Watoto kuimbishwa nyimbo za kuwasifu Wanasiasa si sawa, huenda wakikua watajutia kama nilivyojuta

Watoto kuimbishwa nyimbo za kuwasifu Wanasiasa si sawa, huenda wakikua watajutia kama nilivyojuta

Mawele

Senior Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
119
Reaction score
320
Wakati nipo shule ya msingi miaka iliyopita nilichaguliwa kushiriki paredi na kuimbisha nyimbo kwenye paredi hiyo, nakumbuka mpaka leo nyimbo zile, nyingi zilikuwa za kumpigia chapuo Rais fulani kwani ilikuwa karibu na uchaguzi japo nimekuja kutambua shughuli ile vizuri baad ya kukua, kw wakati ule sikujua maana yake, nimejua ile shughuli hata haikuwa inamuhusu Rais ila ndio ivyo tuliimbishwa na walimu wale waliokuwa wanatufundisha tukiwa tumekusanywa kutoka shule mbalimbali

Nyimbo zile zilijaa sifa na shukurani kwa Rais, Masikini mie niliimba kwa madaha, huku nikisisitizwa kutia mbwembwe nami nikafata bila kujua nachoimba ni nini au kina matokeo gani kwa Taifa langu kumbe nashawishi watu kuona kiongozi yule ni bora wakati hata sijui nini maana ya uongozi kwa mustakabali mzima wa taifa.

Nilikuja kujutia sana baada ya kuja kusikia na kuona namna matendo yaliyofanyika kwenye utawala wa kiongozi yule, wakati najitambua alikuwa mbioni kumaliza miaka 10, nakuja kujua mambo ya ufisadi, rushwa, nk kwenye utawala wa Rais ambaye miaka kadhaa nyuma niliimbishwa kumsifu, nilijutia nikatamani siku zirudi nyuma nikatae kuwa sitashiriki kwenye paredi hiyo.

Nimeyakumbuka haya baada ya kuona watoto wakiimbishwa nyimbo za kusifia viongozi kwenye maadhimisho mbalimbali huku wakiwasifu viongozi kwa kufanya hiki na kile ambacho naamini hata hawajui maana yake ni nini naamini kabisa hawajui walitendalo ila wanatendeshwa vitu ambavyo pengine wangejitambua na kuwa na maamuzi huenda wasingekubali.


.
 
Back
Top Bottom