Watoto hawana faida, hasa kwa masikini. Kuzaa watoto ni mateso ya kujitakia tu

Watoto hawana faida, hasa kwa masikini. Kuzaa watoto ni mateso ya kujitakia tu

Mafundisho yadanganyayo Kwa sisi tunaosoma bible tu akuona kabisa kama unatekeleza agenda ya mpinga kristo kuwa watu wasioe hivyo wawakiane tamaa maana matokeo ya kuoa ni kuzaa hivyo unapingana na agizo la mungu kuwa zaeni muongezeke na kuijaza nchi.

Hivyo tamko lako Lina laani uumbaji wako mwenyewe na kukosoa hadi wazazi wako na kuvunja heshima ya wazazi wako( waeshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na bwana mungu wako)
Hivyo kijana umekwisha kuyatimba autaiona sasa laana inayoanza kukuandama ila nakusihi tubu na ulejee miguuni pa muumba wako na makosa yako yatasamehewa ( ijapokuwa dhambi zako ni nyekundu kama damu utasafishwa uwe kama theruji) akuna dhambi mbaya kama kukufuru.
Deputy God kazini 🤣
 
Yaani nisizae kisa? Kwani huyo Obama ndio mimi? au sijui Clinnton hata nikijifanya nazaa mtoto mmoja nitawafikia kiuchumi? tuzae tu jamani tuzae mapori bado yapo mengi ya kutosha nchi kubwa hii
Ushauri wa kifala sana huu, hayo mapori unayatumieje kama huna mtaji?
 
Ushauri wa kifala sana huu, hayo mapori unayatumieje kama huna mtaji?
hata kuwinda mkuu, kwani jamii za watindiga na wasandawe wana mitaji ya kuishi maporini, let say una watoto wawili au mmoja ndo umasikini hautakuwepo?, je hamna wachina masikini? wazungu masikini hawapo, wajapani masikini hawapo?
 
Je katika vifungu vya neno nilivyoviweka hapo juu Kuna maneno yoyote kati ya hayo uliyoweka? Kuna sehemu biblia imeandika masikini wasizae au ni utashi wako tu?

Kasome upya biblia mkuu, hata Mungu hakumuumba Adamu ndio akaanza kuumba vitu. Alianza kuumba vitu, biblia inasema aliumba mbingu na nchi, akaumba bahari. Maana yake hadi anamuumba Adamu na kumuweka bustani ya Eden ikiwa na kila kitu. Adamu alikula bata bustani ya Eden, aliishi soft life, hakutafuta kuni za kupikia wala kubeba mizigo kila kitu Mungu alikuwa amemuwekea kasoro mwanamke.

Turudi kwako wewe, ikiwa Mungu alifanya yote haya kwa Adam, wewe masikini huna kitu where do you get moral authority ya kuzaa zaa hovyo bila kuwaandalia watoto mazingira mazuri mwishowe wanakuwa chokoraa.
Mkuu hebu tuachane kwanza na hizi hekaya za Imani ya Mungu

Hakuna wakati dunia imewahi kuwa soft, life ni struggling to survive, we’re so many but resources are scary
Toka dunia hii imekua civilized imetengeneza mfumo ambao ni lazima “masikini”(wenye kipato kidogo na wastani) wawe wengi na mataji wachache. Masikini watatumikia matajiri.
Matajiri hao wachache watawarithisha watoto wao utajiri wao na masikini watazaliana ili kuendelea kutumikia matajiri...... NI MFUMO

Na katika huo mfumo kuna fursa ya Tajiri kuwa masikini na Masikini kuwa tajiri...... sasa hii dhana ya kudhani baba yako tu ndio alipaswa kuitumia hiyo fursa awe tajiri akurithishe ni fikra mfu, kama unadhani ni rahisi hivyo basi kuwa wewe tajiri
Una nafasi hiyo, acha kulia lia
Ukishindwa kutajirika basi zaa watoto na wape msingi wa kupambana badala ya kuwaambukiza dhana ya kuwa umasikini wao unatokana na wazazi wao kutowarithisha utajiri

Wewe kuzaliwa na kukulia kwenye umasikini sio kosa la wazazi wako.... ila wewe kufa masikini ni kosa lako na sio la watoto wako
 
hata kuwinda mkuu, kwani jamii za watindiga na wasandawe wana mitaji ya kuishi maporini, let say una watoto wawili au mmoja ndo umasikini hautakuwepo?, je hamna wachina masikini? wazungu masikini hawapo, wajapani masikini hawapo?
Kuwepo kwa Hao watu masikini haikupi wewe ticket ya kuukubali umaskini wako na kuanza kufyatua watoto eti kwa mawazo kila mtoto na sahani yake ukitegemea wahangaike na maisha waje wakutunze uzeeni, that's primitive bro. Leta mtoto ukiwa na uhakika wa maisha sio kuja kutesa kiumbe wa Mungu.
 
Mkuu hebu tuachane kwanza na hizi hekaya za Imani ya Mungu

Hakuna wakati dunia imewahi kuwa soft, life ni struggling to survive, we’re so many but resources are scary
Toka dunia hii imekua civilized imetengeneza mfumo ambao ni lazima “masikini”(wenye kipato kidogo na wastani) wawe wengi na mataji wachache. Masikini watatumikia matajiri.
Matajiri hao wachache watawarithisha watoto wao utajiri wao na masikini watazaliana ili kuendelea kutumikia matajiri...... NI MFUMO

Na katika huo mfumo kuna fursa ya Tajiri kuwa masikini na Masikini kuwa tajiri...... sasa hii dhana ya kudhani baba yako tu ndio alipaswa kuitumia hiyo fursa awe tajiri akurithishe ni fikra mfu, kama unadhani ni rahisi hivyo basi kuwa wewe tajiri
Una nafasi hiyo, acha kulia lia
Ukishindwa kutajirika basi zaa watoto na wape msingi wa kupambana badala ya kuwaambukiza dhana ya kuwa umasikini wao unatokana na wazazi wao kutowarithisha utajiri

Wewe kuzaliwa na kukulia kwenye umasikini sio kosa la wazazi wako.... ila wewe kufa masikini ni kosa lako na sio la watoto wako
Sasa mkuu tukubaliane kutokubaliana! Mimi ninasoma biblia naiamini misingi yake ndio inaniongoza. Wewe unaamini katika elimu dunia kwamba lazima masikini wawepo na matajiri wawepo basi ishi unavyoamini.

Namimi niache niamini umasikini ni dhambi, umasikini ni laana, umasikini unatweza. Sio mpango wa Mungu aliyeniumba eti nije niwe masikini and so far nilishatoka huko so nahangaika kuweka mifumo watoto wangu wasije chapa kaburi langu fimbo kwamba baba alikuja Duniani kucheza mziki, kufanya anasa ameshindwa kutuachia hata mali za kuanzia maisha eti kisa ametupa elimu.

Sio kwa umuhimu urithi wa mtoto kwa dunia hii sio elimu pekee kama ilivyokuwa miaka ya 80, mtoto mpe elimu, ujuzi na mali atayoiendeleza ndio elite wanafanya hivyo duniani.
 
Hiyo tafsiri ni mbovu kumbuka hata iweje hatuwezi kuepuka uwepo wa vibaka mjini hata vijijini, kwan binadamu hatupo sawa ,lakin hii pia imekuja kutupatia maana halisi ya kutegemeana,je kungekua hakuna vibaka polisi wangekua na kazi gani?
Hapo siyo kuacha kuzaa lakin tunatakiwa kuona namna gani mzuri ya kuwafanya hao watoto wapite kwenye njia sahihi ambazo watoto wa miaka 1980 walikua wanapita.

Wanapambaji wengi ambao wanatamba kwa sasa ni watoto wa masikini mfano hansrafael,hamornize,diamond na wengine wengi.
Ndiyo shida ya kuzaliwa nchi masikini, inafikia hatua tunaanza kuamini lazima uhalifu uwepo sababu baadhi ya ajira zitakuwa rehani. Mkuu fatilia nchi za Scandinavian unaambiwa crime rate ni ndogo kiasi kwamba Kuna muda Kuna 0% ya matukio ya uharifu!

Nchi imeweka Sera nzuri raia wanazaa kwa uzazi wa mpango, serikali inaweka na kutoa miundombinu rafiki ya kijamii hadi wasio na ajira Kuna ujira wanalipwa mwisho wa mwezi ili waweze kujikimu mambo muhimu ya kimaisha. Sasa mtu atoke akaibe ili iweje? Fatilia chi kama Brunei sio lazima ufike unaweza hata kusoma online.

Africa kufika huko ni ngumu sababu ya elimu, ubadhirifu wa mali za Uma na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Lakini cha muhimu kama huwezi kubadirisha dunia kwanini usibadirishe maisha yako binafsi? Kuna umuhimu gani wa kuwa na watoto 5 wakati uchumi wako unakuruhusu kuwa na watoto 2? Matokeo yako unaishi 70% of your life ukiteseka living paycheck after paycheck, collecting scraps under dumpsters! Creating a miserable failing generation, living under filthy living hoods!
 
Namimi niache niamini umasikini ni dhambi, umasikini ni laana, umasikini unatweza. Sio mpango wa Mungu aliyeniumba eti nije niwe masikini and so far nilishatoka huko so nahangaika kuweka mifumo watoto wangu wasije chapa kaburi langu fimbo kwamba baba alikuja Duniani kucheza mziki, kufanya anasa ameshindwa kutuachia hata mali za kuanzia maisha eti kisa ametupa elimu.

Sio kwa umuhimu urithi wa mtoto kwa dunia hii sio elimu pekee kama ilivyokuwa miaka ya 80, mtoto mpe elimu, ujuzi na mali atayoiendeleza ndio elite wanafanya hivyo duniani.
Angalau tunakubaliana jambo moja kwamba watoto ni MUHIMU kwasababu ili binadamu waendelee kuwepo duniani ni lazima wazaliane

Utazaa wangapi na utawatunza na kuwaachia nini ni jambo la pili ambalo linajadilika kulingana na mtazamo wa mtu

Baba yangu alikua mtumishi wa umma alitutunza watoto 7 kwa kadiri ya kipato chake tukasoma shule za kayumba, hadi siku anafariki aliacha nyumba tu

Kabla hajafariki alipata changamoto ya magonjwa ya uzeeni lakini kwakuwa watoto wake watano tulikua tumekwishaanza kujitegema tulimuuguza kwa kadiri ya mahitaji yake yote hadi siku anafariki
Mama yetu bado yupo hai ni mzee lakini anapata matunzo stahiki kutoka kwa watoto wake wote tunafanya kazi zetu na tunajimudu kimaisha ingawaje sio matajiri

Japokua Baba yangu aliacha nyumba tu ambayo hadi leo ipo, sijawahi hata siku moja kuwaza kwamba Baba yangu alifanya KOSA kutokutuachia mali za kurithi...... NEVER
Malezi na elimu aliyonipa ilitutosha kabisa watoto wake wote kujimudu kimaisha

Haya ndio maisha ya waTz kwa kiasi kikubwa na haswa watumishi wa umma, urithi pekee wa MALI wanaoweza kuuacha ni nyumba gari na mashamba tu

Mkuu mtu hachagu pa kuzaliwa, ukijikuta umezaliwa na baba kuli mbeba mizigo kariakoo au konda au bodboda usipoteze muda kumlaumu baba yako kwasababu mfumo wa dunia unafanya lazima wawepo wafanya kazi hizo, nijukumu lako kupambana badala ya kutaka baba yako angekua kama Baba yake Mo Dewji aliemrithisha mwanae mabilioni

Na ondoa kabisa fikra kwamba eti kuli huyo hana HAKI ya kuzaa watoto kwa sababu ya umasikini wake...... maisha hayajawai kuwa fair hayapo fair na hayatakaa yaje kuwa fair kama tunavyotamani yawe

Hata kwa mujibu wa hekaya za Bibilia masikini walikuwepo na walitajwa kama wacha Mungu, wengine walikua watumwa na vijakazi kwa manabii, wengine walitoa senti zao za mwisho na sadaka zao zikawa kubwa kuliko matajiri nk nk

So kama wewe unapigania maisha ili wanao waje kurithi mali ni jambo jema pia...... lakini hii ni ngumu kwa watu wengi kama konda, bodaboda, shamba boy nk.
Lakini kwa walio wengi ni malezi elimu na kumrithisha spirt ya kupambania maisha yake kwa sababu wengi pia wanarithi mali ambazo zinakuja kuyayuka na kuja kuishi kwenye ufukara mbaya zaidi pengine kwasababu hawakuandaliwa kupambana
 
Sisi hatuzai bhana tunafyatua kazi inayobaki ni kumwagilia maji tu tukiwasubiri watawala siku moja bomu lilipuke sijui wayajificha wapi
 
Alafu Wanawake mpunguze ujinga kuna Manzi nilimfukuzia Mwaka Jana akanitolea cha mbavu tena Maneno makali Mno angekua mtu mwingine angejipiga kitanzi na kuchukua maamuzi magumu ya kujitoa Uhai, sasa basi siku zimeenda Manzi namshangaa amerudi kwangu na speed ya rocket jet yaan ananiganda km ruba katika kumdadisi kumbe alikua na lijanaume huko wameendelea na mahusiano sasa sijui km kamfanyaje sasa hivi anauguza kidonda cha Siri ambacho anashindwa kumueleza hata Mama yake Mzazi sababu ni Jambo la aibu, now anaanza kuniganda Mimi nimfichie aibu, hivi huyu mtu alinikataa tena kwa Maneno makali namkumbusha anasema hakumbuki, hivi nyie Wanawake hua mnafikiri kabla ya kutenda kweli? Demi Kalpana Kapeace binti kiziwi Midekoo
Huyo jamaa kamfanyeje uko sisirini.
 
kwaiyo sasa bosi mbona haujasema yupi kati ya hao uliowatag apo ndo ana kidonda sirini? au basi nimekumbuka hayanihusu.
 
Back
Top Bottom