Watoto wa Kiafrika wamekuwa wakiaminishwa kuwa mahusiano ni kama kosa na ni kitu cha siri

Professor jr

Member
Joined
Apr 24, 2019
Posts
30
Reaction score
29
Watoto wengi wakiafrika wamekuwa wakiamini kuwa mwenye mahusiano ni kama kosa na ni kitu kinacho takiwa kufanywa kama siri .Nadhani wazizi wengi wengi wamechangia kufanya watoto wawe hivyo ukali na kutojari hisia za watoto toka wadogo .

Lakini tofauti na wenzetu wazungu mtoto toka mdogo amekuwa akiona mahusiano kuwa ni jambo la kawaida hvyo Imekuwa swala la kawaida kwao pia imewajengea kujiamini pia kuwa na mahusiano yanayo dumu mda mrefu maana wengi hujikuta wapo kwenye mahusiano toka udogoni na hata familia zao zina ukaribu.

Madhara ya kutokujua mahusiano toka wadogo

1.Mwisho wa siku tumetengeneza kizazi cha watoto malaya ambao wamejificha kwenye mahusiano kuwa ni siri na kujikuta wopo kwenye mahusiano ya watu wengi kisa ni siri .

2.Tumetengeza ndoa nyingi zisizo dumu;ndoa nyingi hazidum maana watoto wengi wamejikuta wakianza kuwa huru na mahusiano wakiwa wakubwa na hasa wakifika chuo hivyo kukosa hata ile ukaribu sana wa kumjua mwenza wake kabla hawajaoana.

3.Watoto wengi wanakosa emotional intelligence;vijana wengi siku hizi yamekuwa wajinga na limbukeni wa mapenz wameshindwa kuhimili hisia zao hata kujicontrol mwisho wa siku wameishia kuteseka na mapenz lakn kama wangepata uelewa wa mahusiano toka wadogo ingekuwa nzur

Mwisho kabisa napenda kushauri wazazi tujaribu kukufundisha watoto wetu elimu hii ya mahusiano itasaidia sana mfano wapi ulijifunza kuhusu ngono ,ulijifunzia kwa kuangalia porno nadhan mtu akikosea kujifunza kitu inakuwa ngumu kujifunza tena mzazi unatakiwa kufundisha wanao kila kitu kabla ulimwengu haujamdanganya.

Kuwa kwenye mahusiano siyo kosa na wala siyo dhambi tena inasaidia kujenga mahusiano mzur unatengeneza kujiamin na inanifanya mtu kuwa romantic and emotional intelligent.
 
Tatizo ni UTAMADUNI, utamaduni wa Wazungu na wakwetu ni tofauti kabisa, ni kama kusema Wazazi wa kibantu (Baba na Mama) waende ufukweni kuogelea na vichupi mbele ya watoto wao wa kuwazaa

Au Mtoto wa kike amuapproach Mwanaume kumtongoza na amtake amuoe

Kwa huku kwetu ni vigumu tangu enzi, ila kwa hao wazungu ni jambo la kawaida sana, na huu ugumu wetu una faida zake na hasara kidogo.
 
Mwisho kabisa napenda kushauri wazazi tujaribu kukufundisha watoto wetu elimu hii ya mahusiano itasaidia sana mfano wapi ulijifunza kuhusu ngono ,ulijifunzia kwa kuangalia porno nadhan mtu akikosea kujifunza kitu inakuwa ngumu kujifunza tena mzazi unatakiwa kufundisha wanao kila kitu kabla ulimwengu haujamdanganya.
Ndiyo maana kuna baadhi ya makabila au sijui niseme mila bado wanaendeleza mambo ya Unyago
 
Tatizo ni UTAMADUNI, utamaduni wa Wazungu na wakwetu ni tofauti kabisa, ni kama kusema Wazazi wa kibantu (Baba na Mama) waende ufukweni kuogelea na vichupi mbele ya watoto wao wa kuwazaa

Au Mtoto wa kike amuapproach Mwanaume kumtongoza na amtake amuoe

Kwa huku kwetu ni vigumu tangu enzi, ila kwa hao wazungu ni jambo la kawaida sana, na huu ugumu wetu una faida zake na hasara kidogo.
Lakini hili ni zuri sana tukiiga imagine asking your child who is ur girlfriend anaeleza jinsi anafeel na unamuelekeza nini afanye it have got no negative impact
 
Sawa lakini pia inategemea na mindset za Mtoto, kama hayupo strong na hakuna guardians wazuri kama Wazazi huyo Mtoto atapotea tu

Changamoto nyingine Wazazi au walezi wengi wa kiafrika hawana utamaduni wa kukaa muda mrefu na watoto wao na kuzungumza nao kwa Uhuru hasa kuhusu Mapenzi na Mahusiano
 
Watoto wengi wakiafrika wamekuwa wakiamini kuwa mwenye mahusiano ni kama kosa na ni kitu kinacho takiwa kufanywa kama siri .Nadhani wazizi wengi wengi wamechangia kufanya watoto wawe hivyo ukali na kutojari hisia za watoto toka wadogo .
Kinachoogopwa ni mimba za utotoni. Wenzetu dawa na zana za kuzuia mimba ziko kila mtaa na hujua kuzitumia vilivyo. Sisi huku kwetu utamfundisha juu ya mahusiano ila hutakuwa na nyenzo zote za kukabili matokeo hasi ya mahusiano hayo.
 
Tatizo ni UTAMADUNI, utamaduni wa Wazungu na wakwetu ni tofauti kabisa, ni kama kusema Wazazi wa kibantu (Baba na Mama) waende ufukweni kuogelea na vichupi mbele ya watoto wao wa kuwazaa

Au Mtoto wa kike amuapproach Mwanaume kumtongoza na amtake amuoe

Kwa huku kwetu ni vigumu tangu enzi, ila kwa hao wazungu ni jambo la kawaida sana, na huu ugumu wetu una faida zake na hasara kidogo.
Sio kweli. Tamaduni zetu zinatoa mafunzo ya mahusiano (unyago kwa watoto wa kike na jando kwa wakiume). CCM na wadau wake wakapiga marufuku hayo mafunzo.....

Sijui kama unajua hilo?
 
Lakini hili ni zuri sana tukiiga imagine asking your child who is ur girlfriend anaeleza jinsi anafeel na unamuelekeza nini afanye it have got no negative impact

Mbona umeishia kwenye ”who’s your girlfriend…” tu, balansi mzani kwa kuuliza na ile jinsia pendwa![emoji2957]
 
Back
Top Bottom