John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Watoto Kuwatii Wazazi kwa Namna Gani
Maandiko Yanasemaje
1. Katika Wakolosai 3:20, maandiko yanasema: "Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana".
2. Lakini katika Luka 14:26, Yesu alisema: "Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu".
3. Pia, katika Waefeso 6:1, Biblia inasema:
"Enyi watoto, watiini wazazi wenu 'KATIKA BWANA', maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia".
Ufafanuzi kuhusu maandiko
Tunapaswa kuwatii na kuwaheshimu wazazi, lakini kuna mambo muhimu ya kuzingatia. Kwanza, utii ambao hautokani na Mungu. Pili, utii unaochukua nafasi ya Mungu. Huo ndio utii Kristo alioukataa.
Kuhusu utii usioendana na Mungu
Kwa mfano: unakuta mzazi ni mshirikina, halafu anataka kukufundisha na wewe mtoto kuwa mchawi. Au mzazi ni mlevi anataka na wewe uwe mlevi. Au mzazi anafanya biashara haramu anakulazimisha na wewe ufanye biashara haramu.
Kwa hali hiyo, biblia imeruhusu kutokutii na siyo dhambi mbele za Mungu, kwa vile inakuharibia mahusiano yako wewe na Mungu. Zingatia mstari katika Waefeso 6:1 hapo juu, unaosema watiini wazazi wenu "katika BWANA". Kwa hiyo ulevi, uchawi, ufisadi, uasherati, uuaji, n.k. siyo mambo katika Bwana. Hivyo kwa kukataa kushirikiana na mzazi, Mungu hatahesabu kama hukumtii mzazi, japo yeye mzazi ataona kama hukumtii.
Kuhusu utii unaotaka kuchukua nafasi ya Mungu
Kwa mfano: mzazi anakuzuia wewe usimpokee Kristo, anakuzuia usiombe, anakuzuia usitende matendo mema. Au anakuzuia usiitii sauti ya Mungu, kwa mfano pale Mungu anapokuambia acha kufanya jambo fulani lakini mzazi hataki. Katika hali hiyo, huna budi kutupa chini ya mzazi na kuchukua ya Mungu, hata kama mzazi ana maana nzuri kiasi gani kwako. Hapo ndipo Bwana Yesu aliposema: ASIYEMCHUKIA baba yake au mama yake, hawezi kuwa mwanafunzi wangu katika Luka14:26: “kama mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake,na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; na naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu".
Hapa ndipo wengi wanapokwamia. Unakuta Bwana amemuita mtu atoke katika imani fulani ya uongo inayoabudu sanamu, ili amtumikie katika roho na kweli, lakini kwa sababu wazazi wake na ndugu zake ni washirika wazuri katika hiyo imani, anaamua kuwafuata wazazi wake kwa hofu kwamba atakuwa hajawaheshimu wazazi wake. Kumbuka Yesu alisema, adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe. Hivyo, huo ndio wakati wa kubeba msalaba wako na kumfuata Kristo.
Aidha, zingatia andiko la Mathayo 10:32-38: "Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. 33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni. 34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani bali upanga. 35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; 36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. 38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili".
Hivyo, Mungu anapokuita hamaanishi kwamba anataka kukuletea maafa wewe katika familia yako au kati ya ndugu zako. La hasha. Lakini mwanzo lazima mafarakano yawepo kwa sababu hutaeleweka, lakini mwisho wake huwa mzuri.
Kwa wewe kumtii Mungu, utawapata na ndugu zako. Lakini usidhani kwa kuwatii wazazi wako ukamuweka Mungu pembeni, ndiyo umewaokoa wazazi wako, Hapana. Kinyume chake, hapo utaipoteza roho yako pamoja na zao lako.
Mfano mzuri kuhusu mtoto na wazazi kufarakana ni pale ambapo Bwana Yesu Kristo alionekana amerukwa na akili kwa ajili ya Mungu. Watu wa nyumbani mwake hawakumuamini. Maandiko ya Yohana 7:5 na Marko 3:21 yanasema: "Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili". Lakini tunaona kwa kumtii kwake Mungu, watu wa nyumbani mwake walikuja kuokolewa pamoja na dunia nzima. Kama Bwana hakuona haya, kuonekana amerukwa na akili, je, inatupasaje sisi?
Muhimu ni mtoto kuwa na ufahamu kuhusu neno la Mungu, na kufanya lililo sahihi, bila kujali wasemalo wazazi. Katika kufanya hivyo, atakuwa ameokoa roho yake. Aidha, katika kufanya hivyo, busara itatumika.