Watoto wa Cleopa Msuya watinga mahakamani kugombea mali

Watoto wa Cleopa Msuya watinga mahakamani kugombea mali

Mkuu, nadhani hapa unapaswa kuangalia kwa kina kabla ya kuhukumu na kusema 'ubinafsi unatumaliza.' Naruhusiwa kuweka disclaimer hapa kwa sababu namfahamu binafsi mtoto wa kwanza wa Mzee Msuya, yaani George Msuya, na nimeshafanya naye kazi miaka ya huko nyuma. Nakuhakikishia kwa asilimia mia moja, hawa watoto wako tofauti sana na wale watoto wa viongozi wengine tunaowajua sisi ambao baba zao walishika madaraka makubwa kama ya huyu Mzee.
Hawa si watoto wa 'kuhongwa' magari, kuishi kwa uvivu, au kufuja mali wakitegemea jina la baba yao. Mzee Cleopa Msuya alisifika kwa kusomesha watoto wake na kuhakikisha kila mmoja anasimama kwa miguu yake kitaaluma na kuwa na maisha yake ya heshima:
  • George Msuya – Mtoto wa kwanza, ni Mhandisi (Engineer) mbobezi na mwenye weledi wa hali ya juu kwenye kazi zake.
  • Dr. John Msuya – Mtoto wa pili, ni Daktari wa Binadamu (Medical Doctor) mwenye taaluma yake ya heshima.
  • Dr. Joyce Msuya Mpanju – Mtaalamu wa masuala ya mazingira na microbiology, aliyefikia hadi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP na sasa ni Afisa Mwandamizi wa ngazi ya juu kabisa Umoja wa Mataifa (UN).
  • Job Msuya – Naye pia ni Mhandisi (Engineer) anayejiheshimu.
  • Naanjela (Angela) Esther Msuya – Mtaalamu mbobezi wa ukaguzi wa mifumo ya TEHAMA (IT Systems Audit).
    (Kumbuka mtoto mwingine, Geofrey Msuya, alitangulia mbele ya haki tangu mwaka 2005).
Mkuu, watu wenye akili hizi, wasomi wa kiwango hiki, na wenye kazi zao kubwa hawawezi kwenda mahakamani kwa 'ubinafsi wa njaa' au 'kutawanya mali'.
Kisheria na kiungwana, kwenda mahakamani kupinga usimamizi wa mirathi sio ugomvi wala sio uharibifu; bali ni kutafuta tafsiri sahihi ya kisheria na kulinda mali zisipotee. Kwenye shauri hili la sasa, Job Msuya alienda mahakamani kuomba amri ya kulinda mali (kama vile nyumba ya Upanga) kwa sababu aliona wasimamizi wenzake wanafanya maamuzi bila ridhaa ya pamoja. Huku si kutawanya, bali ni kulinda mali isiyuzwe kienyeji au kwa bei ya chini chini chini ya kiwango.
Hawa watoto wana fedha na kazi zao. Wanachofanya sasa ni kusimamia taratibu zilizonyooka ili kile alichokiacha baba yao kibaki salama na kigawanywe kwa haki na uwazi. Wangekuwa hawajasoma au hawana akili, wangesafiri na mapanga au kurogana, lakini kwa sababu wameelimika, wametumia chombo halali cha sheria ambacho ni Mahakama Kuu.
Tusiwalaumu watoto kwa kutumia akili na sheria kulinda urithi wao!
Mpaka suala linapelekwa mahakamani ina maana wameshindwa kukubaliana, kushindwa kukubaliana tafsiri among them wako ambao 'hawajanyooka' katika kusimaia na kuendesha mali za urithi wa baba yao.
Si rahisi kufahamu sababu za 'baadhi' ya ndugu kwenda kinyume na taratibu zinavyopaswa kuwa na kutokukubaliana na ndugu wengine mpaka kupelekea suala kupelekwa mahakamnani lakini it's obvious kwamba there is a big fracture among those family members.
Pamoja na kwamba ni njia halali kupeleka suala hilo mahakamani but isn't it tarnishing the image of their family, hapa lawalama zipelekwe kwa waliogoma kukubaliana na wenzao mpaka kusababisha suala kupelekwa mahakamani.
Mtu anayepeleka suala mahakamani ina maana amekosa kupata suluhu/haki katika ngazi ya familia, it's obvious that some are bullying others.
 
huu ndio upuuz wa kuishi bila kuacha wosia. andikeni wosia wazee kifo ni maumbile lazima utakufa. hapo ungekuta.kila mtu anakufa na chake.
Wosia hausaidii, kama una mali gawa mapema wewe uwe kama serikali, ukiwa hai mali ni za kwako unasimamia na kuzifaidi huku uliyempa akizilinda na kujitahidi kuziendeleza kupitia kwako na Kila mtu anakuwa anaona. Ukifa Kila mtu anaendeleza alichopewa, hapo hakuna ugomvi.
 
Familia tajiri huacha migogoro kwa wanafamilia, tofauti na familia masikini huacha madeni ya mazishi
Bora uachiwe mgogoro wa mali unajipa moyo hutatoka mikono mitupu sasa wewebuachiwe madeni ya mazishi yaani mtu ameshakufa wewe huku unaangaika kulipa deni lake changamoto sana..
 
Mkuu, nadhani hapa unapaswa kuangalia kwa kina kabla ya kuhukumu na kusema 'ubinafsi unatumaliza.' Naruhusiwa kuweka disclaimer hapa kwa sababu namfahamu binafsi mtoto wa kwanza wa Mzee Msuya, yaani George Msuya, na nimeshafanya naye kazi miaka ya huko nyuma. Nakuhakikishia kwa asilimia mia moja, hawa watoto wako tofauti sana na wale watoto wa viongozi wengine tunaowajua sisi ambao baba zao walishika madaraka makubwa kama ya huyu Mzee.
Hawa si watoto wa 'kuhongwa' magari, kuishi kwa uvivu, au kufuja mali wakitegemea jina la baba yao. Mzee Cleopa Msuya alisifika kwa kusomesha watoto wake na kuhakikisha kila mmoja anasimama kwa miguu yake kitaaluma na kuwa na maisha yake ya heshima:
  • George Msuya – Mtoto wa kwanza, ni Mhandisi (Engineer) mbobezi na mwenye weledi wa hali ya juu kwenye kazi zake.
  • Dr. John Msuya – Mtoto wa pili, ni Daktari wa Binadamu (Medical Doctor) mwenye taaluma yake ya heshima.
  • Dr. Joyce Msuya Mpanju – Mtaalamu wa masuala ya mazingira na microbiology, aliyefikia hadi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP na sasa ni Afisa Mwandamizi wa ngazi ya juu kabisa Umoja wa Mataifa (UN).
  • Job Msuya – Naye pia ni Mhandisi (Engineer) anayejiheshimu.
  • Naanjela (Angela) Esther Msuya – Mtaalamu mbobezi wa ukaguzi wa mifumo ya TEHAMA (IT Systems Audit).
    (Kumbuka mtoto mwingine, Geofrey Msuya, alitangulia mbele ya haki tangu mwaka 2005).
Mkuu, watu wenye akili hizi, wasomi wa kiwango hiki, na wenye kazi zao kubwa hawawezi kwenda mahakamani kwa 'ubinafsi wa njaa' au 'kutawanya mali'.
Kisheria na kiungwana, kwenda mahakamani kupinga usimamizi wa mirathi sio ugomvi wala sio uharibifu; bali ni kutafuta tafsiri sahihi ya kisheria na kulinda mali zisipotee. Kwenye shauri hili la sasa, Job Msuya alienda mahakamani kuomba amri ya kulinda mali (kama vile nyumba ya Upanga) kwa sababu aliona wasimamizi wenzake wanafanya maamuzi bila ridhaa ya pamoja. Huku si kutawanya, bali ni kulinda mali isiyuzwe kienyeji au kwa bei ya chini chini chini ya kiwango.
Hawa watoto wana fedha na kazi zao. Wanachofanya sasa ni kusimamia taratibu zilizonyooka ili kile alichokiacha baba yao kibaki salama na kigawanywe kwa haki na uwazi. Wangekuwa hawajasoma au hawana akili, wangesafiri na mapanga au kurogana, lakini kwa sababu wameelimika, wametumia chombo halali cha sheria ambacho ni Mahakama Kuu.
Tusiwalaumu watoto kwa kutumia akili na sheria kulinda urithi wao!
Pamoja na usomi wote huo wameshidwa nini kuyamaliza kindugu badala ya kukimbilia mahakamani? Kama kuna mmoja hashirikishwi ametafuta sababu ya kutoshirikishwa ni nini? Huko kote ni kukosa hekima na busara. Na hapa ndipo inadhihirisha kwamba unaweza kusoma lakini ukashindwa kuelimika, kama George ndiye chanzo cha kutomshirikisha mdogo wake kwenye mambo makubwa kama haya basi hajaelimika! Yaani mko watano na mmesoma vizuri mnashindwaje kuelewana?
 
tugawane kila mtu afe na chake
Issue ni kwamba watoto hawafanani unaweza ukawa na watoto 10 mwenye akili ya utajiri ni mmoja tu wengine wote wana akili za kimasikini tu sasa hao wenye akili za kimasikini ndio wanaoleta usumbufu mara anataka auze nyumba mara anataka auze mifugo mara anataka auze viwanja yeye ni kuuza tu sio kuendeleza, sasa hawa wenye akili za hivi ndio wanaowasumbua wenzao kwenye familia baada ya msiba kutokea ooh tuuze nyumba kila mtu apate chake ooh tuuze shamba kila mtu apate chake

Mfano;
Kuna wana familia waliachiwa Shamba kubwa na Mzee wao basi lile shamba wakawa wanalima kwa kupokezana mwaka huu analima huyu mwaka unaofuata analima mwingine hivyo hivyo, sasa kuna wengine wakawa hawanufahiki ambao wana akili za kimasikini sababu walikua wanapata mazao kidogo wakati wenzao wakilima wanapata mazao mengi na shamba linawanufaisha sana wanapata maendeleo ukatokea mgogoro na mvurugano ikaibuka ile kauli ya basi tukose wote tuliuze lile shamba wakakatiana vipande wakaliuza, sasa hivi wote wamebakia mikono mitupu kabisa hela haipo wameshakula na shamba halipo tena wameshaliuza
 
Huyu Mpanju nilidhani miaka yote kuwa ni Mhaya! Au kuna Mpanju mwingine, na atokee kupitia kwenye nafasi hizo hizo ulizotaja?

Mzee baba hiyo Mpanju hapo mbona iko straight kuwa huyu ni Mrs Mpanju...
 
Hawa viongozi wa juu si wanakuwa na mali za kutosha ambapo mgawanyo unakuwa mzuri kwa watoto 3 kuridhika?
Inawezekana labda shida unakuta kuna nyumba ipo Masaki ambapo kila mmoja anaitolea macho nani afanye kurithi
 
Mtu yeyote msomi / familia ya wasomi haya mambo kugombea Mali za mzee utasikia kwa familia za mafukara wa AKILI (maskini wa akili) hakuna UMASKINI mbaya kama UMASKINI wa MAARIFA

NB. SISI MZEE ALITUPA ELIMU TENA AKASEMA HATA TUSIPO MSAIDIA KWA CHOCHOTE ATLEAST TUWEZE KUJIMUDU KABLA HAJAFA ALIHAKIKISHA MALI KAZIGAWA KWA ALIO WAPENDA FULL STOP

KILA SIKU HUWA NAZUNGUMZA NA WEWE KWENYE ULIMWENGU WA ROHO NAMISS CALL ZAKO

KILA LEGACY YAKO IPO VYEMA WALA HATUJAGOMBANIA CHOCHOTE ZAIDI YA KUWA WAMOJA NA KUKUENZI DAIMA

ATLEAST MIMI NA NDUGU ZANGU TULIKUA NA BABA... BABA AMBAE NIKIJARIBU KUWA BABA BORA KULIKO YEYE VIATU VINAPWAYA PUMZIKA MZEE WANGU
Elimu haisaidii ,elimu ndiyo chanzo cha ubinafsi na kupelekana mahakamani...Ni lazima muwe na akili wa kujitambua ,elimu inafundisha ubepari.

Ina maana hawa watoto hawajasoma🤣🤣
 
Hapa ni engineer TU wanawaza wasiwe na njaa, nikuhakikishie TU huyo daktari, sijui mkaguzi wa tehama Wana njaa TU , na huenda bila mirathi ya baba yao wangekuwa sakala flani, ila nimependa mzee kafa na watu wanagombania Mali zako Ina maana ulitimiza wajibu wako duniani , mzee angejua angezaa watoto na wanawake tofauti tofauti isingeleta shida Kwa sababu kabla hujafa unandika mirathi sababu unajua ukifa TU Kuna ******* watauana kisa Mali zako
Unawajua?
 
Back
Top Bottom