Namimi niache niamini umasikini ni dhambi, umasikini ni laana, umasikini unatweza. Sio mpango wa Mungu aliyeniumba eti nije niwe masikini and so far nilishatoka huko so nahangaika kuweka mifumo watoto wangu wasije chapa kaburi langu fimbo kwamba baba alikuja Duniani kucheza mziki, kufanya anasa ameshindwa kutuachia hata mali za kuanzia maisha eti kisa ametupa elimu.
Sio kwa umuhimu urithi wa mtoto kwa dunia hii sio elimu pekee kama ilivyokuwa miaka ya 80, mtoto mpe elimu, ujuzi na mali atayoiendeleza ndio elite wanafanya hivyo duniani.
Angalau tunakubaliana jambo moja kwamba watoto ni MUHIMU kwasababu ili binadamu waendelee kuwepo duniani ni lazima wazaliane
Utazaa wangapi na utawatunza na kuwaachia nini ni jambo la pili ambalo linajadilika kulingana na mtazamo wa mtu
Baba yangu alikua mtumishi wa umma alitutunza watoto 7 kwa kadiri ya kipato chake tukasoma shule za kayumba, hadi siku anafariki aliacha nyumba tu
Kabla hajafariki alipata changamoto ya magonjwa ya uzeeni lakini kwakuwa watoto wake watano tulikua tumekwishaanza kujitegema tulimuuguza kwa kadiri ya mahitaji yake yote hadi siku anafariki
Mama yetu bado yupo hai ni mzee lakini anapata matunzo stahiki kutoka kwa watoto wake wote tunafanya kazi zetu na tunajimudu kimaisha ingawaje sio matajiri
Japokua Baba yangu aliacha nyumba tu ambayo hadi leo ipo, sijawahi hata siku moja kuwaza kwamba Baba yangu alifanya KOSA kutokutuachia mali za kurithi...... NEVER
Malezi na elimu aliyonipa ilitutosha kabisa watoto wake wote kujimudu kimaisha
Haya ndio maisha ya waTz kwa kiasi kikubwa na haswa watumishi wa umma, urithi pekee wa MALI wanaoweza kuuacha ni nyumba gari na mashamba tu
Mkuu mtu hachagu pa kuzaliwa, ukijikuta umezaliwa na baba kuli mbeba mizigo kariakoo au konda au bodboda usipoteze muda kumlaumu baba yako kwasababu mfumo wa dunia unafanya lazima wawepo wafanya kazi hizo, nijukumu lako kupambana badala ya kutaka baba yako angekua kama Baba yake Mo Dewji aliemrithisha mwanae mabilioni
Na ondoa kabisa fikra kwamba eti kuli huyo hana HAKI ya kuzaa watoto kwa sababu ya umasikini wake...... maisha hayajawai kuwa fair hayapo fair na hayatakaa yaje kuwa fair kama tunavyotamani yawe
Hata kwa mujibu wa hekaya za Bibilia masikini walikuwepo na walitajwa kama wacha Mungu, wengine walikua watumwa na vijakazi kwa manabii, wengine walitoa senti zao za mwisho na sadaka zao zikawa kubwa kuliko matajiri nk nk
So kama wewe unapigania maisha ili wanao waje kurithi mali ni jambo jema pia...... lakini hii ni ngumu kwa watu wengi kama konda, bodaboda, shamba boy nk.
Lakini kwa walio wengi ni malezi elimu na kumrithisha spirt ya kupambania maisha yake kwa sababu wengi pia wanarithi mali ambazo zinakuja kuyayuka na kuja kuishi kwenye ufukara mbaya zaidi pengine kwasababu hawakuandaliwa kupambana