ( ijapokuwa dhambi zako ni nyekundu kama damu utasafishwa uwe kama theruji) akuna dhambi mbaya kama kukufuru.
 
Ukiwa na akili timamu huwezi shadadia kuzaa watoto wengi usioweza kuwamudu.
Zaidi zaidi ni kujiongezea na kuwaongezea shida hao watoto.
Watanzania wengi wanazaa bila mpangolio. Ndio maana kumejaa wahuni kila kona . Mtu ana watoto 6, kapanga chumba kimoja, kipato kwa siku elfu 10 , unategemea nini kwa mtu kama huyo. Unawapa shida watoto wako tu.
 
Shida ipo kwenye mgao wa keki ya taifa hatuna viongozi tuna watawala
 
Yaani nisizae kisa? Kwani huyo Obama ndio mimi? au sijui Clinnton hata nikijifanya nazaa mtoto mmoja nitawafikia kiuchumi? tuzae tu jamani tuzae mapori bado yapo mengi ya kutosha nchi kubwa hii
 
Miaka ya 1980 kurudi nyuma watoto walikuwa sehemu ya nguvu kazi ya familia. Hivyo mtu akiwa na watoto wengi alihesabika kana kwamba anamiliki matrekta kadhaa ya kumsaidia ktk kilimo.

Siku hizi mambo yamebadilika. Watoto hawana thamani tena, sana sana wamegeuka kuwa sawa na kujitwisha zigo la misumari kichwani. Watoto wanateseka na mzazi anateseka.

Kuzaa tuwaachie matajiri ambao wana mali za kurithisha watoto wao. Wewe mwenye kajumba kamoja na gari lako la mkopo acha kuzaa, utatujazia vibaka na wadangaji mitaani.

Si mnaona mlundikano wa vijana ambao ni vibaka na madadapoa mijini na vijijini siku hizi? Au mnadhani hao vijana walijizaa?

Obama ana watoto 2.
W. Bush ana mtoto 1.
Clinton ana mtoto 1.
.
Wewe masikini unapata wapi ujasiri wa kuzaa watoto?
Labda huelewi kuwa nchi zilizokuwa zinazaliana kidogo sasa hivi wanahaha watu wazae.

Unaonesha kwenu ilikuwa mnazaliana mpata watumwa.

AlhamduliLlah, Waislam tunafahamu kuwa watoto ni moja katika furaha za duniani.
 
Kwahiyo kwa mujibu wa Bibilia “maneno matakatifu ya Mungu” yanaelekeza masikini wasio na uwezo wa kuachia urithi hadi wajukuu basi wasizae watoto?
Je katika vifungu vya neno nilivyoviweka hapo juu Kuna maneno yoyote kati ya hayo uliyoweka? Kuna sehemu biblia imeandika masikini wasizae au ni utashi wako tu?

Kasome upya biblia mkuu, hata Mungu hakumuumba Adamu ndio akaanza kuumba vitu. Alianza kuumba vitu, biblia inasema aliumba mbingu na nchi, akaumba bahari. Maana yake hadi anamuumba Adamu na kumuweka bustani ya Eden ikiwa na kila kitu. Adamu alikula bata bustani ya Eden, aliishi soft life, hakutafuta kuni za kupikia wala kubeba mizigo kila kitu Mungu alikuwa amemuwekea kasoro mwanamke.

Turudi kwako wewe, ikiwa Mungu alifanya yote haya kwa Adam, wewe masikini huna kitu where do you get moral authority ya kuzaa zaa hovyo bila kuwaandalia watoto mazingira mazuri mwishowe wanakuwa chokoraa.
 
Back
Top Bottom