Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Nilipoanza form one nikawa busy na masomo ila nilibaki kuwa mshabiki tu mpira, isitoshe nilikutana na wababe wa mpira jambo ambalo lilinifanya niachie nafasi watu waoneshe viwango vyao.

Jinsi muda ulivyozidi kwenda hadi kufika Advance nikaacha kushabikia kabisa mpira hadi sasa hivi, mpira sina time nao kabisa
Haaaa....world cup 98 kuna dogo aalikuwa anaipenda sana Brazil...ilipotolewa dogo akawa analia Huku anarudi nyumbani. Kumbe home kwao walikuwa wanamtafuta mpaka wamechoka ....akafika home na machozi ya Brazil ....wakamuuliza unalia nini...eti mpira dogo alipigwa sana lakini hakuacha kutizama....
 
Ila mkuu, goli 20? mlikuwa mnacheza na wasichana au mabonge?
Tushaanza kuwaona ambao hawajapitia haya maisha...huu mchezo ilikua mnaweza anza saa nane baada ya kutoka class mpaka giza liingie,..ka weekend ndo mnaweza cheza asubuhi mpaka jioni.
 
Tushaanza kuwaona ambao hawajapitia haya maisha...huu mchezo ilikua mnaweza anza saa nane baada ya kutoka class mpaka giza liingie,..ka weekend ndo mnaweza cheza asubuhi mpaka jioni.


Taratibu kijana..
Aisee hata kama mpira upo damuni utacheza weee mwishowe unahitaji kwenda kukamua ng'ombe...waliokuwa wanafikisha magoli 20 ni wale ambao kwao walikuwa na wafanyakazi (mliokulia mjini).

Na nikisema hivyo bado hutanielewa maana leo ukifika maeneo ya Ngangamfumuni (Moshi, KLM) pamekuwa mjini kabisa hata mimi mwenyewe huwa siamini.

Narudia tena taratibu na kauli zako...
 
Hakunaga kuumia halafu mechi lazima ichezwe wakati wa jua kali la saa 4 hadi 10 jioni Kudadeki.Wanaokumbuka Jasho linafananaje waseme
 
Me kuna siku nilifunga magoli 75!
Halafu kuna ile kitu inaitwa tobo, ukipigwa tobo aisee ilikuwa unakimbizwa, ukikamatwa unakula kisago...ponea yako ilikuwa unapaswa ukimbie hadi ushike kisiki au mti uliopangwa!
Magoli 75..!? Mlikua mnacheza mdako nyie sio mpila
 
nakumbuka kiwanja chetu cha mtaa kilichukuliwa na wakubwa kwa mda baada ya uwanja wao mkubwa kuchukuliwa kufanyiwa mikutano ya kidini pande za kawe home,, sasa wakawa wanatunyanyasa kila ikifika saa kumi tu, wanakuja kutufukuza wacheze wao.. tukaunda tume ya kuwaondoa hawa ma bro,, tukakubaliana twende beach tukachukue mbigili za kutosha tukazimwage uwanja mzima mpaka magolini.. tukaenda tukajaza mifuko na mifuko, tukazimwaga usiku zote,,, kimbembe kesho yake, wakubwa wanakuja kucheza hawajatukuta wakaona mtelezo,, sie tumekaa tunawaangali tu,, maana wengine walikua na viatu wengine hawana,, wengine walioanguka wanakutana nazo,, mpira haukuchezeka siku hiyo, wakaanz kutusaka tukazoe miba tuliyoimwaga uwanja mzima. hakuna aliyekubali kama kamwaga mbigili.. na wao ndo ikawa mwisho wao kucheza pale wakahamia uwanja mwengine,, vijana tukarudi tukaanza kuzitoa mojamoja japo hatukuzimaliza,, ila shuhuli nasi ilitupata ya kuchomwa nazo maana hatukuzimaliza,, zilikuja kuisha kwa kutuchoma, unaiokota unaenda kuitupa..
Aaaaaaaaahahah nyie mlipaswa muwe marekani maana sio kwa vizuizi hivyo asee hahaha hvo ni vizuizi vya kimataifa
 
Tunachanga hela tunanunua Kondomu 70 tunachukua tatu tunafuma! Mpaka zinaisha hapo hsta gozi cha mtoto.. Usipochanga no kucheza na ukiingia kinguvu watu wanasema KINYAMA HICHO basi ukigusa mpira unarukiwa mabuti na rafu za kufa mtu mwisho unarud nje
Aahah hako kamsemo ka kinyama hichoo aseee ukiitiwa hivyo ni bora hata usepe maana hata ukikaa nje ya uwanja wahuni wanakufata na kukuchezea rafu
 
Hiki cheo nilikitumia kwa uaminfu mkuu..kuna siku nimeingia sculi j3 kaptula imejaa mafuta ya maandazi weekend ckufua....nikamwita RAIA mmoja nkamwambia anipe ya kwake alaf namfuta jina LA wasumbufu. Axee mstarini kwenye ukaguzi alichapwa za kutosha mwili mzima mtaalamu nimetulia tuu
Dah vitisho kumbe vimechipukia huku?? Aaahahaha st kayumba mwalimu asee
 
sasa huo mpira kuna watu hawajui mpka leo unafumwa kwa kamba za aina gn
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nilikuwa nacheza mpaka kiza kinaingia. Nilionywa sikusikia maana tuliambiwa kurudi nyumbani mwisho saa 12. Baba akanichoka. Siku moja nafika home baba kanichukua na kuniweka ndani ya pipa la maji ya baridi(mwezi wa saba nyanda za baridi) Nilikaa mle meno yakigongana. Mama (bless you mama) kapiga magoti kuniombea msamaha. Baba kagoma, huku akiniangalia na kuvuta sigara yake sport. Sitasahau ila sikukoma.
 
Nakumbuka tu nilikuwa mkali wa kupiga madochi mpaks mpira unafumuka .......lakini baadae nliacha mpira sabab wakati wa kugawa wachezaji mpo kati kati ya uwanja mm nlikuwa wa mwisho kuchukuliwa ( kila timu hainitaki) yaani kila kapteni anasema "na huyo mchukueni tunawapa!" yaani baada ya hapo ugusishwi pasi hata moja....hahahah
 
Nimefuma sana vinyenga,Nimechimba sana hadi dore gumba muonekano wake ni shida. Na miss sana. Viwanja vile magorofani,mahakamani airport,nonde,mwenge,muungano,sangu dah!watoto wa siku hizi wao na memory hata hawachezi
 
Back
Top Bottom